Mbinu ya Majaliwa kuficha aibu na Kazi ya Serikali ya lazima ya uokoaji

Mbinu ya Majaliwa kuficha aibu na Kazi ya Serikali ya lazima ya uokoaji

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Mimi ni mmoja wa walioamini katika story ya Majaliwa Jackson kijana wa kihaya aliyeokoa abiria siku ile ya ajali ya Ndege ndani ya Ziwa Victoria. Nilipomuona anaongea katika runinga akihojiwa na mtangazaji wa TBC asubuhi baada ya ajali kutokea jana yake nikaamini nilichokiona.

Kijana ameucheza vizuri uhusika wake kadri script ilivyomuelekeza kucheza, mpaka akaalikwa bungeni na akapiga selfie nyingi na warembo wa Sinza, akawa maarufu ghafla na ajali nzima na vifo vya abiria vikapoteza umaarufu.

Serikali imefunika hii aibu kwa gharama za Majaliwa. Na hata kama amepewa pesa za wasamaria wema, ni pesa ambazo hazilingani na fedheha nzima ya ndege kuzama pasipo muokoaji wa maana aliyesomea uokoaji kusogea karibu kabisa na Ndege ile!.

Uokoaji ni jukumu la serikali, na halikwepeki hata siku moja. Anaweza kutumika Majaliwa anayepatikana karibu na tukio na akatumika kuzima uzembe mzima, lakini bado ukweli unasimama kama ukweli kuwa uokoaji ni jukumu la kiserikali.

Ni kazi ya kwanza kufanywa na serikali kwa mlipa kodi anayetoka jasho mchana na usiku ili achangie mfuko wa hazina. Uokoaji sio suala la kuchukuliwa kama ni ziada, hapana, ni jukumu la kiserikali kulinda maisha ya raia wake.

Bima wamesema watalipa, lakini hii haiondoi ukweli kwamba ile ni ajali ya pili kutokea ndani ya Ziwa Victoria, ya kwanza ikiua watu wasiopungua 1,000 mwaka 1996. Hii ni ya ajali ya pili na hakuna chombo cha uokoaji chenye kufanana na serikali.

Yanapotokea matukio kama haya ndipo watu huwa wana haki ya kuhoji manunuzi ya magari ya milioni 400 yanayopishana barabarani nchi nzima na anasa nyingi halafu hakipo kinachomfikia mtu wa kawaida akiwa anasisitiziwa kila mara juu ya umuhimu wa kulipa kodi kila mara!.

Safari hii ametumika Jackson Majaliwa 'kuuwa soo" lakini ni suluhisho dogo na la muda mfupi tu. La kufanyiwa kazi ni suluhisho lenye kueleweka na kukubalika miongoni mwa walipa kodi. Miongoni mwa wanaoumia kugharamia matanuzi ya kila siku ya serikali.
 
Umenena vyema kila mwananchi akiwa wazi kueleza mapungufu ya serikali yetu ndipo itakapoamka usingizini.
 
Haya ni matokeo ya state kuamua Chama kiMoja kushika hatamu KWA Muda mrefu na kuzoea madaraka na kuona hakuna mbadala zaidi yao!

Tungekuwa na utamaduni wa kupokezana vijiti nadhani UJINGA kama huu usinge kuwepo!!
 
Haya ni matokeo ya state kuamua Chama kiMoja kushika hatamu KWA Muda mrefu na kuzoea madaraka na kuona hakuna mbadala zaidi yao!

Tungekuwa na utamaduni wa kupokezana vijiti nadhani UJINGA kama huu usinge kuwepo!!

Hapa umenena ukweli. Huwa najiuliza hao wanaojiita state huwa wanapatikana vipi? Isije kuwa ni lazima uwe na kadi ya ccm ndio uwe state. Ndio maana mimi huwa nasisitiza, machafuko pekee ndio yatarudisha nchi yetu kwenye mstari wa utawala bora na unaowajibika kwa wananchi, na sio kulinda maslahi ya magenge yaliyo ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom