Mbinu bora za kivita: Russia and Ukraine war case

Wewe una uhakika kama kuna vita kati ya Russia na Ukraine?
 
Malezo yako yana upungufu fulani. Unashindwa kuelewa kuwa Nchi za Magharibi zimeanza kuisaidia Ukraine baada ya kuona udhaifu wa Urusi na uwezekano wa Ukraine kushinda vita hiyo. Msaada wa kwanza kabisa wa Marekani ilikuwa ni kumpa hifadhi Rais wa Ukraine na familia yake nje ya nchi, lakini yeye akajibu haihitaji ride ya kuondoka Ukraine bali anahitaji risasi za kupambana na mvamizi.

Urusi ilitegemea sana vitisho kwa kudhani kuwa ikija na askari wengi sana na vifaru vingi basi serikali ya Kiev itaogopa na kukimbia, hivyo Putin angesimika serikali ya kibaraka wake Yakunovych aliyepinduliwa miaka tisa iliyopita. Baada ya Ukraine kumobilize raia kupinga uvamizi huo, urusi ikajikuta imeshtukizwa kuwa haikuwa imejiandaa kukumbana na mapigano ya ana kwa ana. Jeshi la Urusi halina mbinu nzuri za kupigana ana kwa ana, linatumia mbinu za kizamani sana za kufyeka kila kitu kwa kutumia mizinga ya masafa marefu lakini wanapokumbana ana kwa ana wanashindwa. Limekuwa ni jambo la kawaida sana kuona jeshi la urusi wanauwawa au kutekwa kwa wingi kwa mpigo kwa sababu ya kutokuwa na mbinu nzuri za kivita. Weakeness hizo ndizo zimesababisha nchi za Magharibi kuona kuwa kumbe Urusi ni paper tiger lakni hawana ubavu wa kupigana, ndiyo maana wakaanza kuipa Ukraine misaada ya silaha.
 
Maelezo mazuri na ndo maana vifaru vingi unakuta watu hawapo
 

Imagine msafari wa vifaru mkubwa kama wa kutoka Dar kulekea Chalinze unaongozana kwenda kuiteka Iringa,bila kuwaza je madaraja yakivunjwa watafikaje hata Morogoro na kujiokoa kurudi Dar?
Ndo walichokifanya msafara mkubwa unaelekea tu Kiev kama harusi bila kujali Ukraine wana jeshi pia ,mwisho wa siku mbinu waliyobakiwa ni kurusha tu makombora hovyo kwenye majengo ili kuogopesha raia ili wajiokoe
 
Plan ya Russia ilishafeli ,ndani ya masaa 72 waliyosema wamefeli bila hata nchi za magharibu kutoa silaha ,karibia wiki mbili silaha bado haikuanza kuingizwa Ukraine
 
Kama ukraine ataendelea kupewa siraha anazopewa
hii vita sio yakuisha hivi karibun,
 
Hoja zako zimekaa kishabiki sina haja ya kukujibu.
 
Kama ukraine ataendelea kupewa siraha anazopewa
hii vita sio yakuisha hivi karibun,
... sote tunakubali Ukraine ni very weak by all aspects kwa Russia; hilo halina mjadala. Kwa hiyo ili vita iishe haraka Ukraine isipewe msaada ili kumrahisishia mrusi kazi ya kuiteka na kuikalia kimabavu?
 
Plan ya Russia ilishafeli ,ndani ya masaa 72 waliyosema wamefeli bila hata nchi za magharibu kutoa silaha ,karibia wiki mbili silaha bado haikuanza kuingizwa Ukraine
Punguza ushabiki vita sio mpila kusema ina muda maalumu.
Nyinyi ndio huwa mnaharibu nyuzi za watu kwa kuendekeza ushabiki.

Srovakia,Jamuhuri ya check na Poland ni mataifa ya kwanza kupeleka silaha siku ya pili tu baada ya vita kuanza na hata kabla ya vita Ukraine ilikuwa inapokea maelfu ya tani za silaha kutoka nchi za magharibi karibia kila siku.

