Mbinu 6 za kumsahihisha Mkeo pale anapokosea pasipo kuumiza Hisia zake

Mbinu 6 za kumsahihisha Mkeo pale anapokosea pasipo kuumiza Hisia zake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MBINU 6 ZA KUMSAHIHISHA MKEO PALE ANAPOKOSEA PASIPO KUUMIZA HISIA ZAKE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Ukiishi na Mwanamke utagundua Wanawake NI viumbe weñye makosa mengi madogo madogo àmbayo Kwa kiasi kikubwa hawayafanyi Kwa kupenda.

Uchunguzi wàngu unaonyesha kuwa makosa mengi yanatokana na kuendeshwa na HISIA. Makosa machache yakitokana na usahaulifu unaochangiwa na tàbia yao ya kuwa na mambo meñgi.

Ukitaka kuishi VIZURI na Mkeo Siku zote za Maisha yako Basi Kamwe usijifananishe naye, usijilinganishe naye.
Mwanamke anaakili kama Mwanaume lakini Akili hiyo haifanyi Kazi kiume.
Mwanamke anahisia kama Mwanaume lakini HISIA hizô hazi-operate kama Mwanaume.

Kama utajilinganisha na Mkeo NI wazi utamkasirikia na kuona kama anakufanyia makusudi kufanya Makosa. Jambo ambalo siô Sahihi.

Nimesema Makosa madogo madogo àmbayo NI mengi hufanywa bila ya waô kuamua.

Ila makosa Makubwa mengi wanafanya Kwa kuamua yàani wanafanya Kwa dhamiri.

Sisi Watibeli tunasamehe Makosa àmbayo hayajafanywa Kwa dhamiri/kukusudia.

Makosa Makubwa kama Usaliti( cheating), Kosa la kwenda Kwa Mganga au uchawi, Kosa la kuchukua Mîkopo pasipo kuomba ruhusa kwako Mumewe hayo ni Makosa Makubwa àmbayo Watibeli hatufikirii mara Mbili na adhabu zake zîpo wazi tangu Siku ya Kwanza.
Makosa hayo hayahitaji kusahihishwa Bali NI kufukuzwa Moja Kwa Moja,

Kosa la Mwanamke kuchukua Mkopo Kwa Siri hii NI Mada ñyiñgine àmbayo Kwa hakika nitakuja na àndiko lake.

Sitaki kuwachosha na maelezo marefu. Zifuatazo NI MBINU Kumi za kumsahihisha Mkeo pale anapokosea pasipo kuumiza hisia zake;

1. Usimkaripie Wala Kumlaumu.
Mwanaume ni ule uwezo wa kuyafanya mambo magumu kuwa yakawaida au rahisi. Hii itaonyesha ukomavu wako.

Watu wanaofokafoka, laumulaumu kisaikokojia wanatatizo la Akili, au Wana emotional damage. Mwanaume hapaswi kuwa Mtu kufokafoka au kulaumu.
Mwanaume ni mtoa suluhisho.

Mkeo ni mwanafunzi kwako, wewe kwàke ni Mwalimu. Njia rahisi na Bora ya kumfundisha mwanafunzi siô kumkaripia au kumlaumu

Mfano, amevunja na kuharibu kitu.
Usimfokee Wala kumlaumu,

Mwambie; Pole, haujaumia, atajibu, kama ameumia onyesha kujali zaidi kuumia kwàke. Mfanyie utaratibu WA tiba.
Kama hajaumia, rekebisha hicho kitu alichoharibu, kama haiwezeniki haidhuru.
Mwambie, asijali kitanunuliwa kingine au kitarekebishwa.

Mwambie, Siku nyingine awe MAKINI hasa na vitu vya umeme kwani siô tuu vinaweza kuharibika Bali vinaweza kumuumiza hata yeye Jambo ambalo NI hatari mwambie, NI Vizuri akiwa anashika vitu aina hiyo akushirikishe.

Elewa, hiyo ni ajali(uzembe) inaweza tokana na kutokujua au Kutokuwa MAKINI.

Hapo mtazidi kujenga mahusiano Yenu. Vitu visiharibu utu wenu(mahusiano Yenu) usivipe Vitu thamani kuliko Mkeo. Hivyo NI vitu tuu.

2. Usimuabishe mbele za Watoto na Watu.
Hili pia ni tatizo la wengi.
Ameshakosea, Makosa yake yasikufanye ukosee.
Amekosea Kupika labda Kwa kuunguza au kuweka chumvi nyingi.
Mwambie, Leo kidôgo umeteleza, chumvi imezidi. Chàkula cha Jana na juzi kilikuwa kitamu na ulifanya Vizuri. Inatosha.

