KERO Responded Mbezi Beach na Salasala tunauziwa maji Tsh 1,500 hadi 2,000 kwa dumu, Viongozi husika mmeridhika na hali hii kila Mwaka?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa siku kadhaa nimekuwa nikinunua maji kwa Sh 2,000 kwa dumu nikiwa Salasala nimempigia na rafiki yangu yupo Mbezi Beach kwa Komba changamoto ni hiyo hiyo. Hali hii imenifanya nihisi kama inanifilisi, nikalazimika kuamua kufuata maji mwenyewe japo kwenye jua kali. Nimezunguka mtaa mzima bila mafanikio; maeneo mawili tu niliyopata maji, nayo yalikuwa ya chumvi.

Nikaelekezwa kufika eneo la Jogoo, karibu na ofisi ndogo yenye mitambo ya DAWASA. Nilipofika, maji yalikuwa yanauzwa Tsh 500 kwa dumu, lakini kulikuwa na watu wengi waliokesha na madumu na ndoo zao wakisubiri maji. Naambiwa kuwa hayo ni maji ya DAWASA, lakini bei ni Tsh 500 kwa dumu au ndoo kubwa, na Tsh 300 kwa ndoo ndogo.
Kwa kweli, hali hii ikiendelea, wakazi wengi wa Dar es Salaam tuko kwenye hatari ya kufilisika. Fikiria kununua maji kwa Tsh 500 bila hata kujumlisha gharama ya usafiri. Akina mama na watoto saa 11 alfajiri wanakimbizana na ndoo wakitafuta maji na mengine ni ya chumvi.

Najiuliza kama viongozi wanafahamu ukubwa wa changamoto hii. Kwa sasa mambo hayaendi sawa; kila ukifikiria changamoto ya maji, moyo unakosa amani. Wananchi tunateseka sana hasa kipindi cha jua kali.

Wametoa taarifa kwamba baadhi ya maeneo maji yatanza kutoka lakini ukifuatilia taarifa hiyo haina uhalisia katika utekezwaji wake maana maeneo mengi yaliyobainishwa hususani mwambao wa Tegeta na Madale maji hakuna.

Wito wangu kwa viongozi: tafuteni suluhu ya kudumu. Wananchi hatupaswi kuteseka hivi kila mwaka kana kwamba hakuna watu tuliowapa jukumu la kusimamia mipango kwa kutumia kodi zetu.
View attachment 3514871
View attachment 3514900
Mbezi Jogoo kuna mitambo ya maji ya Dawasa.​
Mabeberu wanatuonea wivu wamekata maji.
 
Wachimbe visima tu....

Hivi ule mradi wa kidunda uliishia wapi

Ova
 
Bahati mbaya sana, kwenye uchaguzi utakaofuata, chama kile kile ambacho kimeshindwa kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa miaka 60, kitakuja kuwaambia wananchi hao kuwa kitawalaetea maji kama mtamchagua mgombea wake. Na kuna wajinga wataamini.
 
Kwa siku kadhaa nimekuwa nikinunua maji kwa Sh 2,000 kwa dumu nikiwa Salasala nimempigia na rafiki yangu yupo Mbezi Beach kwa Komba changamoto ni hiyo hiyo. Hali hii imenifanya nihisi kama inanifilisi, nikalazimika kuamua kufuata maji mwenyewe japo kwenye jua kali. Nimezunguka mtaa mzima bila mafanikio; maeneo mawili tu niliyopata maji, nayo yalikuwa ya chumvi.

Nikaelekezwa kufika eneo la Jogoo, karibu na ofisi ndogo yenye mitambo ya DAWASA. Nilipofika, maji yalikuwa yanauzwa Tsh 500 kwa dumu, lakini kulikuwa na watu wengi waliokesha na madumu na ndoo zao wakisubiri maji. Naambiwa kuwa hayo ni maji ya DAWASA, lakini bei ni Tsh 500 kwa dumu au ndoo kubwa, na Tsh 300 kwa ndoo ndogo.
Kwa kweli, hali hii ikiendelea, wakazi wengi wa Dar es Salaam tuko kwenye hatari ya kufilisika. Fikiria kununua maji kwa Tsh 500 bila hata kujumlisha gharama ya usafiri. Akina mama na watoto saa 11 alfajiri wanakimbizana na ndoo wakitafuta maji na mengine ni ya chumvi.

Najiuliza kama viongozi wanafahamu ukubwa wa changamoto hii. Kwa sasa mambo hayaendi sawa; kila ukifikiria changamoto ya maji, moyo unakosa amani. Wananchi tunateseka sana hasa kipindi cha jua kali.

Wametoa taarifa kwamba baadhi ya maeneo maji yatanza kutoka lakini ukifuatilia taarifa hiyo haina uhalisia katika utekezwaji wake maana maeneo mengi yaliyobainishwa hususani mwambao wa Tegeta na Madale maji hakuna.

Wito wangu kwa viongozi: tafuteni suluhu ya kudumu. Wananchi hatupaswi kuteseka hivi kila mwaka kana kwamba hakuna watu tuliowapa jukumu la kusimamia mipango kwa kutumia kodi zetu.
View attachment 3514871
View attachment 3514900
Mbezi Jogoo kuna mitambo ya maji ya Dawasa.​
Dah!! Hakika poleni sana.
 
Utawasikia hii vita vya kiuchumi, sijui amani amani, tunaonewa wivu na rasimali, viongozi wa kitanzania wajinga sana.

Haya Msigwa, je mataifa ya nje watatuonea wivu kukosa maji?
 
Back
Top Bottom