Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Wasalaam ndugu zanguni nyote.
Uzi wa Leo sio wa kinoko, ila tu tufundishane mbinu mbalimbali ambazo watu hutumia kuficha utajiri wao, hasa ule ambao wameupata kinyume na tarabu, au kwa njia zisizo halali na kadhalika.
Nitaleta Visa kadhaa .
Kisa Cha Kwanza
Kisa Cha Pili
Kisa Cha Tatu
Kisa Cha Nne
1. HELA ZANGU NI ZA MAJINI, PIA NINA MABWANA WAWILI MOMBASA, KAMA NA NYIE MNATAKA UTAJIRI TWENDE NIWAPELEKE.
Hiki ni kisa cha bwana mmoja, yeye aliajiriwa Benki moja kama mhudumu/ mesenja, akiwa na jukumu la kutumwa shughuli mbalimbali za kiofisi. Na kutokana na ukubwa na wingi wa matawi ya Benki hiyo, huyu mhudumu tumuite kwa jina la uficho Mbususu, alipewa gari ili kurahisisha shughuli zake.
Hiki lilikuwa ni kipindi cha utawala wa uncle SCAR na marafiki zake, Mafisi yenye uchu na uroho wa ajabu, wakijulikana kwa majina Shenzi, Banzai na Ed.
Mafisi haya yalihakikisha yanakula kila kilicho mbele yao, na nchi nzima ikawa Chukua Chako Mapema.
Basi hiyo Benki ilikuwa ya umma, huyu ndugu Mbususu aliyokuwa akitumikia.
Wakubwa wa Benki Ile nao wakaona wasiwe mafala, wakatengeneza mirija yao ya uvunaji wa mapesa kutoka kwa kina Zakayo na kutoka kwenye ugunduzi wa Nicola Tesla, kila siku wakawa wanavuta zaidi ya milioni mia.
Mbususu alikuwa akipewa hundi, anachukua pesa taslimu, na kuzigawa kwa wakubwa, kisha yeye anabaki kama na tumilioni tuwili au tutatu kila siku.
Kutokana na hela hizo Mr. Mbususu akanunua tugari kadhaa, tukafika kama 12, akajenga jumba la kifahari ufukweni.
Kosa linatoka.
Basi siku moja Mr. Mbususu akaamua kuyakatia bima Magari yake, akaona bima ya Bei nafuu ni pale Benki kwao. Akaenda kukata bima huko.
Mkataji bima akashtuka, huyu mesenja Magari 12 yote yako kwa jina lake kayapataje? Hela kapata wapi?
Basi kwa Siri akawajulisha idara ya ulinzi na usalama ya Benki. Idara ikaanza kumchunguza bila Mr. Mbususu kujua.
Idara ikagundua kuwa Mr. Mbususu amejenga jengo Hilo kwa kupitia mkandarasi wa Kichina, wakadata kabisa.
Basi mkuu wa idara akaamua Mr. Mbususu akmatwe, ahojiwe na afunguliwe mashitaka ya kuibia Benki.
Basi ilikuwa asubuhi moja tulivu, Mr. Mbususu akapigiwa simu kwamba anahitajika ofisini kwa Mkurugenzi Mkuu wa idara ya ulinzi na usalama ya Benki.
Mr. Mbususu akajua ni majukumu ya kawaida, akaitika wito.
Alipofika kwenye ofisi hiyo akashangaa receiptionist Yuko serious sana hana utani Kama siku zote, na anamhudumia kama anamhudumia mgeni mahsus, akamuuliza kama atapenda kahawa, chocolate, cocoa, Milo au chai, Mr. Mbususu muda wote huu yuko kwenye bumbuwazi.
Mara punde akatokea afisa mmoja ambaye wanafahamiana sana, lakini kwa ajabu naye akajitambulisha kisha kasema Nahitaji kufanya mahojiano na wewe.
Afisa akamweleze juu ya uchunguzi wao na akataka aseme amepata vipi Mali hizo.
Mr. Mbususu akasema kwamba Siri ya utajiri wake ni kwamba ana majini ya kumuingizia hela, na pia ana mabwana wawili Mombasa, Waarabu hao wana hela kinoma.
Afisa akawaita polisi, polisi wakamchukua Mr. Mbususu na kumpeleka central ambalo walimtesa sana na kumlazimisha atoe Siri ya utajiri wake. Msimamo wa Mr. Mbususu ulikuwa ulele, hela za majini na mabwana wawili Mombasa, Kama na nyie mnataka nitawapeleka Mombasa, Tena Waaravu wanasema watz ni watamu sana, alisema Mr. Mbususu.
Mr. Mbususu aliwaeleza polisi kwamba yeye ni mesenja, hana kompyuta, hashiki hela wala Hana funguo za strong room je kaibaje hela? Akawaomba polisi wamfafanulie njia anayoitumia kuibia Benki.
Baada ya majadiliano marefu kati ya polisi na Benki, wakaona hamna ushahidi wa moja kwa moja wa Mr. Mbususu kuibia Benki, Mr. Mbususu akarudishwa kazini. Aliporudishwa kazini Mr. Mbususu akaishtaki Benki akitaka imsafishe kutokana na tuhuma za wizi na pia imlipe kwa mateso aliyoyapata ikiwa ni pamoja na kupigwa, mateso ya kuingiziwa chupa kubwa ya bia, kupigwa shoti za umeme etc.
Mr. Mbususu akalipwa shilingi bilioni 1.2
Maisha yake yako safi kabisa, ila like dili la wakubwa likaja kushtukiwa wakubwa wakatomuliwa kazini.