Mbinu ya CHADEMA ya "Win the crowd, and fate will kneel before you" ipo 70% kuelekea kuiangusha CCM

Mbinu ya CHADEMA ya "Win the crowd, and fate will kneel before you" ipo 70% kuelekea kuiangusha CCM

Katika uhalisia, uchaguzi ukiwa huru na wa haki kabisa, ukifanyika hata leo, CCM haiwezi kupata hata 30%. Huo ndiyo ukweli. Na hata wao wanajua, ndiyo maana wameamua kuutegemea ukatili.

Utekaji na mauaji ya Oct 29, yameifanya CCM na serikali ichukiwe zaidi ya alivyochukiwa hata mkoloni, maana mauaji yaliyofanyika yalikuwa ya kutisha na makubwa, zaidi hata ya mara elfu moja yaliyowahi kufanywa na utawala wa mkoloni. Ndiyo maana leo hii ikutokea muna option ya kuchagua kutawaliwa na CCM au mkoloni, wengi wataona aheri kutawaliwa na mkoloni. CCM na Serikali wanachukiwa kuliko kitu chochote kwa sababu uovu walioufanya haujawahi kufanya ni mwovu yeyote tangu kuanza kwa taifa la Tanganyika naTanzania.

Hapana mkuu inategemea watakuweka nani.

Kwa sababu kizazi hiki hakiangalii chama kinaangalia MTU.
 
Je CCM inaweza kubadilika?
JPM alitaka kuibadilisha CCM alifanikiwa kimiundombinu lakini kiutu alishindwa
Sio kwamba alishindwa bahati mbaya, bali alikuwa anapambanana na nyakati. Ni sawa na kuwa mzee, kisha ukawa hutaki unapakaa nywele dark & lovely ili uonekane kijana. Hata Magufuli kupora uchaguzi hakupora kwa bahati mbaya, alijua uchaguzi wa halali bado wapinzani wangepata kura nyingi, jambo ambalo lingeharibu propaganda yake ya kukubali na ccm kuwa bora.

Ni vile sasa uongo imekuwa sehemu ya ccm, lakini wakati wa Magufuli ndio wananchi wengi walipoteza imani na zoezi la kura. Mama Samia naye akaiga tembo kunya kwenye uchaguzi huu, matokeo yake kapasuka msamba.
 
Mitandao inapenda content za hasira na ukosoaji, ndiyo maana inaonekana kama upande mmoja una nguvu zaidi.

Lakini hiyo ni reflection ya platform dynamics tu.
Issue ni CONTENT, AGENDA na MAAMUZI.

Kwasasa huyo BIBI YENU, watu amabo kwenye jamii taswira zao ni mbaya, yeye ndio watu wake anawapenda.

Kila tatizo, hata la MBU kutua kwenye PUMBU anachoona ni KUPIGA NYUNDO tu.

Alipewa nafasi kubwa sana kwa iweao wake, halafu kibaya zaodow anaojifanya kumsaidia, badala kumshauri wanafanya UCHAWA na kumpa anachotaka.
 
