Mbinu ya kumaliza vita ni kutoongeza wahusika(maadui)

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

1. Panapokuwa na vita baina ya watu wawili njia pekee ya kutopanua vita hiyo ni kutoongeza wahusika.

2. Mbinu nyingi ni kuhakikisha vita haidumu muda mrefu. Kwa sababu vita kadiri inavyochukuaa muda mrefu ndicho hasara na mgogoro unavyopanuka na kuongeza wahusika.

3. Kupigana muda mrefu pia ni kuwapa nafasi adui wasiohusika kuona na kutathmini uwezo wako.

4. Kupigana muda mrefu au migogoro ya muda mrefu hupelekea maadui wengine kama walikuwa wanakuheshimu heshima kwako ipungue.

5. Kupigana muda mrefu ni kuzalisha ujasiri kwa wale waliodhaifu.

6. Kupigana muda mrefu ni kutoa mwanya kwa maadui wa nje kuvamia nchi au familia na kuidondosha.
Familia ambayo Mume na mke wanagombana mara kwa mara ni rahisi adui wa nje kuivamia na kuidondosha.

7. Mapigano ya muda mrefu huwapa mbinu lile kundi dhaifu la kushinda kundi lenye nguvu.

8. Hata uwe na nguvu zipi ukipigana na kundi dhaifu kwa muda mrefu utajikuta unapigwa. Na kuna sababu.
Katika mchezo wa Draft hata uwe bingwa kiasi gani. Ukacheza na mtu anayejua kawaida. Utamfunga michezo 20 tuu ya kwanza then sio ajabu michezo inayofuata utajikuta unaanza kutoa suluhu yaani hamfungani.
Kwa wachezaji wa Draft wanajua hili.

Ndio maana wale mabingwa wa draft hawezi kubali ucheze naye mfululizo michezo mingi. Kwani kiwango na akili yake itastack kama sio kushuka.

9. Hii ni kusema, siku zote ukipambana na mwenye nguvu siku zote aliyedhaifu ndiye ana gain huku mwenye nguvu ndiye ana loose. Dhaifu akili yake huwa active na hujifunza mambo mapya na kutafuta mbinu mara elfu huku aliye na nguvu akiwa palepale.

10. Vita ya Hamas na Israel mnufaika zaidi pale kimedani ni Hamas kwa sababu yeye ndiye anagain huku Israel analoose.

11. Watawala werevu hujua kabisa Mkubwa apambanapo na mdogo basi mdogo ndiye anagain. Hivyo mara nyingi huepuka vita vya muda mrefu na watu dhaifu.

12. Marekani ni taifa kubwa moja ya mbinu zake ni kuwapiganisha maadui zake. Hii ni mbinu inayofanya kazi na kumfanya achukue tathmini akiwa mbali huku akiwa mpiganaji kivuli.

13. Unapotumia mbinu ya kuteka, kupoteza na kuua ni mbinu ambayo itakusaidia tuu dakika za mwanzoni lakini ni shimo refu unalojichimbia mwenyewe. Na mbinu hiyo huongeza mgogoro na kupanua vita.

14. Wazungu sio wajinga kuweka demokrasia. Hakuna nchi zilizopotia umwagaji wa damu, udikteta kama nchi za ulaya.

15. Migogoro ya muda mrefu ndani ya nyumba au taifa huleta mpasuko na utengano.

Siku njema

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
100%
 
Back
Top Bottom