Mbeya: Zaidi ya Mawakili 100 wamejitokeza kuwatetea Dkt Slaa na Wenzake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa kutoka kwa Phillipo Mwakilima Wakili wa Watuhumiwa wa Uhaini , inaeleza kwamba zaidi ya Mawakili 100 wamejitokeza kumtetea Dkt. Slaa na wenzake kwenye kesi ya uhaini inayowakabili.

Tayari wengine wamekwishaanza kuripoti Mkoani Mbeya kwa ajili hiyo .

---

Your browser is not able to display this video.
Zaidi ya mawakili 100 kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo TLS wanatarajia kuungana na mawakili watatu kumtetea Balozi Dk Willibrod Slaa na wenzake wawili katika kesi ya uahaini wanayotuhumiwa nayo.

Akizungumza nje ya Mahakama Wakili Philip Mwakilima anayewatetea Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali amesema mawakili hao wameshaanza kuwasili Jijini Mbeya kwa ajili ya kesi hiyo.

Hata hivyo watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya ikiwa ni siku ya nne bila kufikishwa mahakamani kwa kesi ya uhaini wanayotuhumiwa nayo.

Mwakilima amesema kwa mujibu wa sheria watuhumiwa walipaswa kufikishwa mahakamani leo lakini hawajafikishwa na wanakusudia kufungua kesi kwa lengo la kuiomba Mahakama imlazinishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwafikisha mahakamani au kuwaachilia endapo watabaki wakiwashikilia.
 
Great news
 
Unamwacha kicheko akufundishe kuongiza unategemea mazuri mzee yule anachojua ni kuchekacheka tu
 
Copy: TLS

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…