Mbinu ya kutangaza biashara aliyotumia mmiliki wa neel salt

Mbinu ya kutangaza biashara aliyotumia mmiliki wa neel salt

Joined
Aug 8, 2017
Posts
72
Reaction score
84
Habari wakuu...

Leo katika pitapita zangu Mjini Dar es Salaam nikakumbuka Yale Mabango ya Neel Salt yalivokuwa yametapakaa Mji mzima kila barabara wakitangaza Chumvi hiyo,
Kwenye TV nako yalikuwa yamesambazwa Sana,
Watu wakaona kumbe Kuna chumvi hiyo wakaizoea na Kuona ni chumvi ya kawaida Kama chumvi nyingine,
Walisambaza madukani Sana Mpaka sasa ni Chumvi inayouzika na kuzoeleka Kama chumvi zingine...

Lkn Kwa sasa Mabango yamepungua Sana na Kutoweka kabisa na matangazo kupungua kwenye media Kwa Asilimia kubwa...

Dalili inaonesha Mmiliki Tayari kisharidhika na soko na kaamua Kupunguza Gharama za Matangazo Kwa sasa...

AKILI KUBWA SANA ILITUMIKA...
Kuna haja ya wajasiriamali wengine kutumia hii Mbinu.
 
Usiitumie chumvi hiyo (una bahati kusoma post hii)
 
ni kweli mkuu ila matangazo kwenye vyombo vya habari si hela ndogo, kwahiyo inafaa mjasiriamali ajiangalie ananguvu gani na ni biashara gani anafanya na analenga wateja gani
 
Issue sio kwamba ameamua kutoendelea kufanya matangazo. Issue ni kwamba matangazo yake aliyafanya kwa kumtumia marehem King Majuto. Jamaa baada ya kufa serikali ikiongozwa na waziri Mwakyembe waliamua ku-reevaluate ule mkataba na wakagundua kuwa mkataba haukuwa in favour kwa marehemu and so akapigwa stop kutumia matangazo yote hasa yale yenye picha ya marehemu.
 
Halafu siku hizi imechakachuliwa. mchanga mwingi sana kwenye chumvi yake. kuna namna au wajanja wameiba vifungashio wanafungasha chumvi isiyo na viwango. ajitathimini tena.
 
yale yale ya chai jaba ni chai tamu[emoji16][emoji16],sijui kuna chai za ladha ngapi???
 
Issue sio kwamba ameamua kutoendelea kufanya matangazo. Issue ni kwamba matangazo yake aliyafanya kwa kumtumia marehem King Majuto. Jamaa baada ya kufa serikali ikiongozwa na waziri Mwakyembe waliamua ku-reevaluate ule mkataba na wakagundua kuwa mkataba haukuwa in favour kwa marehemu and so akapigwa stop kutumia matangazo yote hasa yale yenye picha ya marehemu.
Mbona alivyokuwa mzima hawakufuatilia ili wamsaidie kupata haki zake?
 
Back
Top Bottom