Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.



Asanteni.
Wakristo kwenye ndoto huwa mnapigwa sana aisee. Inaonekana hamjui chochote kuhusu ndiyo.

Katika mada yako nilitegemea ungeweka maandiko ya Yesu kuwapa muongozo endapo ukiota ndoto ya namna hii ujue ya kweli na ukiotea ndogo ya namna hii ujue ya uongo bali ya kishetani.

Kwahiyo nyinyi mnasimulia tu kila mnachoona kisha mnakiamini na kuja kuwasimulia watu.

Ndoto ni jambo pana sana.
 
Huwa sikatai kabisa kuhusu mtu na Mungu wake, wala ubishani. Na nina amini katika Mungu ni halisi na Mbingu ni halisi.
cha msingi vipimio ni hivi.

1. ..."wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu."1 Wakorintho 12:3

2. Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;
1 Wathesalonike 5: 19-21

3. Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 1 Yohana 4:1

4. Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Isaya 8:20

5. Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
Kumbukumbu la Torati 13:1-3

Ukitumia kanuni hizi hutapata taabu kujua huu ni uongo au ukweli wote hata walioenda mbingu wakataka kuoa au kuolewa WANAPIMIKA HAPA. kanuni hizo ni uko Maabara una test sample tofauti na unajua genuine ni ipi.
 
Naona mwny thread hatak kunijibu,nalileta swali kwenu nyote unaeamini mbinguni ni juu ,ila naomba mtu huyo atakaesema ndio mbinguni ni juu awe amepita na darasa la elimu dunia pia
 
Ni bora mtu aniambie katokewa na Mungu fresh wakaongea yao yakaisha akarudi kitandan fresh,ila maswala ya kupaishwa juu na mabwawa mpk kafikishwa mbinguni na akapaona,asee haiwez kuwa kweli
 
Mimi binafsi nimejichagulia kadhehebu kangu naamini Mungu,upendo na dhambi vyote vipo ila siamini kuhusu Moto wa milele,niko na huu utaratibu baada ya kufatilia mafundisho ya biblia

Kuna mtu atasema swala la moto limerudiwa sijui mara nne kwny biblia,hilo nafahamu na nishafundishwa kuhusu hayo mafundisho,
 
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.

Binafsi nadeclare interest kuwa ninatumika Kanisa la TAG kama Mzee wa Kanisa huku Nyanda za juu kusini pia ni Mtumishi wa Serikali na huwa nahubiri mara moja moja. Siandiki hivi kwa kufurahisha watu au kujisifu wala kutaka kumsafisha

Asanteni.
Kwa nini Zumaridi mlimbishia makumuita muongo?

Kwa nini shuda yako ni baada ya Mwakasege hauoni kuna kaupendeleo?
 
Huyu anasema huu ni ushuhuda wake binafsi, kamuona Yesu, tutajua vipi kama hana matatizo ya akili anaona maluweluwe tu?
Nakubaliana na wewe, fuatilia vizuri wale church Fathers wenyewe na maaskofu na mapadre hadi Papa hakuna anayeweza kukuletea story kama hizi za kwenda mbinguni.

Naamini ni illusion zake tu zinamsumbuwa, binafsi Mimi huwa naota napiga story na Marais wa nchi tofauti hadi mama Samia, nikiamka najuwa hizi ni ndoto, ila nakuwa nashukuru sijaota ndoto mbaya zile za kufukuzwa na majoka au mnyama mkali hadi unapaa ndio unajiokowa.

Mimi nimeshaota Mara nyingi tu napaa, yani nikikutana na kitu kibaya silaha yangu huwa napaa kabisa mawinguni na kusafiri mbali sehemu ambazo sijawahi kufika, sasa hawa jamaa zetu wakiota ndoto kama hizi anakuja na ushuhuda eti alikuwa mbinguni, dah haya mambo mengine ni shida kwakweli.
 
