Kinengunengu
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 1,716
- 4,375
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.
Binafsi nadeclare interest kuwa ninatumika Kanisa la TAG kama Mzee wa Kanisa huku Nyanda za juu kusini pia ni Mtumishi wa Serikali na huwa nahubiri mara moja moja. Siandiki hivi kwa kufurahisha watu au kujisifu wala kutaka kumsafisha Mwalimu Mwakasege ila naeleza kile nilichoshuhudia na kile ambacho Mungu amenitendea.
Kwa umri na muda niliomtumikia Mungu kama Mkristo nafahamu Mungu anajifunua kwa watu wengi yeye binafsi na pia kuwafunulia kuhusu wengi kuhusu mbingu.
Binafsi, nashuhudia leo na kikiwa na akili timamu na dhamira njema Moyoni mwangu kuwa nimemuona mwenye haki "Yesu Kristo" si chini ya mara 4 toka nikiwa mdogo na amenitokea kwa namna mbalimbali tofauti na watu wanavyokashfu kuwa tutatokewa na Mapepo yaliyovaa sura ya "Bryan Deacon" yule aliyeigiza "Filamu ya Yesu" Pia nashuhudia, Mungu kunifunulia na kuiona mbingu.
Mafunuo haya ya kutokewa na Yesu kwangu mimi hayakuwa kwa jinsi ya kimwili "yaani kunitokea physically" ila ni katika ndoto na Maono ya usiku pia wakati nasali nikajiona tu nimekutana naye.
Leo sitaelezea kuhusu kutokewa na Yesu ila nitaelezea kuhusu ushuhuda wangu wa kuiona Mbingu ila nasisitiza katika hilo, kila maono, ndoto au mafunuo ya Kimungu yanajengwa chini ya Neno la Mungu. Neno: Ayubu 33:14-16 hapa Mungu anasema kuhusu kusema na wanadamu kuhusu ndoto ns mqono ya usiku.
Neno: Yoel 2: 28-29 Anasema kuhusu "Ndoto na Maono".
Kuhusu Mungu kuwafunulia watumishi wake mbingu, tunaona Paulo anasema namna alivyochukuliwa na kuoneshwa kuhusu Mbingu katika 2 Korintho 12: 2-9 pia Stephano naye anafunuliwa katika Matendo ya Mitume 7:56 na pia Mtume Yohana anafunuliwa kuhusu Mbingu wakati anaandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
Binafsi, Nakumbuka ilikuwa 2016. Mungu alinipa Neno toka Yeremia 33:3 inayosema "Niite nami nitakuitikia na nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua" pia kwa muda mrefu nilikuwa naimba moyoni mwangu wimbo mmoja wa zamani sijui uliimbwa na kwaya gani ila kuna kipande wanaimba " Nimpeleleza nani raha ya Mbingu×2, Yesu ndiye wa Kumpeleleza"
Nakumbuka Siku hiyo niliamka kama kawaida saa 9 alfajiri na kusali. Ilipofika saa 11:45 nikasema nilale kidogo ili nikiamka saa 1 hivi niende kazini. Nilipolala kama saa 12 alfajiri nikaona Malaika mmoja aliye kama mwanadamu amevaa mavazi meupe yenye kung'ara huku akiwa mwenye sura inayong'ara ananiambia "nimetumwa nikufuate". Akanishika mkono, nikaona natoka kwenye mwili upande wenye moyo.
Nikapita kwenye bati la nyumba bila kizuizi. Safari ya kupanda juu ikaanza kwa speed ya ajabu huku akiwa amenishika Mkono. Nikaangalia chini na kuona mwili wangu, mke na mtoto wangu wamelala kitandani. Unaona nyumba na miti ya duniani. Tukapaa juu kwa spidi nikaangalia chini tena na kuona kadunia kalivyo kadogo then tukafika katika nchi ile ambayo "watu" wanaimba na kumuabudu Mungu. Nikaungana nao tuliimba "Bwana Mungu nashangaa kabisa"
Sijui nielezeje muonekano wake nchi ile ila ni nzuri na ya meta meta. Hali ya hewa na mazingira ni tofauti na huku duniani. Nchi ile ni kweli na mji ule ni kweli. Jitahidi usikose kuingia mji ule.
Baadaye nikaambiwa turudi na kwa speed ya ajabu, najikuta naingia mwilini mwangu upande wa kushoto kwenye moyo, mwili ukawa kama umepigwa "shot" nikashtuka.
Binafsi, nimewasikia na kuwaona watumishi wengi wa Mungu wanaoshuhudia kuhusu Mbingu huku kwetu na sehemu myingine. Ukiacha hao maarufu, japo "Zumaridi hapana kwani inaonekana ana shida ya akili" Ukiacha Mwakasege, hata Marehemu Kulola alishashuhudia siku moja kufunuliwa kuhusu Mbingu.
Nami nimeona nishare uzoefu wangu kuhusu Mafunuo ya Mbingu. Siku nyingine nitaeleza kuhusu kutokewa na Yesu ana tutokeaje, yupoje na tunajuaje kama ni Yesu.
Asanteni.