Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kama wewe ni mfanyabiashara unayepokea malipo kwa njia za kidigitali (Lipa Namba, Benki, au Mtandao wa Simu), kuwa makini sana usije ukapigwa! 🚨
Kumeibuka mbinu mpya ya utapeli ambapo matapeli wanatumia Akili Mnemba (AI) na programu za kughushi ili kuwapiga wafanyabiashara wanaopokea malipo kwa njia za kidigitali kama vile Lipa Namba au Benki. Mchezo huu mchafu umefichuka hivi karibuni mjini Dar es Salaam baada ya mfanyabiashara mmoja wa huduma za kuagiza bidhaa kuingizwa mkenge na kutapeliwa takribani Tsh. Milioni 47.
Kutokana na kasi ya maendeleo ya teknolojia, matapeli hawa wamegundua mianya mipya ya kutumia udhaifu wa wafanyabiashara wanaoweka imani yao yote kwenye picha za risiti bila kuhakiki akaunti zao.
Mbinu wanayotumia ni ya kijanja lakini yenye hatari kubwa sana.