Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Ukiacha hao maarufu, japo "Zumaridi hapana kwani inaonekana ana shida ya akili" Ukiacha Mwakasege, hata Marehemu Kulola alishashuhudia siku moja kufunuliwa kuhusu Mbingu.

Kwanini unasema zumaridi ni mental case? Kwa sababu anaongea pumba sio? Kwa taarifa yako wewe na zumaridi mpo kundi moja. Kama ni maono wote mna maono kama ni shida ya akili wote ni mnayo.
 
Kwanini unasema zumaridi ni mental case? Kwa sababu anaongea pumba sio? Kwa taarifa yako wewe na zumaridi mpo kundi moja. Kama ni maono wote mna maono kama ni shida ya akili wote ni mnayo.
Aahahhaa

Zumaridi ana akilisema in reverse
 
Umeeleza vizuri,Suala la kwenda Mbinguni kwa mkristo wala sio la kushangaa,tatizo kuna watu wakisika mtu kaenda mbinguni wanaanza kuwaza kama wao kwamba mtu kavaa mkanda nje na viatu na begi lake anasubiri basi la kumpaisha ndio maana anaona ni kitu kisichowezekana.

Kupelekwa mbinguni,inatoka roho yako ambayo ndio imevalishwa huu mwili,unaacha mwili wako kitandani unauona,au vinginevyo unapewa maono ya namna mbingu ilivyo.
 
Jama Yesu walimpinga, hata wewe watakupinga.. Mungu ni harisi, mbingu na malaika wa Mungu ni harisi, maono na ndoto vipo na uzoefu wa ki Mungu upo.. Mungu ni Yule Yule jana , leo na hata Kesho
Amina bro, hiyo ya kupinga usiwe na shaka nayo ni kitu cha kawaida kwani ilikuwepo na itaendelea kuwepo hadi mwisho wa dahari.
 

Siwezi na
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.

Binafsi nadeclare interest kuwa ninatumika Kanisa la TAG kama Mzee wa Kanisa huku Nyanda za juu kusini pia ni Mtumishi wa

Asanteni.

Dubai kweli ipo, umewahi kwenda?
 
Hauko peke yako watu wengi hukutwa na hiyo hali lakini ndoto ni ndoto tu. Ukiota unapaa, ukiota una mbawa kama malaika, ukiota tajiri, ukiota uko ulaya, angani bado ni ndoto tu.
Acha ujuaji.

Kanuni ya msingi ni kuacha ubishi wa kijinga kwenye jambo usilolifahamu.

Busara ni kufyata domo na kusikiliza maoni mengine kisha uchekeche.
 
Siwezi na


Dubai kweli ipo, umewahi kwenda?
Bro jaribu kuficha uchi wa akili yako. Humu JF ni wengi tunakuheshimu na pia sio kila thread unatakiwa uchangie. Nyingine zinakuzidi upeo wako, fanya kama hujaziona. Unajidharirisha bro, samahani kwa hilo ndugu yangu. Nenda MMU kule kuna mada za DeepPond anahadithia kuhusu mchepuko wake🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hahaaaaa, kizazi cha hovyo cha kuanzia 1990 chenye kupinga na kubisha kula kitu bwana!!!!
Mtumishi hiki kizazi kuwa cha ajabu kumechangiwa pia na mafundisho na mienendo yenu nyie viongozi.

Mfano, mnawaombea waumini wapokee mafanikio kwa imani(pesa, magari, nyumba n.k).
Lakini nyie mnapohitaji hivyo vitu mnawalazimisha hao masikini wawachangie.
Kwanini nyie pia msiombeane msubiri Mungu awape kwa njia hiyo ya imani?
 
Hawa ni wajinga wamekuwa programmed kupinga mambo ya aina hii.
Hiyo ni Roho kamali sister, katika kitu ambacho shetani amejitahidi na kufanikiwa ni kuwaaminisha watu kupinga kuhusu uwepo wa Mungu na ndio kinachofanyika huku. Kimsingi, inatakiwa tuwachukulie kama walivyo na tuwaombee ili Nuru ya Mungu iwazukie mioyoni mwao.
 
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.




Asanteni.
Tujuwe umetokea hadi unaandika uzi huu
 
Kama Mungu wako ni hai na ndie Mungu muumba wa mbingu na vyote vinavyo onekana na visivyo onekana, na unatambua maana ya neema, hutompinga mtoa mda, Mungu ni upendo na anapenda tuishi kama ulimwengu wake au kutupa hata uzoefu wa mambo yaliyo jawa na utukufu wake, ikiwamo wanaopata neema ya kwenda mbinguni, kukutana na malaika, na viumbe mbali mbali wa mbinguni.. ila kama una mungu mfu hilo haliwezekani
 
Mtumishi hiki kizazi kuwa cha ajabu kumechangiwa pia na mafundisho na mienendo yenu nyie viongozi.

Mfano, mnawaombea waumini wapokee mafanikio kwa imani(pesa, magari, nyumba n.k).
Lakini nyie mnapohitaji hivyo vitu mnawalazimisha hao madikini wawachangie.
Kwanini nyie pia msiombeane msubiri Mungu awape kwa njia hiyo ya imani?
Siwezi kupinga hoja yako ndugu yangu. Ni kweli sasa katika kitu ambacho Shetani amefanikiwa katika kanisa ni kupandikiza magugu jatika Ngano. Ni kweli ukifikiria na kutazama yanayoendelea makanisani yanaumiza Moyo kwani kuna magugu mengi.

Hoja yangu mimi ilikuwa ni kupinga kila kitu kinachohusu Mungu na wengi kutamani kusikia na kupokea habari mbaya zinazohusu kanisa na watu wengine.
 
Back
Top Bottom