Uchaguzi 2020 Mbezi beach Vs Mtoni Kijichi | Chagua CCM upate maendeleo chagua upinzani uendelee kusota

Uchaguzi 2020 Mbezi beach Vs Mtoni Kijichi | Chagua CCM upate maendeleo chagua upinzani uendelee kusota

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Hii kila mtu kichwani mwake kila mmoja na maamuzi yake kwenye box

MBEZI BEACH
Ila ni kwamba Mbezi beach,Tegeta maeneo ya Kawe yalionekana ya hadhi sana ukiangalia mpangilio na geografia ya maeneo hayo yamepangwa vizuri na hata ujenzi wa nyumba zake kidogo ni za hadhi ya juu. Katika pita pita zangu panavitia sana lakini MITAA NI MIBOVU HAKUNA NJIA ZA LAMI jambo kumeendelea toka kitambo.

MTONI KIJICHI
Huku mtoni kimegawanyika kuna maeneo yaliyopimwa na ya kawaida,ila kwenye makazi si haba japo ni mji flan unaokuja juu kwa kasi sana mitaa yote ina lami na taa zake hata ile mitaa isiyopitika kwa gari imejengwa vizuri kabisa. Kiukweli ukiambiwa uchague sehem ya kuishi kwa sasa kati ya hizo sehem mbili lazima uchague Mtoni Kijichi tu.

Sasa tujiulize ni wabunge gani wameongoza haya maeneo? Ni vyama gani vinaongoza haya maeneo? Kwa upande Mtoni Kijichi CCM.
 
Na bado sababu watashinda tena. Wanaoisoma zaidi ni wale wanaochagua wapinzani
Kuna mtaa jirani walichagua upinzani .......namba ilisomeka kisawasawa sijui kama uchaguzi huu watarudia tena.....maana baadae yule mpinzani waliesoma nae namba pamoja akaja kuunga juhudi ndo kidogo vibarabara vikapata pumzi
 
Ni dhahiri kabisa hata Magu mwenyewe anathibitisha hilo
 
Kuna mtaa jirani walichagua upinzani .......namba ilisomeka kisawasawa sijui kama uchaguzi huu watarudia tena.....maana baadae yule mpinzani waliesoma nae namba pamoja akaja kuunga juhudi ndo kidogo vibarabara vikapata pumzi
Kibaya zaidi Magufuli hafichi ubaguzi huu vya vyama
 
Wewe mpumbavu nini kwani CCM inaendeleza mtu, Serikali inaweka fursa tu maendeleo ni juhudi zako mwenyewe binafsi ,shinda kijiweni kama maendeleo utayapata na CCM yako hiyo
 
Mbezi beach/Mtoni kijichi ruvu waichague CCM au waendeelee kuokota viroba vilivyosheheni miili ya watanzania
 
Afe Mmaasai afe Mmang'ati wana Kawe ninaowajua Mimi Wazee wa 'Kuchinja' Kimoyomoyo Gwajima atapita tu kwa Msaada wa Polisi na Mamlaka.
 
Wewe mpumbavu nini kwani CCM inaendeleza mtu, Serikali inaweka fursa tu maendeleo ni juhudi zako mwenyewe binafsi ,shinda kijiweni kama maendeleo utayapata na CCM yako hiyo
Punguza jazba kaka utakuwa hujamuelewa jamaa au hujasoma uzi
 
Afe Mmaasai afe Mmang'ati wana Kawe ninaowajua Mimi Wazee wa 'Kuchinja' Kimoyomoyo Gwajima atapita tu kwa Msaada wa Polisi na Mamlaka.
Mimi kama mkazi wa jimbo hilo kiuchaguzi tutaona mkuu.
 
Wewe mpumbavu nini kwani CCM inaendeleza mtu, Serikali inaweka fursa tu maendeleo ni juhudi zako mwenyewe binafsi ,shinda kijiweni kama maendeleo utayapata na CCM yako hiyo
Umeelewa uzi lakini? Au umeandika na akili za hangover kichwani?
 
Maendeleo hayana chama.
Ewaaah wewe wanena!

Huko Mbezi beach kutabaki kuwa Mbezi beach...

Mtoni Kijichi ilikuwa kwenye mpango wa siku nyingi tu wa maendeleo, lakini kulikuwa na mngoni diwani wa CCM R.I.P, alipiga sana hela.

Magu alipoingia, miradi ya barabara za kule, nafikiri kukawa na uchunguzi, inasemekana, mkiti wa miundombinu yeye, kampuni ya ujenzi yeye, mkaguzi yeye!
Bahasha za kaki tu zilikuwa zinatembea.
Akapigwa stop, hakuchukua round stroke, kifo.

Kijichi ilikuwa muhimu kwa maghorofa ya Dau, kuvutia wanunuzi kwa kuwa na miundo mbinu itakayoeezesha kuungana na Kigamboni, Mbagala, Kongowe e.t.c.

Kijichi maendeleo yaliharibiwa na chama hicho hicho kilichopaswa kuyaleta.

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Jamani hivi aliyekuwa Mbunge wa huko mumewe nani??

Nazungumzia Mbezi Beach lakini.
 
CCM NI MAJANGA KWETU.MIAKA HII MITANO TUMEISOMA NAMBA
Ila CCM waliwataarifu wakati wa kampeni zao za 2015 kwa kale kawimbo kao katamu......´´Tumejipanga, mwaka huu wataisoma...´´. Tatizo kwakuwa mlishazoea kulaghaiwa, hamkuamini. Mlifikiri porojo zile zile. Kumbe Ngosha akisema anamaanisha 😂.
 
Miaka 60 ya Uhuru bado tunahangaika na Umasikini pamoja na Raslimali Alizoziacha Hayati Baba Wa Taifa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
hatukufwata barabara wala mataa barabarani, na kama tunataka tutaweka wenyewe hali zetu zinaporuhusu

Tanga/Tabora/Morogoro/Dodoma kila siku CCM inaongoza kumefanyika nini?

miaka 59 ya Uhuru bado unaitikadi za kikoloni,serious??

2015 - nilimchagua Kippi na Magufuli
2020 - nitamchagua Halima na yeyote toka upinzani, na bado ntabaki na kadi yangu ya CCM

kaa ukijua Mbezi Beach/Kilongawima/Salasala/Bahari beach/Ununio/Mbweni/Tegeta/Boko/Bunju etc tunajitambua usitufananishe na wa Ulanga au Muheza sijui Tabora na Dodoma
 
Back
Top Bottom