page ya ikulu comment Mia moja za Aina mo
 
CCM vs CHADEMA..no 21 sio wote wanaopinga taarifa ya tume ni CHADEMA hilo ulijue na kuipinga haimanishi kusaliti chama..lingine ukipita vijiwe mbali mbali utagundua wengi wanayoisema vibaya CCM na serikali ni CHADEMA, lakin idadi yao haitikisi CCM...Vijiwe vingi CCM ni kama hawapo kabisa na wala hutowasikia wakichangia chochote, lakini, haimanishi kwamba hawapo kabisa kwa maana hyo CHADEMA wanasikika kwasababu bado wanahasira na uchungu moyoni....swala la CHADEMA kuiangusha CCM bado saaaana labda vizaz na vizaz vipotee vije vizazi vingine na wakati huo CCM imeshapata mbinu mpya. Labda CCM yenyewe ijibwage chini ndo CHADEMA isimame kidete...ukitembea ngazi za mashina huko chini CHADEMA haijajizatiti bado saana...CCM itaondolewa na Wananchi wa vyama vyote na wasio na vyama kama wananchi watapewa nguvu kubwa kwenye katiba ijayo au mfumo wa vyama ukisukwa upya, lakini kwa CHADEMA Yenyewe haiwezi na haitoweza kwani haijajizatiti vizuri kuanzia ngazi ya shina hadi vijana..tukumbuke kuna viapo vya CHAMA.
Haya maelezo yako marefu, uhalisia unakataa. Ccm inakataliwa na vijana wa kizazi hiki, maana kinaonekana ni chama cha wazee. Ni sawa na vijana wa sasa useme watapenda nyimbo za Ottu jazi maana wana mabadiliko, waache kupenda za kizazi chao eti kisa zina lugha ngumu. Never on earth. Vijana wa sasa hawana huo upuuzi wa toka kwenye matawi? Ukiona Bado unawaza kuhusu matawi, ujue bado unawaza kizamani sana.
 
Nionyeshe KANU ya Kenya ilipo, maana hata makada wake walikuwa wanasema hivi hivi. Nyakati hizi haziibebi vyama vya ukombozi. Tazama wanachokutana nacho FRELOMO, ANC nk.
Endelea kukariri mambo
 
Mbinu ya CHADEMA YA "Win the crowd, and fate will kneel before you" IPO ASILIMIA 70% KUELEKEA KUIANGUSHA CCM.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Katika Falsafs za siasa. Zipo mbinu nyingi Sana za kuishinda serikali iliyopo madarakani.

2. Elewa, Serikali inaweza kutawala nchi, lakini wananchi hutawala na kuamua hatma ya serikali.

3. Falsafa za kitibeli zinasema, Serikali inaweza kuwa na jeshi, pesa, au taasis imara, lakini ikipoteza uungwaji mkono wa watu wengi, uthabiti wake huwa hatarini.

4. Kwa maana hiyo, chunguzi zangu zimebaini mbinu wanazotumia na CHADEMA na wanaharakati zipo well calculated na wanauhakika na kile wanachokifanya.

5. Wanauhakika kwa sababu wanatumaini, Wana pata matokeo mazuri waliyoyatarajia.

6. Unapotawala nchi au unapokuwa umeshika Dola. Moja ya vitu mambo nyeti muhimu ni UMMA. Ushawishi kwa watu. Je watu wanakupenda? Je unakubalika.
Hata uwe na miguvu kama Mungu kama hukubaliki na hupendwi ni matter ya muda.

7. Ndio maana CHADEMA na Wanaharakati wanamatumaini makubwa, Wana ujasiri kwani uwekezaji wao mkubwa wanautumia kujenga ufa, naam kufarakanisha Serikali na umma.

8. Katika uwanja wa vita vya siasa. Kuna kanuni isemayo Win the "Win the crowd, and fate will kneel before you"
Kanuni hii haijawahi kushindwa popote pale. Ni kanuni ya ushindi. Ingawaje inaweza kuchukua muda mrefu.

9. Unateka nyoyo za Watu.
Unaonyesha matendo ya huruma, kuwatetea, kuwapigania watu.
Unaonyesha weledi.
Unawaaminisha na kuwahakikishia maisha bora. Na kuhakikishia mateso waliyonayo yatakoma.

10. Mtu kama Magufuli ali- win Crowd ingawaje yapo makosa aliyoyafanya.

11. Makosa ya CCM na serikali ni kushindwa kuelewa mbinu za kimedani za chini kwa chini za kuangusha mbuyu kwa kutumia Wembe.

12. Propaganda+ Media ni silaha hatari ambayo Chadema na wanaharakati wanazitumia kushambulia na kumsogeza adui yao(CCM na Serikali ) nyuma.

13. Miaka ya hivi karibuni vijana wengi hawafuatilii Media kama Channel za Luningani. Watu wamehamia kwenye Mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na Tiktok.

