Mbinguni hakuna kuoa – kama hujaoa, oa sasa ufurahie maisha!

Status
Not open for further replies.

Mbinguni ndio mahali gani ??
 
Nimeishakuambia mimi ni bibi Arusi wa Mfalme, au kama Kiswahili hujui: "Am the Covenant Bride of the Heavenly Bridegroom."
Unaolewa na Mungu wa Mbinguni?
 
Unatakiwa upate mke wa kufanana na wewe mwenye Poor Brain unayeshindwa hata kuandika mashairi.
Kumbuka hata Adamu alifanyiwa msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2:18
“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake; nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
 
mimi nimesha jikatia tamaa ya kuoa kwa kukosa hela, yaani imepelekea kutojiamini kabisa yaani ninatamani kuwa na familia lakini kila nikijaribu hata kulazimisha lakini wapi, apa ninaandika nina maumivu ya moyo naona sina thamani, nina mengi ya kuzungumza lakini sina wakumwambia
 
Unaolewa na Mungu wa Mbinguni?
Ufunuo 19:9
Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa katika karamu ya arusi ya Mwana-kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

Nilitoa kadi ya MWALIKO hapa, hukuipata?
 
Endelea kukaa siti ya mbele, ntakurudia...utafurahi muda si mrefu!
 
Mbinguni ndio mahali gani ??
Jibu liko hapa. Soma kwa makini huku ukitafuna popcorn, utaelewa 🙂
 
Usasa tujadili nini maana wanojadili siasa wanauwana cha maana kipi embu tufahamishe
Mwambie kwa SAUTI KUBWA halafu subiri uone labda atasikia.
Umenena vema kabisa: Heri tujadili mambo ya ufalme wa mbinguni kwa sababu dunia hii inapita na siasa zake.
1 Yohana 2:17
“Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake; bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”
 
Hayo sio mashairi mama angu ni maneno kutoka katika akili yangu
 
We kumbe chizi, kabla ya hiyo bible alikuwepo babu yangu mwana nanjilinji.

Hakukuwa na bible Wala hizo fake notes, zaidi ya asili.
Wewe naona ni Intelligent businessman katika mambo ya fedha na uchumi lakini kuhusu spiritual business bado unahitaji kusoma zaidi. Kumbuka kuwa ukweli hauzuiliki kwa sababu historia ya familia yako haikuujua. Biblia haikuanzisha maisha, lakini inafunua maana ya maisha. Uwepo wa mababu zetu kabla ya Biblia haupingi ujumbe wa Biblia, kama vile ambavyo mvua ilikuwepo kabla ya thermometers, lakini hilo halimaanishi vipimo vya hali ya hewa ni “fake.” Una uhuru wa kuamini chochote, lakini mimi nimeonja neema ya Mungu na nina hakika: kuna nguvu ndani ya Neno la Mungu ambalo halijatungwa na mwanadamu.
 
Endelea kukaa siti ya mbele, ntakurudia...utafurahi muda si mrefu!
acha ndugu yangu nashindwa nifanyeje, ninayo yapitia mungu mwenyewe ndiye anayejua na naona muda simrefu nitaugua sonona.
Mungu aniepushe nimechoka
 
acha ndugu yangu nashindwa nifanyeje, ninayo yapitia mungu mwenyewe ndiye anajua na naona muda simrefu nitaugua sonona.
Mungu aniepushe nimechoka
Mungu amekuona ndio sababu amekuleta hapa ili upate jibu la tatizo lako. Nilikuahidi, endelea kukaa siti ya mbele ntakurudia. Utafurahi tu. Mungu hana upendeleo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…