Mbinu mbalimbali ambazo hutumiwa na watumishi wa umma, wafanyabiashara nk kuficha utajiri wao

KISA CHA PILI.

KISA CHA MTOZA USHURU, MAJUMBA, VIWANJA, MASHAMBA NA MATENKI YA MAPESA.

Huyu bwana ndugu Zakayo, yeye aliamua kuficha ukwasi wake kwenye ardhi.

Akasogea jirani na Kazinzumbwi na Zingiziwa, akachikua eneo kubwa sana.

Akajenga nyumba nyingi sana zaidi ya 70, na kuna mapesa yake akayaficha nyakati za usiku kwenye matenki ya kuhifadhia maji.

Basi haya yalifnyika kipindi cha Chukua Chako Mapema ucle SCAR akitawala kwa kolabo na Mafisi matatu yenye uchu na uroho wa ajabu ambao ni Shenzi, Banzai na Ed.

Utawala ulipobadilika akaaingia mtawala mpya, Fundi mwashi.
Akamtia misukosuko huyu mwamba na kumpora hela zake kibao, akamwachia huru mwaka 2017.
 
Nasinzia nikikuwaza.., sio wewe, nawaza pesa
 
Ndio mkopo umezalisha faida nikajengea na kununua magari.
Mkopo ukizalisha faida maana yake wewe unafanya biashara?Basi tuonesha risiti za TRA unazolipia kodi tulinganishe utajiri wako kama unalingana na kodi unayolipa.Vp hapo utatoboa?
Smtz serikali zakizandiki zikitaka kukuamulia kukufilisi huwa hazikosi sababu.
 
KISA CHA TATU.

KISA CHA KIJANA BAROBARO NA MAISHA YA CHINI KABISA (FUKARA) KUMBE NI TAJIRI MKUBWA.

Kisa hiki chamhusu kijana mmoja shababi mwenye nguvu zake za kutosha kumsukuma tembo kwa mikono yake.

Kisa hiki kilitokea kwenye jiji la maraha, jiji lililoporwa ukuu wa nchi na kubaki kuwa makao makuu ya ubuyu na Visa vya kina Manunu, Mkadeda, Mshana Jr na wengine wengi walio maarufu. Makao Makuu ya Masupa Staa wa instagram.

Huyu kijana tumuite Mr. Mbunye, yeye alikuwa ni mwajiriwa wa shirika moja kubwa la mifuko ya hifadhi za Jamii.

Shirika hili lilikuwa mahiri kwa kununua ardhi kwa Bei ndogo kisha Hudanganya kwamba wamenunua kwa Bei kubwa, chenji ziliingia mikononi mwa wajanja wachache na miongoni mwao alikuwa ni huyu Mr. Bunye.

Walichokuwa wakifanya mbali na kudanganya gharama za manunuzi, ni pamoja na kuchelewa mafao ya wastaafu, zile hela za wastaafu zilikuwa zikiingizwa kwenye akaunti binafsi za wajanja wachache akaunti za fixed account, hela ikisha mature riba huliwa na wajanja wachache.
Waliendelea na mchezo huu kwa miaka mingi sana ya ule utawala wa Chukua Chako Mapema uncle SCAR na rafiki zake mafisi wenye uchu na uroho wakiongozwa na Shenzi, Banzai, na Ed.

Alipo ingia mtawala mpya Simba, alianza kufukua makaburi, kuanzia mradi ule mkubwa uliopo ng'ambo ya Bahari, majengo marefu katikati ya jiji, na sehemu nyingine.

Uchunguzi huo ukagundua madudu ya kutisha, Mr Mbunye naye alikuwa na magunia ya mapesa kayahifadhi nyumbani.

Mr. Mbunye machale yakamcheza, akaenda kununua kigari kikirikuu, akachukua nyraka zake zote muhimu, akazitia kimpangilio kwenye gari, akachomelea bodi lote kimadhubuti, akazuga na kakufuli.

Akaendesha hicho kigari Hadi kwa mjomba wa mke wake huko Ngudu, akamwambia hii gari nimeinunua kwa jamaa yangu ni mbovu, nikiitengeneza hapo nitakapo pata pesa nitaitengeneza kisha wewe itakuwa unitumia.

Jamaa akaing'oa hiyo gari magurudumu yake. Akaiweka juu ya mawe, ikapigwa na vumbi la kutosha.

Kamatakamata ikaanza Mr. Mbunye naye akakamatwa, uchunguzi ukafanyika, wakampekua kila mahali, kila ndugu na jamaa yake akapatwa misukosuko, lakini hakuna aliyekashtukia kale ka gari kabovu juu ya mawe.
Muda mrefu wa uchunguzi ukapita na hakukuwa na ushahidi wa kumtia hatini.

Mr. Mbunye akaachiwa huru, akarudishwa kazini.

Kazini akaomba apunguzwe kazini ili akapate nafasi ya kujitibu.

Akalipwa mafao yake yote. Akakarudia kagari kake kwa shangwe.

Mr. Mbunye akaibuka kidedea bila kushitukiwa.

Sasa ana biashara zake halali za uchukuzi na clearing and forwarding akiwa na malori mengi sana ya mizigo na mafuta, ana kampuni kubwa ya kuzimisha mitambo ya ujenzi, anakula hela yake kiulaini.
 
@Bujibuji hii code ngumu sana aisee..
 
Back
Top Bottom