14. Kama utakuwa Makini, utagundua Wanaharakati waliokinyume na CCM na Serikali wananguvu kubwa kwenye social media ukilinganisha na Wanaoiunga mkono CCM na serikali.

15. Kwa hapa JF top ten ya wenye nguvu kuanzia ya engagement, followers, likes wengi wapo opposite na CCM na serikali.

16. Ukiingia kwenye Facebook na tiktok nako halikadhalika. Wana power na unaweza ku predict future mini kinaenda kutokea.

17. Unaweza Fanya jaribio la utafiti wako. Fanya hivi,
Tafuta mtu asiyejulikana, ambaye hajawahi kutumia mitandao kabisa.
Mpe Scripts aiponde CCM, aiponde serikali kwa kiasi cha kutisha.
Then angalia nini kitatokea.
MTU huyo watu watamjia juu wakimuunga mkono, wakimpenda, wakishare na ku-like post zake.
Ni kwamba umma utakuwa upande wake.

Ikiwezekana watamchangia kwa hiyari Yao wenyewe bila kulazimishwa.

18. Kisha tafuta mtu mwingine unknown person, ambaye hajawahi kutumia mitandao ya kijamii.
Kisha MPE Scripts aipongeze, aipambe CCM na Serikali.
Then angalia reactions za watu. Utagundua hatapata engagement kubwa. Na watakao- engage naye watamtukana Sana.
Hii inaweza kukupa picha kamili ilivyo.

19. Unapo win the Crowds ume win hatma.

20. Nimeangalia MTU yeyote anapojihusisha na CCM na serikali anajikuta kwenye Hali ngumu Sana Hasa huko mtandaoni.
Anashambuliwa bila kujali alikuwa na heshima au mchango gani ndani ya jamii.
Ukifuatilia maoni ya watu mtandaoni utagundua zaidi ya asilimia 70-90 ya watoa maoni hushambulia CCM na Serikali inapotokea mtu anaisifu.

21. Hivi Karibuni kuna sheikhe mmoja mwenye heshima alikuwa akiwakaripia wanaopinga ripoti ya tume ya chande, huku akiwalaani.
Kila nilipoona Ile video kwenye akaunti mbalimbali akaunti zote, Waliotoa maoni walimtukana kwa zaidi ya asilimia 90% Bola kujali dini zao.

22. Jeshi la wananchi nalo lilijikuta kwenye hali ya namna hiyohiyo. Kutukanwa na kupondwa.

23. Tume ya Jaji Chande nayo kama walivyotangaza, matusi zaidi ya 300 yalitumwa kwa SMS. Hiyo ni feedback ambayo kwa watu makini, na Wana usalama lazima waichukue kama sehemu ya kuunda Mkakati wa kufanyia kazi baashi ya issues ili kuwaleta wananchi waiamini serikali na kukiamini chama cha mapinduzi.

24. Pili, hakukuwa na sababu ya kutangaza hiyo feedback ya matusi zaidi ya 300 kwani hiyo kwa waliotukana na wasioipenda ccm na serikali kwao ni positive reinforcement.

25. Zaidi, Hakuna sababu ya kuwakamata waliotukana kwani ni makosa yaleyale yanarudiwa na malengo ya wanaharakati na Chadema yanafanikiwa kirahisi Sana.

27. Katika mapigano ya kisiasa. Mtawala ukimshambulia mpinzani wako alafu umati wakawa wanaimba muache muache, mtawala mwenye akili na mbinu za kimedani humuacha mara moja. Kwa sababu kutomuahia mpinzani wako no hasara na kunaongeza maadui mpaka waliondani yako.
Lakini ukimuachia unatengeneza mazingira ya kuwagawa wapinzani wako makundi mawili.
Wapo watakaoona unawasikiliza na unahuruma, wataanza kukuunga mkono. Huku wengine wataona ni kwa sababu walishinikiza.