Hata jana raisi wa Ukraine alisema kuwa ili Ukraine iweze kupigana na Urusi kwa muda mrefu inategemeana na msaada gani atakao pewa na nchi za magharibi tofauti na hapo hawataweza na watashindwa.
Sasa tumsikilize nani kati yako na raisi wa Ukraine?

Ukraine mpaka sasa imesha pokea silaha zenye thamani ya 30$bilion tangu vita kuanza hivi unajua hizo silaha ni nyingi kiasi gani?
Na je unadhani Ukraine ingekuwa na hali gani iwapo isingewa hizo silaha?
 
Ukraine anatumia shock tactics kivita

Ambayo ni offensive maneuver which attempts to place the enemy under psychological pressure by a rapid and fully-committed advance with the aim of causing Russians combatants to retreat.
 
kwani Russia walipokuwa wanavamia hakujua outcomes? Unaingiaje kwenye vita ambayo baadaye unalalamika kuwa mwingine anasaidiwa?hawakujua hayo walipokuwa wanaanza?
 
Naona msaada wa silaha umeshatosha.Sasa wapeleke watu kwa sababu majeshi ya Ukraine ikiwemo kikosi kilichoitwa hatari sana kile cha Azov batallion wameshaangamia.Ukisikia askari 26000 wa Urusi wamekufa ujuwe humo ndani kuna wengi zaidi wa Ukraine na wanawaficha ndani ya hesabu ya maiti wa Urusi.Haya mabomu ya hypersonic unadhani yanatua mbugani.Ni kwenye kambi za waukraine. Na iwapo hawawezi kupeleka watu basi Urusi ikaze kamba tu kiuchumi na makombora ya masafa marefu mwishowe NATO watasambaratika.
 
kwani Russia walipokuwa wanavamia hakujua outcomes? Unaingiaje kwenye vita ambayo baadaye unalalamika kuwa mwingine anasaidiwa?hawakujua hayo walipokuwa wanaanza?
Kwani kuna aliye lalamikia mbona kichwa chako kimejaa maji badala ya akili.

Mtoa mada kaleta hoja ndio tunaijadiri na sio kulalamika.
 
Kama ilivyo kwa upande wa pili hata wewe pia ni blinded ni Russia military superiority kuliko uharisia wenyewe. Ukiwa na mahaba au chuki basi maoni yako yanakuwa niyakihisia kuliko ukweli wenyewe. Kama ilivyo mabeberu ana tabia ya kumuonea mdogo na kumuogopa mkubwa. Jiulize mbona russia kavamia ukraine na si Poland ambae ni member wa nato, jiulize pia mbona nato members wanapeleka silaha na si askari. Hapa ukileta ushabiki utakuwa muhenga
 
Kwani kuna aliye lalamikia mbona kichwa chako kimejaa maji badala ya akili.

Mtoa mada kaleta hoja ndio tunaijadiri na sio kulalamika.
uwe unajibu kwa staha matusi kila mtu anaweza na siyo kila mtu wa kumtusi
 
Ili ushinde vita Yeyote chino ya anga mzima Usheheni Kindakindaki mambo haya!
1-Watu
2-Uchumi
3-Silaha
Uchumi ni asilimia ndogo sana kwenyevita watu mbinu na silaha ndyo Jambo la msingi alafu Ukrein siyo nchi ndogo kama nchi za kiarabu

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Russia harushi makombora ovyoo makombora mengi yamelenga target ndyo maana unaona jeshi la ukrein nguvu ya anga na mizinga limepunguzwa nguvu Kwa asilimia 70 makosa ya Rusia ni kwenda kwenye vita bila kuaribu miundo mbinu ya msingi Kwa Ukrein mbinu ambayo alikuja kuitumia baadaye. Kwenye phase 2 na yote ni sababu alienda kufanya operesheni bila kujipanga Kwa vita kamili kubadil mbinu na kuchukua maeneo ya mashariki ni Jambo la msingi kwake kuliko kung'ang'ania kuchukua Kiev

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…