Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
1. Mbinu ya “Chaguo la Uongo” (False Choice Trick)
Mfano:
“Ungependa tukutane saa 9 au saa 11?”
Kwa nje inaonekana ni wewe unachagua, lakini kisaikolojia chaguo zote mbili zinampeleka mpangaji kwenye anachotaka.
Saikolojia Inavyofanya Kazi:
Hii inaitwa Illusion of Control. Wakati ubongo wako unaamini una uhuru wa kuchagua, haufanyi upinzani. Hii hutumika sana kwenye biashara, siasa, na hata kwenye mahusiano ya kimapenzi. Unapoweka chaguo mbili ambazo zote zinaelekea kwenye matokeo unayotaka, unampa mwathirika hisia ya kuwa na ushawishi wakati hana.
2. Mbinu ya “Chelewesha & Kutoweka” (Delay & Vanish Tactic)
Mfano:
Mtu akikukosea heshima, badala ya kujibu kwa hasira, unanyamaza, unasmile kidogo, kisha unatoka bila neno.
Saikolojia Inavyofanya Kazi:
Ubongo wa binadamu haupendi vitu visivyo na majibu. Kukosa jibu kunamuacha mpinzani katika hali ya kuchanganyikiwa (cognitive dissonance), akijiuliza alikosea wapi. Utulivu wako unamnyima kuridhika kwa “ushindi wa hoja,” na badala yake anaanza kujihisi mdogo kisaikolojia.
3. Mbinu ya “Nanga ya Kutaja Jina” (Name Drop Anchor)
Mfano:
“Ni wazo zuri sana, Amina. Unajua Amina, nimegundua kitu…”
Unarudia jina la mtu mara nyingi katika mazungumzo.
Saikolojia Inavyofanya Kazi:
Hii inatumia principle ya familiarity. Ubongo huamini zaidi kitu kinachojulikana. Kutaja jina mara nyingi huchochea hisia za ukaribu na uaminifu, hata kama mnahusiana kwa muda mfupi.
4. Mbinu ya “Mguso wa Bahati Mbaya” (Accidental Touch Trick)
Mfano:
Kugusa bega au mkono wa mtu kwa muda mfupi wakati wa mazungumzo.
5. Mtego wa Kuiga (The Mirroring Trap)
Mfano:
Unaiga mwendo au lugha ya mwili ya mtu taratibu, kisha unabadilisha pozi. Wakiiga tena, tayari umepata udhibiti wa kisaikolojia.
Ukitumia mbinu hizi vizuri kwa kuzingatia misingi ya nguzo za maongezi ikiwemo staha na kujiamini, basi inakuwa rahisi kumshawishi mtu yeyote akubaliane na mawazo yako. Hata mwanamke unayemmudu kuchomoka inakuwa ngumu