MBINU MBADALA YA KUSAFISHA JF: Tuungane kuwazika "Cyber Troops" kwa kutumia kitufe cha "Ignore"

... Haya bwana, sisi kina Baba Levo tuwaambie nini wataalam wa AI!!? 😅 ... nilikuwa najaribu tu kuwa mjanja wa mitaani wa zama za mawe 'CAVEMAN' miye!
 
Mi nililijua hili na kuanza kulitekeleza siku nyingi huko.

Ninapoipima hoja ya mtu na kujiridhisha kwamba huyu ni chawa, hapo hapo bila kuwaza mara2, nakungunta ignore kubwa.

Kina tantalila na wengine mfano wake nishamalizana nao siku nyingi sana na nishapumzika kutwishwa stress mie.
 
... Haya bwana, sisi kina Baba Levo tuwaambie nini wataalam wa AI!!? 😅 ... nilikuwa najaribu tu kuwa mjanja wa mitaani wa zama za mawe 'CAVEMAN' miye!
Kishimbe wa Kishimbe Pamoja sana mkuu! Shukrani sana kwa uungwana wako, kwa kupokea hoja hii kwa ucheshi, na kwa kukubali mabadiliko ya kiteknolojia kwa namna hii. Ni jambo la kiungwana sana kuona jinsi unavyoenda na wakati, kwani sote tunajifunza kila siku jukwaani hapa ili kulinda ustaarabu na amani yetu ya akili.
Sasa mkuu wangu, tunaomba utusaidie pia kuwaelimisha na kuwavuta marafiki zetu Kraang na BORNNAGAIN ili nao waje huku karne mpya ya kidijitali. Wasaidie kuelewa kuwa kitufe cha 'Ignore' hakipo kwa ubaya, bali ni zana ya kisasa ya kusaidia kila mtu kuchagua kile kinachomfaa kwenye screen yake bila kuingilia uhuru wa mwenzake. Tuko pamoja sana mkuu, na uwe na wakati mwema
 
Kiukweli Tangu nimejua kuweka ignore, basi maisha yangu yamekua mepesi sana.
The mission 2017 Umemaliza kila kitu mkuu! Hiyo ndiyo siri kubwa ya kufurahia mitandao ya kijamii siku hizi.
Unatumia bando lako, unatumia simu yako, na unachagua kwa uhuru kile kinachoingia kwenye macho yako. Kulinda amani ya akili ni jambo la msingi sana. Safi sana kwa kushiriki ushuhuda huu mzuri!
 
Tatizo la kiufundi lipo kwenye utambuzi wa mhusika kuelewa kama yupo kwenye ignore list yako!

Wataalamu wa App hii wangetengeneza unapo muignore mtu naye ajue kabisa.

Wajinga jinga na wote wenye harufu ya chawa, akili zingeliwasogea haraka.
 
kweli kama vile X zamani Twitter unaleta ujinga unakula block
 
Noted

Homeboi
 
Noted
Homeboi
 
Noted
Homeboi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…