28. Nimalize kwa kusema, mambo haya yanahitaji kuangalia kete za mbele kuliko zilizopo mkononi.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Chama tawala kimefanikiwa kuvuka hivi viunzi kwa mtindo wa kutoa matumaini na mabadiliko kila baada ya miaka 10. Sasa hivi kinachoendelea ni kusukuma gurudumu lifike 2030. Kuna uwezekano mbinu ile ile itatumika na pengine ikafanya kazi tena japokuwa kuna usemi kila lenye mwanzo lina mwisho.
 
CCM kama chama cha siasa kilishaanguka miaka kadhaa iliyopita.

Kilichobaki sasa ni dola ndio inayoibeba CCM.

Siku polisi na wanajeshi wa vyeo vya juu wakiamua waiache CCM ijitegemee yenyewe kama chama cha siasa ndio siku itakayotoka madarakani mazima.

Yale maandamano ya Oct 29 hayajatokea kwa bahati mbaya.

Ni picha kubwa ya jinsi gani watu wanaichukia CCM.

Na CCM wanalitambua hilo vizuri sana.

Ndio maana wanawaacha polisi watende wanavyopenda wakijua na wao wanalindwa wabakie madarakani.

It's a win win situation.

NB

CCM IS NO LONGER A POLITICAL PARTY.
Kwa mazingira ya sasa CCM ni redundant mno. Kilifaa wakati wa ukombozi na ujenzi wa utaifa. Kipindi cha mageuzi hawawezi kuhimili.
 
Magufuli hakuna kwenye nchi hii na aliyewahi kutokea aliyeweza ku win Crowds kama yeye.

Mimi sikuwa namkubali kwani nilimuona kama manipulator (mlaghai) na vitendo vya utekaji vilipoamzia kwake.

Lakini huko kwingine alikuwa Bora kuliko hata Wazungu.

Wananchi Weng walirejesha Imani kwa CCM na serikali. Isipokuwa wananchi wenyw mitazamo ya kidemokrasia na Uhuru.

Kama Magufuli angekuwa mzuri kwenye kuvumiliaa wakosoaji wake. Ninakuhakikishia angekuwa Rais wa muda wote kuliko hata Nyerere.
💯
 
CCM ilishaanguka muda mrefu ndiyo maana inatumia dola kubaki madarakani.
 
Unafikiri kwa nini hakuna Tume huru ya uchaguzi kama usemayo ni kweli?

Unajuaa maana ya uwanja sawa, na refa asiwe na upendeleo?
ukiniuliza hvo namimi nitakuuliza hv..Toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi 1992 walikuwa wapi?Kwanini leo ndo waone umuhimu wa tume huru ya uchaguzi? Mfa maji siku zote haachi kutapa tapa...Hiyo tume huru ya uchaguzi nani atakuwa msimamizi mkuu na atawajibika kwanani? bado tutaludi kule kule..kuiondoa CCM ni kufumua mifumo iliyopo kwenye katiba ya sasa na kuludisha nguvu kwa wananchi..lakin msijiaminishe kwamba CHADEMA inauwezo wa kuingusha CCM never! never! never ! mm sipo chama chochote naichukia siasa kwani iliniharibia maisha yangu..
 
Haya maelezo yako marefu, uhalisia unakataa. Ccm inakataliwa na vijana wa kizazi hiki, maana kinaonekana ni chama cha wazee. Ni sawa na vijana wa sasa useme watapenda nyimbo za Ottu jazi maana wana mabadiliko, waache kupenda za kizazi chao eti kisa zina lugha ngumu. Never on earth. Vijana wa sasa hawana huo upuuzi wa toka kwenye matawi? Ukiona Bado unawaza kuhusu matawi, ujue bado unawaza kizamani sana.
Uvccm ni wazee? hapo ndo mnapofeli kwa kujiaminisha uongo wenzemu wanawekeza rika lote nyie mnabaki kusema wanakataliwa na vijana wasasa..ni kweli CCM inakataliwa mdomoni nasio moyoni..chukua hilo.
 
Back
Top Bottom