Hayo ni yako kamanda na huyo Mungu wako unayemuamini. Kwangu tu mimi mwanadamu "kinengunengu" pesa ni karatasi tu zilizokuwa "printed" na wanadamu na hazina thamani isije kuwa kwa Mungu wangu yeye aliye mmiliki wa vitu vyote. Inawezekana thamani ya Mungu wako ni sawa na pesa ndio maana anakuja kwako ukiwa na pesa ila wangu mimi ni wa thamani zaidi ya vyote. Yeye ni wa vyote katika vyote.
UsilaZimishe unakutanaga namungu kumbuka vizuri izosiku ulikua unaota ulikula nini inawezekana ulikula kipolo cha maharage umepigwa hakuna mungu ulikutana nae maharagwe yakilala yanatengenezaga kakilevi inawezekana ulilewa nakama unakubaliana na hili lako kubali nala Zumaridi usijipendekeze kwa Mwakasege
 
Nakumbuka we mzee ulimuuzia mama angu papai ukasema umepewa na yesu ulivyoenda mbinguni

Sema papai lilikuwa tam sana mkuu
 
Inaonekana bro una frastruation zako maana si kwa kuhara huku. Mbona mtu katoa shuhuda yaje, then wewe unaandika vitu visivyohusiana?
Sina frustration yoyote bro..!! Tunawapa tu facts zao kwa kucheza na akili za watu..!! Hizo shuhuda wala hazina ushahidi wowote ya kwamba ni za kweli. USISAHAU WAONGO WAPO PIA. NA NI KAZI SANA KUMTOFAUTISHA MUONGO NA MKWELI KWENYE DUNIA YA LEO. Haitosishi kwa yeye kusema tu..!!
 
Kwa kawaida ndoto zinatokana na mambo tunayoyafikia na kuwazia kwa muda mwingi lakini hii haithibitishi ndoto ni jambo la kweli.

Kumbuka ndoto ni "images" au mfuatano wa picha zinazotengenezwa na subconcious mind na kama nilivyosema ndoto maza zote zinafuata mambo tunayoyaamini sana au kutumia muda mwingi kuyafikiria.

Hiyo maana yake kama wewe ni born again Christian na muda mwingi unawazia kuhusu mbingu, yesu, mungu, malaika, shetani au mambo mengine ya kiroho basi ni rahisi kuona matuko yenye kufanana na haya kwenye ndoto zako kwasababu subconcious mind inatengeneza images zinazokuonyesha mfano wa mbingu, yesu, mungu nk.

Ndiyo maana ndoto nyingi za namna hii ukichunguza zinasimuliwa na watu dini wanaotumia muda mwingi kuwaza mambo ya namna hii.

Pia ukichunguza watu wanaoishi maisha ya woga, kukandamizwa na wasiwasi basi ni rahisi kwao kuota wameenda jehanamu au sehemu za mateso. Unadhani kwanini?

Hiyo yote ni trick za bongo zetu tu, lakini hakuna ukweli katika vitu walivyoota.

Mwisho, ukiota umeingia heaven au sehemu nzuri hiyo maana yake kuna mambo mazuri unahitaji katika maisha yako lakini unakosa. Ni namna ubongo wako unakuonyesha matamanio yako unayoshindwa kuyatimiza katika physical world.
 
Umeeleza vizuri,Suala la kwenda Mbinguni kwa mkristo wala sio la kushangaa,tatizo kuna watu wakisika mtu kaenda mbinguni wanaanza kuwaza kama wao kwamba mtu kavaa mkanda nje na viatu na begi lake anasubiri basi la kumpaisha ndio maana anaona ni kitu kisichowezekana.

Kupelekwa mbinguni,inatoka roho yako ambayo ndio imevalishwa huu mwili,unaacha mwili wako kitandani unauona,au vinginevyo unapewa maono ya namna mbingu ilivyo.
Sasa wasio mjua Mungu wataelewa nini,ogopa sana jambo usilo lijua akaja mtu kutaka kukuaminisha ,kuishi maisha ya neema na kumjua Mungu si watu wote walio jaaliwa.

Ingawa kumekuwa na mafundisho mengi ya kumwelekea Mungu lakini ni wachache mno wanao yajali na hata kuyaelewa na kufuaata yasemavyo.

