MENEMENE TEKERI NA PERESI
JF-Expert Member
- Mar 11, 2022
- 5,392
- 14,646
Dah kweli wewe mzawa kaka ,msalimie Sana Muddy ,Mimi zamani ile nikikaa mitaa ya Machungwa Ila torori ,keko juu ,Magurumbasi zilikuwa sehemu zangu za kujidai na wazee wahuni akina mzee KyambaKina Matumla wamehama wapo Mbagala. Keko hakuna ambaye hamjui Muddy. Sisi home kulikuwa jirani na Mzee Khasim aliyeimbwa na Muhidin Gurumo
Kumbe hajui kituHuna lolote unalojua
Hao wahuni wako wapoJamaa bado Sana,kwenda kufanya nao zoezi,kujua wazazi wao,kurudi usiku , hahahhaahahah,unawafahamu wahuni kweli,watu wamevurugwa halafu ujipeleke kwenye kambi yao,acha hizo
Huku sisi tuna wasela nnya!.
Kuna watu tumekua kwenye mazingra magumu ya ki geng geng.......Huyu angepata hata mitikas miwili ya huyo mwamba mpaka kifo chake angefuta huu upuuzi wake.
Hahaaa nilikamataga kidemu fulani kumbe ni kidemu cha wahuni.Wagongee mademu zao ili wakuone rijali
Nipo curious kujua ulikua UNAISHI mbagala ipi..Wanasemaga kambi popote
Kuna watu hawawezi kuishi hata siku mbili tu maeneo yaliyopinda, wanaogopa wahuni na vibaka, sijui panya road
Nishawahi kuishi Dar nikiwa na familia yangu huko Mbagala na lilikuwa kipindi cha panya road, hakuna muhuni alisumbua
Hapa nitawapa mbinu kadhaa
1. Unapoombwa hela na wahuni usiwape.
Wahuni Huwa wanapenda kutikisa watu Kwa kuwapima msimamo wao.
Anaweza akakwambia
Oyaa Uncle nigei jero ya fegi
Mjibu huna au hutaki yaani isionekane ni haki kupewa kazi Bure
2. Shiriki mambo ya kijamii ya wahuni.
Wapewe michango kama ya mechi za ndondo, shughuli zao n.k
3. Kuwa mbabe kiasi
Itokee hata mhuni akizingua unampasua
4. Rudi usiku bila hofu
Ili wahuni au vibaka wasikuumize, we uwe na utamaduni wa kuingia na kutokea chimbo zao bila woga
5. Wajue wahuni baadhi
Ili wahuni wasikuumize we wajue wenzao kadhaa kwenye mtaa hata wakujue Kwa jina labda braza Salum
6. Usikae home Kinyonge au kike kike
Labda weekend upo unafua na kukaangiza, hapo wahuni watakulia timing na watakuchukulia vyako
7. Fanya mazoezi nao
Kama ni kupiga chuma, muulize muhuni chimbo zao za kupiga chuma ni wapi, nenda pale kiwashe hadi wakutambue kuwa huyu si mnyoge
8. Juana na wazazi au ndugu zao
9 . Wakosoe wanapokosea na watishie kuwa unaweza kuwaadhibu, hapa watakuheshimu
Miaka ya 90 huko moshi kulikua na wahuni , wanazamia Nairobi wanaiba ndinga kali kali tu wanazichimbia handaki , kitu ikitoka huko piru, ipo sokoni kwa I'd tofauti kabisa, wale wahuni walimiliki mpaka private jet zao wenyewe .Huku sisi tuna wasela nnya!.
muhuni anajua kutafuta pesa, pili anajui kuitumia anaweza akakaa miezi ama mwaka huoni ana misheni lkn anakula,anakunywa na anadrive maana wahuni wanapiga dili moja la maana anakula maisha sio watu wakutumia nguvu sanaa kutafuta pesa ni akili!, huwa wanakuwa radhi sana hata kuua ukigusa familia yake!.. sasa hapa bongo muhuni anaiba kwao badala yeye ndo akatafute alete aokoe jahazi!.
muhuni unafanya tukio unakamatwa na polisi wilaya hiyohiyo ama mkoa huohuo!, muhuni akifanya tukio mkimkosa ndo mmemkosa na mkimkamata kama sio nje ya nchi basi mbali.. sa mtu anafanya tukio zito huna hata pesa yakukimbilia unaenda kujificha kwenye magheto ya watu ambao nao wakija kupigwa mabanzi ya shingo wanakutoa...🤣
Kazingua mengi tu,ata hyo ya kurudi usiku sana eti ndio wajue wewe ni mbishi.Hapo kwenye kuwanyima hela umezingua ..
Sasa utajengaje urafiki na wahuni Kama huwapi hela ?
huo ndo uhuni sasa!Miaka ya 90 huko moshi kulikua na wahuni , wanazamia Nairobi wanaiba ndinga kali kali tu wanazichimbia handaki , kitu ikitoka huko piru, ipo sokoni kwa I'd tofauti kabisa, wale wahuni walimiliki mpaka private jet zao wenyewe .