Sio unaanza kupigapiga kelele kama mwehu tenà mbele ya Watoto. Huo siô Ubaba, Wababa hawafanyagi hivyo.

3. Kuwa na desturi ya kumsifia anapofanya vizuri ili isimpe shida Siku ukimkosoa.

Siku zote úkiwa MTU WA kukosoa tuu pasipo kumsifia Kwa Yale mzuri atakuona unagubu, Huna shukrani, mlalamishi.
Na pia ukimsifia tuu pasipo Kumkosoa atakuona kama Chawa wake.

Mkeo akifanya mzuri mpe Sifa na elezea jinsi unavyofurahia uwèpo wake katika Maisha yako.

4. Msaidie kufanya Masahihisho Kwa Upendo
Shiriki naye katika kusahihisha Makosa yake ili ajifunze Kwa vitendo.
Mwanaume ni package lazima uwe na vitu vingi kuliko Mkeo.

Unapomsaidia Mkeo kufanya Masahihisho Kwa pàmoja unamjengea tàbia ya naye kukusaidia pale utakapofanya Makosa. Unapomuacha afanye mwenyewe huku ukimsimanga naye atafanya vivyohivyo Siku utakapokosea.

Elewa, Kwa asilimia 90 Maisha NI kile upandacho.

5. Mfanye mkamilifu kupitia Makosa yake.
Makosa ndîo humfanya MTU kuwa mkamilifu. Bila Makosa MTU hawezi kuwa mkamilifu.
Ingawaje ukamilifu katika Makosa hutegemea na namna Makosa hayo yanavyosahihishwa.

Mwambie asijali, ndîo anajifunza, Siku akijua hawezi kukosea. Atakuwa mkamilifu katika Jambo Hilo.

6. Mfundishe kutofanya Makosa yàani kuwa MAKINI.
Kuwa MAKINI kunahitaji, ujuzi na maarifa, Muda Sahihi, na Akili ilyotulia.
Kufanya vitu Kwa mpangilio Sahihi.

Zingatia, mambo yôte haya ili uyafanye unapaswa uwe umekomaa, úwe na uwezo WA kudhibiti HISIA zako, na uwe na Upendo thabiti.

Elewa, jinsi unavyoshughulikia matatizo madogo madogo ya Mwanamke wako ndîo itaamua hatma nzuri au mbaya ya mahusiano Yenu. Pia Kwa kiasi kikubwa makosa madogo madogo Wanawake wanayoyafanya ndîo hupelekea waô kufanya Makosa Makubwa kama Usaliti, ushirikina na uchawi n.k. kama hutojua namna ya kuyashughulikia.

Elewa, Mwanamke anapendwa kupendwa Hilo ndîo Jambo Namba Moja Kwa Mwanamke yeyote Duniani. Hiyo kupenda Pesa ni kwaajili ya kutaka kupendwa yàani awe Mrembo na azidi kuvutia Upendo Kwa Watu.

Elewa Mwanamke huweza kubadilika na kutokukupenda pale atakapoona hapendwi na kama utamfanya asipendwe(ukishindwa kumhudumia Mkeo hakuna atakayempenda kwani atajichokea na kuwa kama gari bovu).
Mwanamke hata kama haumpendi lakini ukamfanya akapendwa na Watu Wengine anaweza kuvumilia ndàni ya Ndoa.

Note: Usimpende Mwanamke kama Huwezi kumpenda. Utajiumiza.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Mkuu wewe kila kitu huwa una ufahamu nacho tu.. inaonekana una life stable sana kuanzia

  • kumiliki ukwasi wa kutosha
  • kuwa na mke anaekuheshimu na kukutii
  • Kuwa na heshima ya kutosha sana pale ukweni
  • kuwa na watoto waelewa na mfano bora mitaa uliyopo
  • kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayokuzunguka
 
That's too theoretical, can't work with our African ladies.

Hujawahi kusikia Wanawake hawapendi Wanaume laini (Soft hearted Men).

"Mwanaume wangu nimemkamata kweli kweli, hafurukuti hata Kwa dawa"

Oa uone mambo yalivyo magumu Kwa ground 🙌
 
Mkuu wewe kila kitu huwa una ufahamu nacho tu.. inaonekana una life stable sana kuanzia

  • kumiliki ukwasi wa kutosha
  • kuwa na mke anaekuheshimu na kukutii
  • kuwa na watoto waelewa na mfano bora mitaa uliyopo
  • kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayokuzunguka

Hapana Mkûu. Wewe ndîo Unanion hivyo.
Sijui mambo meñgi mno kama fizikia, kemia, hisabati, tehama, lugha zote za kigeni, jiogolojia, masuala yote ya udaktari, n.k.