Enzi za zamani kumjua Mungu ilikuwa ni siri nzito na ilikuwa ni baadhi ya familia tu zinazo mjua na kumtumikia mwenyezi Mungu,wengine wengi walikuwa wakiponda anasa na mambo machafu wakati wote wala hawakutambua uwepo wake ,na wengine wale wenye kutambua kwa kiasi waliishia kupuuzia tu,Maandiko yapo wazi juu ya hili.

Mtu awaye yote asiye kuwa karibu na Mungu na wala asiye jishughurisha naye hawezi kumuelewa mtoa mada,Kuna watu wapo deep sana katika imani.
Mnatakiwa mueelewe kwanza neno imani.
Ili kitu kitendeke lazima kwanza uamini.

Usipo kuwa na imani, wewe utaishia kufanya mambo madogo madogo tu ya kidunia ambayo kila mtu anauwezo wa kufanya ,utaota ndoto za kushiba na kupandishwa vyeo makazin au kuota una kula tunda kimasihara

Dunia ina mambo mengi ,unaweza ukajua baadhi ya mambo na ukazani umeimaliza kumbe hakuna kitu unajua.
Mimi nimekaa na watu walio jikita kwenye imani hadi nikaona kama wanaigiza kumbe ndo maisha yao.Wewe unae ishi kidunia mambo ya imani ni nini kushughurika nayo? na kwa sababu ipi ujue nani alienda wapi na akarudi ? Ya kazi gani sasa ! Hata ukiamini au usipo amini itakusaidia nini,si kujichosha bure huko!
Ya ngoswe muachie ngoswe ,wewe agiza bapa kubwa tupige ,tushushie na yule asiye pendwa na wale watu .

Imani ni siri ,siri hufichwa ,ni sawa na uchawi ,watu huamini upo na wengine kata kata hukataa,ndivyo ilivyo .Kukubali au kukataa jambo haiondoi uhalisia wa uwepo wake au kutokuwepo kwake.

Imani ni mlango unao ingiza nguvu ndani yako na hata kujua au kuona na hata kutenda mambo mageni au yasiyo ya kawaida kwa mwanadamu.

Mimi nina imani na ninaamini katika kile mtu anachoeleza mana nina imani ya kwamba lolote linawezekana.

Kwa mfano katika mambo mengi ya wazi wanayo fanya watu yanayo husu imani ni uchawi,uchawi ni vilahisi zaidi kuuona ama kuushuhudia kazi zake,japo hufichwa ila ni rahisi sana kuziona kazi zake katika mazingira tofauti tofauti.

Ili uchawi ufanye kazi lazima imani itumike na ihusike.Jambo lolote ukitaka ulifahamu vyema basi jitahidi kushiriki pamoja na washirika wake.Ukitaka kuijua imani yoyote kaa na watu wa umani hiyo.

Mfano sisi sote tumesoma ,na hapo mwanzo angali tupo wadogo tulikuwa hatujui chochote kuhusu elimu ,iwe kusoma au kuandika,tulihangaika sana kuumba herufi moja moja tu,yaani hata kuandika herufi 'a' kwetu ilikuwa mtihani.
Ila taratibu tukaja jikuta tunaweza kusomewa imla na tukaandika vyema na kukokotoa hesabu matata vyema kabisa.Leo hii tusingejifunza kuandika na kusoma si tungeona ni mambo yasiyo wezekana aslani .

Basi chochote na lolote linawezekana ingali tukiwa hai hapa tuniani.
Basi tambua jambo lolote usilo lijua ,uambiwapo lipo au hutokea ingawa wewe hujawahi shuhudia ama kuona usiwe mwepesi wa kubisha tu ,maana mengi bado huyajui hata ukiwa na phd yako,wewe bado tu ,unaweza ukayaona na kuyajua yanayo onekana kwa macho ya mwilini tu ila yale yasiyo onekana kwa macho ya mwilini usiyajue.

Basi tuamini kwa kuona au kusikia na hata tusipo ona ama kusikia twaamini mana tunayo imani na ishara zatuijia .
 
Back
Top Bottom