Russia huwa wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa ya mbali.
2. Misafara mikubwa ya kijeshi yenye kila kitu.
Ukraine wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa mafupi mafupi.
2. Kujitawanya katika makundi madogo ya askari wenye silaha ndogo ndogo.
Kila mbinu ina faida na hasara zake, tatizo ni namna unavyoitumia hiyo mbinu. Kwa mfano, Mbinu ya Russia ya kutumia makombora ya masafa ya mbali imeishia kulenga majengo ya kiraia ambayo hayana tena watu ndani yake au kuua raia wasiokuwa na hatia kuliko wapiganaji halisi, kwa kuwa Ukraine ilishajipanga kwa hilo muda mrefu kabla ya vita kuwatawanya wapiganaji wake maeneo yasiyo rasmi.
Pili mbinu ya kutumia misafara mikubwa yenye kila kitu ililenga kuyachukua maeneo ya Ukraine na kuyakalia moja kwa moja, lakini lengo hilo limekuwa ni hasara kwa Russia baada ya kukuta baadhi ya maeneo miundo mbinu ya madaraja kubomolewa kabisa kiasi cha kuwafanya kukaa siku kadhaa eneo hilo wakijipanga kuvuka, kuishiwa nishati, chakula, kuzungukwa ghafla na makundi ya askari wa Ukraine kiasi cha kukosa nafasi ya kutorokea nk. Waza tu, kikosi cha Askari 2000 wa Russia, wakiwa na vifaru 30, magari makubwa 60, magari madogo 30 halafu kijikute kimekwama kijiji kimoja ndani ndani huko kwa siku kama saba hivi, hakuna umeme, maji, mawasiliano ya uhakika, hakiwezi kusonga mbele maana daraja la kuvuka mto limesambaratishwa vibaya, halafu kinapata habari kuwa kimezungukwa pande zote na vikundi kama 10 vya wapiganaji wa Ukraine vyenye askari 20 kwa kikundi, wakiwa na bunduki, drones, makombora ya kubebwa begani ya masafa mafupi, na wako kama 3km tu toka eneo walipo. Nini kitafuata kwa Russia? Jibu ni moja tu, askari wote 2000 watatawanywa pande zote, vifaru na magari vitaachwa eneo moja kwanza, na katika hali ya kawaida huenda nusu ya askari wa Russia wataangamia. Na hicho ndio kinaendelea Russia kwa sasa.