Mbinguni hakuna kuoa – kama hujaoa, oa sasa ufurahie maisha!

Status
Not open for further replies.
Na nilicho gundua
Couple yetu ina bamba
Ohh yabambaa

Hata liwake inyeshe mvua
Mi nawe sambamba
Ohh sambamba

Wewe ni wangu mamaa
Couple yetu ina bamba
Ohh ina bamba

I CANT LIVE WITHOUT YOU 🥺 🥺 🥺 IFOMANE.....
A’udhu billahi min ash shaytaan ir-rajeem
Hata mkikesha club asubuhi mko gym
unampenda na kumheshimu
Mkata shombo ukipenda muite ndimu😋
 
Kwanini unanifanyia hvo..
Just imagine ungekua weww ungekua na hali gani..?
Ningekuwa mimi ningemshukuru Mungu kwa kila jambo
1 Wathesalonike 5:18
"Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu."
 
Wanaojiita watumishi wa Mungu wanachukulia maisha poa sana!!
Ukiwa ndani ya Yesu maisha ni poa sana.
Na wewe Ibn Unuq onja uone jinsi Bwana alivyo mwema
Zaburi 34:8
Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia.
 
Mbona unadanganya wenzako mkuu? Ujuwe vijana wa Kiislam hawakuelewi, wao walishaambiwa wanawake wa hapa duniani hawafai, wanawake wazuri wako mbinguni tu, hivyo wajiue tu mapema wawahi mabikra wao 72 walioandaliwa na Mungu kwa ajili yao. Wewe unakuja na hoja tofauti, shauri yako....utasomewa albadiri, ohooo!
 
Mimi sijadanganya watu, mkuu. Muulize jenerali wao Covax ameandika katika mojawapo ya nyuzi zake kwamba na wao wanamwamini Yesu. Sasa Yesu ndiye aliyesema kwamba katika kiyama ya wafu hakuna kuoa wala kuolewa. Nani wa kuaminiwa: Yesu au hao waliotunga hadith za mabikra?
Halafu kwa taarifa yako laana ya aina yoyote iwe ya albadiri, hainipati. Shetani mwenyewe ananijua mimi ni nani. Nikimkemea kwa Jina la Yesu, anatimua mbioooooooooooooooo
 
Ndugu yangu Niomi kaka , niliahidi ntakurudia.

Kwanza pole sana kwa maumivu unayopitia. Sasa fahamu haya mambo muhimu:

1. Thamani yako haitegemei pesa. Biblia inasema hivi:
Mathayo 10:29-31
"Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu; lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi."

Maana ya Maandiko hayo ni kwamba Mungu anakujali hata kama huna pesa. Wewe ni wa thamani machoni pake kuliko mashomoro(ndege).

2. Mke mwenye busara, mtu hupewa na Mungu
Mit 19:14
"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA."

Ukimuomba Mungu na kumtumaini, anaweza kukufungulia mlango, ukapata mke mzuri, ukaoa bila hata kutumia gharama kubwa. Mungu anaweza kukutendea muujiza hata gharama za arusi ukalipiwa na watu wengine. Ninazo shuhuda nyingi za watu waliooa kwa njia ya miujiza.

3. Mungu huinua waliovunjika moyo
Zaburi 34:18
"Bwana yupo karibu na waliovunjika moyo, Na huwaokoa waliopondeka roho."

Kama Maandiko hayo yalivyonena, Mungu yuko karibu na wewe. Maumivu yako na machozi yako Mungu ameyaona.

4. Chukua sasa hatua hii muhimu: Kama hujaokoka, nakusihi uamue leo kuokoka. Ukiokoka, Mungu atakuwa karibu na wewe sana. Hivyo utakapoomba atasikia na kukupa haja ya moyo wako kama Yesu alivyoahidi katika Mt 7:7

Kuokoka ni rahisi sana. Ukifuatisha sala ifuatayo ya toba, utaokoka sasa hivi, na Mungu ataanza kusikia maombi yako na kukusaidia.

Omba hivi:
"Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa na asante kwa kuwa sasa mimi ni mtoto wa Mungu. Naamini kila nitakaloliomba kuanzia leo, utanipa ee Mungu sawasawa na jinsi ulivyoahidi. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho.

Ukiishajiunga na kanisa hilo, usiache kumshirikisha Mchungaji wa Kanisa hilo kuhusu hitaji lako la kupata mke ili na yeye akuombee. Na mimi nitakuombea. Kamwe usikate tamaa. Naamini muda si mrefu utapata mke mwenye busara na furaha yako itakuwa timilifu.
Yn 16:24
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.

Mungu akutunze, na akupe haja ya moyo wako, katika Jina la Yesu, Amen.
 
Ningekuwa mimi ningemshukuru Mungu kwa kila jambo
1 Wathesalonike 5:18
"Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu."
Namshukuru Mungu kwa kunipa wewe...
Furaha yangu ni wewe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…