Mbinu mpya ya Utapeli Mjini: Mfanyabiasha usitume au kukabidhi Mzigo kwa kuangalia Screenshot ya Risiti!

Ujumbe muhimu kwa wafanyabiashara ni huu: usiamini risiti au screenshot pekee. Thibitisha malipo moja kwa moja kupitia taarifa ya benki, akaunti ya Lipa Namba, au ujumbe rasmi kutoka kwa mtoa huduma kabla ya kumkabidhi mteja bidhaa au huduma.
 
Hata huyo alietapeliwa mil 47 kwa kuangalia screenshot ni fala vilevile!

Nimeiona hiyo clip hapo chini..HATA HIVYO.. huyo jamaa wa TikTok stori zake nyingi 99💯 HUWA NI ZA KUTUNGA

HUWEZI MTUMIA MTU MZIGO WA MIL 47 KWA KUANGALIA SCREEN SHOT PADIPO KUHAKIKI SALIO!
 
Daaah hakuna sms kwenye mitandao ya simu na bank? Basi kucheki balance ada ni shilingi 50. Unatapeliwa 47 million.
 
Unatumaje bila kudhibitisha kama imeingia kwenye account? Kama ni mobile banking slip ina QR codes, kama ni manual slip inabidi isome kwanza

Huko ni kujitakia
Vipi tiketi za mabasi za online ambazo unatumiwa sms tu
 
Vipi tiketi za mabasi za online ambazo unatumiwa sms tu
Kwamba zina shida gani, kwa nani, mteja au wakala wa bus?
Ajent mpuuzi tu ndio anamkatia mtu tiketi kabla ya kutuma pesa, tofauti na hapo lazima awe mteja wako wa mara kwa mara na unamuamini kwa hadhi yake nauli ya 60k kwake sio kitu cha kukimbia. Tofauti na hapo atume hela kwenye simu ndio wakala afanye booking.
Mfano mimi naweza kukatiwa tiketi hela naenda kumpa stend kwa sababu anajua sina njaa

Kwa mteja, tiketi ni online generated tena anaweza kujikatia mwenyewe online na kulipa mwenyewe booking ikakamilika. Huhitaji hako katiketi maana sms ya tiketi inasoma, na ukifika kwenye bus wanaweza kukutolea hardcopy
 
Vipi hazi editiki
 
Nauli na ninakoenda
Wewe jamaa sijui unatokea kijiji gani! Kwanza ajent unayemtumia nauli kabla ya tiketi ni mtu unayemuamini na unafanya nane miamala mara kwa mara, huyo ni mwehu mpaka aedit nauli? Pili katika mazingira ambayo huna ajent reliable kwa nini usikate tiketi mwenyewe kwenye mtandao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…