Ungenambia napenda kujifunza mambo meñgi na kuya-share ningekujibu Naam.

Siô kîla MTU kipaombele chake NI utajiri Mkûu.
 
Hapana Mkûu. Wewe ndîo Unanion hivyo.
Sijui mambo meñgi mno kama fizikia, kemia, hisabati, tehama, lugha zote za kigeni, jiogolojia, masuala yote ya udaktari, n.k.

Ungenambia napenda kujifunza mambo meñgi na kuya-share ningekujibu Naam.

Siô kîla MTU kipaombele chake NI utajiri Mkûu.
Anyway, I was just kidding..
Huwa nakubali sana post zako. Huwa nadokoa dokoa baadhi ya details
 
That's too theoretical, can't work with our African ladies.

Hujawahi kusikia Wanawake hawapendi Wanaume laini (Soft hearted Men).

"Mwanaume wangu nimemkamata kweli kweli, hafurukuti hata Kwa dawa"

Oa uone mambo yalivyo magumu Kwa ground 🙌

Kufanya hivyo siô kuwa soft,
Soft wanachomaanisha Wanawake NI Mwanaume asiyejitambua, mwenye Akili mgando, mwenye kuendeshwa kihisia na mwenye mwili nyororo.

Wengi wakisikia Wanawake wanapenda Wanaume wasiosoft Akili yao hufikiria Ubabe, ukorofi, ushenzi n.k.
Sifa hizô Hakuna Mwanamke mwenye Akili timamu hawezi kubali Mwanaume mbabe, anayeendeshwa na mihemko, anayetukana hovyohovyo anayechepuka bila Akili yaani kidogo tuu umekamatwa.
 
Kufanya hivyo siô kuwa soft,
Soft wanachomaanisha Wanawake NI Mwanaume asiyejitambua, mwenye Akili mgando, mwenye kuendeshwa kihisia na mwenye mwili nyororo.

Wengi wakisikia Wanawake wanapenda Wanaume wasiosoft Akili yao hufikiria Ubaba, ukorofi, ushenzi n.k.
Sifa hizô Hakuna Mwanamke mwenye Akili timamu anazitaka.
Nasemaje Mkuu, oa uje ulete Mrejesho hapa.

Wewe si Thomaso yule jamaa ambaye hakuamini Masihi amefufuka?

Nenda hivyo hivyo soft hearted uone kama hujaashwa usiku wa manane umfungulie Mkeo mlango akiwa ametoka kulewa na her besties zake
 
Nasemaje Mkuu, oa uje ulete Mrejesho hapa.

Wewe si Thomaso yule jamaa ambaye hakuamini Masihi amefufuka?

Nenda hivyo hivyo soft hearted uone kama hujaashwa usiku wa manane umfungulie Mkeo mlango akiwa ametoka kulewa na her besties zake

Watibeli tunatumia nguvu kûbwa katika chaguzi na siô kutumia Ñguvu kwèñye kupigania machaguzi yetu

Siwezi oa Mke anayekunywa pombe achilia mbali mlevi.

Ñipo na familia mwaka WA nane huu.
Mke na Watoto wawili.
 
Watibeli tunatumia nguvu kûbwa katika chaguzi na siô kutumia Ñguvu kwèñye kupigania machaguzi yetu

Siwezi oa Mke anayekunywa pombe achilia mbali mlevi.

Ñipo na familia mwaka WA nane huu.
Mke na Watoto wawili.
Umepata bahati Kuoa Mke asiyekunywa pombe achilia mbali Mlevi

Mimi pia nina hiyo bahati 🙏

Kwa maisha ya sasa, ukifanya tathmini kati ya Wanawake 3 hadi 5 kati ya 10 utakuta wanakunywa pombe.

Mwanamke anayekunywa pombe ni rahisi kukengeuka na kukuendesha ndani ya nyumba iwapo utampa hiyo first class service.

Kiasili Mwanaume ni Kichwa na Kiongozi wa familia, Mwanamke ameumbwa kupokea maagizo na maelekezo ya wewe Mwanaume.

Ukiwa too soft jiandae kumkabidhi Madaraka Mkeo ndani ya nyumba akuongoze
 
Back
Top Bottom