FestoKaguo
Senior Member
- Apr 1, 2022
- 128
- 202
Kujifunza kitu kipya ni rahisi, lakini kukikumbuka kwa muda mrefu mara nyingi ni changamoto. Wanafunzi, watafiti, na hata wafanyakazi kazini mara nyingi hukutana na hali ya kusoma kwa bidii lakini baada ya muda mfupi kusahau mengi waliyosoma.
Habari njema ni kwamba kuna mbinu za kitaaluma na za kisaikolojia zinazoweza kuongeza uwezo wako wa kukumbuka. Ukitumia mbinu hizi, unaweza kukumbuka zaidi ya 80% ya kitu ulichokisoma.
Hapa kuna mbinu saba rahisi lakini zenye matokeo makubwa:
Badala ya kusoma maandiko mara nyingi, jaribu kujipima. Funga kitabu au article unayoisoma kisha anza kujiuliza maswali kama vile: “Nimekumbuka nini hapa?”
Kwa kufanya hivi, utalakuwa unaulazimisha ubongo wako kurudisha kumbukumbu za ulichokisoma badala ya kuishia kuzipokea tu na kusahau. Utafiti unaonyesha hii ndiyo njia bora zaidi ya kuimarisha kumbukumbu.
Kama huna mtu wa kumfundisha, jitengenezee video au andika maelezo mafupi kana kwamba unamfundisha mwanafunzi.
Hii itakusaidia kuona uhusiano wa mawazo uliyonayo na kuunganisha key points kwa urahisi.
6. Fanya Mazoezi ya Muda Mfupi (Pomodoro Technique)
Usijilazimishe kusoma masaa manne mfululizo. Gawanya muda wako kwa vipindi vya dakika 25–30, kisha pumzika kwa dakika 5 au 10. Njia hii husaidia ubongo wa mwanadamu kuwa makini na kuepuka kuchoka haraka.
7. Tumia Mbinu za Mnemonics na Storytelling
Hizi ni mbinu za kukumbuka kwa kupitia mifano au hadithi kwa mfano kama unajifunza hatua 5 za kitu fulani, tengeneza kifupi chake yaani acronym au hadithi fupi inayojumuisha hizo hatua kama ilivyo kwneye hesabu tunasema MAGAZIJUTO au BODMAS. Ubongo huwa unakumbuka hadithi kwa urahisi zaidi kuliko namba au orodha ndefu.
Kumbukumbu sio suala la kusoma mara nyingi pekee, bali ni jinsi unavyoshirikiana na maarifa hayo unayoyapata. Ukiunganisha mbinu hizi saba kujipima, kurudia kwa vipindi tofauti tofauti, kuelezea kwa undani, kufundisha, kutumia picha, kupanga muda vizuri, na kutumia mnemonics basi unaweza kuongeza uwezo wako wa kukumbuka hadi zaidi ya 80% za kitu ulichosoma.
Jaribu leo hii, na utaona tofauti kubwa katika jinsi unavyohifadhi na kutumia maarifa yako.
Habari njema ni kwamba kuna mbinu za kitaaluma na za kisaikolojia zinazoweza kuongeza uwezo wako wa kukumbuka. Ukitumia mbinu hizi, unaweza kukumbuka zaidi ya 80% ya kitu ulichokisoma.
Hapa kuna mbinu saba rahisi lakini zenye matokeo makubwa:
1. Tumia Active Recall (Kujipima)
Badala ya kusoma maandiko mara nyingi, jaribu kujipima. Funga kitabu au article unayoisoma kisha anza kujiuliza maswali kama vile: “Nimekumbuka nini hapa?”
Kwa kufanya hivi, utalakuwa unaulazimisha ubongo wako kurudisha kumbukumbu za ulichokisoma badala ya kuishia kuzipokea tu na kusahau. Utafiti unaonyesha hii ndiyo njia bora zaidi ya kuimarisha kumbukumbu.
2. Fanya Spaced Repetition (Kurudia kwa Vipindi)
Usisome mara moja kisha uache. Gawanya muda wa kusoma na kurudia kidogo kidogo kile unachosoma kila baada ya siku chache. Kwa mfano ukisoma leo, rudia tena kesho, kisha baada ya siku tatu, wiki moja, na kadhalika. Mfumo huu husaidia kumbukumbu kubaki kwa muda mrefu.3. Changanua kwa Ufafanuzi (Elaborative Learning)
Usijifunze kwa kukariri tu. Jiulize maswali kama:- Kwa nini hiki ni muhimu?
- kinaunganishaje na kile nilichojifunza kabla?
Hii husaidia ubongo kuhifadhi kumbukumbu kwenye mtandao mkubwa wa maarifa badala ya kukaa peke yake.
4. Fanya Mazoezi ya Kufundisha (Teach Back)
Ukimfundisha mtu mwingine kitu ulichokisoma, akili yako inalazimika kukieleza kwa lugha rahisi. Hii inakufanya maarifa yako uliyoyapata yawe kwenye kumbukumbu ya kudumu.Kama huna mtu wa kumfundisha, jitengenezee video au andika maelezo mafupi kana kwamba unamfundisha mwanafunzi.
5. Tumia Mind Maps na Michoro
Ubongo hupenda picha kuliko maandishi marefu. Jaribu kuunda mind map, mchoro, au flow chart.Hii itakusaidia kuona uhusiano wa mawazo uliyonayo na kuunganisha key points kwa urahisi.