bibliatimes
Member
- May 13, 2025
- 7
- 9
MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI KWA MUDA MREFU-1
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu.
Leo nataka nikupe mbinu kadhaa za kukusaidia kuomba vizuri na kwa muda mrefu.
Hakikisha Unafuatilia somo hili Hadi mwisho na Mungu atakuinua viwango vingine kimaombi.
Ni muhimu sana kwa mwana wa Mungu kuhakikisha unakua katika eneo la kuomba, Kuna viwango lazima uonekane unavuka na kuongezeka kimaombi kwa kadili unavyozidi kutembea na Mungu.
Ni lazima uchukie kuwa mtoto mchanga ambaye bado unahangaika inapokuja kwenye swala la kuomba Ijapokuwa uko na miaka ya kutosha ama miezi ya kutosha tangu ulipompokea Yesu. Unaomba dakika mbili, tano, kumi na Tano unachoka, huwezi kuomba na kukaa kwenye uwepo wa Mungu hata nusu saa au hata saa Moja ukiongea na naye.Chukia hali hii na ufanye maamuzi ya kuishinda.
Kuna faida nyingi sana za kukaa kwenye maombi kwa muda mrefu, ambazo pia nitakufundisha baada ya kumaliza kukupa mbinu za kuomba.
Ninajua Kuna mtu unatamani kuomba muda mrefu lakini unashindwa unaishia kuomba dakika Tano au kumi, lakini ndani mwako unajisikia kabisa kuwa hapana; natakiwa kufanya zaidi ya hapo, na unaelewa ndani ya moyo wako kuwa kuomba hivi dakika Tano, kumi, kumi na Tano haziwezi kunivusha hapa nilipo. Na unasikia kiu kubwa ya kutamani kuomba zaidi.
Basi zifuatazo ni mbinu za kukusaidia kutimiza kiu yako ya kuomba kwa muda mrefu;
1: Andaa mpangilio maalumu wa maombi yako.
Watu wengi wanafikiri kupangilia maombi sio kuwa kiroho, hapana mambo ya rohoni pia huwa na utaratibu fulani wa kukusaidia kupeleka hoja zako mbele za Mungu.
Isaya 41:21 "Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo"
Ni hatari sana mfalme anapokaa kukusikiliza halafu anakwambia haya leta hoja zako, halafu unaenda kiholela hata hujajiandaa jinsi ya kupangilia hoja na uanzie wapi na kuishia wapi.
Mara nyingi huwa naona watu wanaingia kuomba huku hawajaandaa maombi Yao na wanasema Roho Mtakatifu ataniongoza.
Kuingia kwenye maombi bila kuandaa hoja zako na ukisema Roho atakuongoza huo unaitwa uvivu wa kujiandaa kabla ya kuomba na unamtumia Roho Mtakatifu kama mbadala wa uvivu wako.
Mbona unapopeleka report ya kazi kwa boss wako, au unapoenda kwenye usahili, au unapeleka uwasilishwaji (presentation) mahali haulali tu bila kuandaa chochote na kusema nikifika Roho Mtakatifu ataniongoza cha kuongea.
Huo ni uvivu na kutokujali mambo yako ya kiroho na mahusiano yako Mungu, na kumchukulia Mungu kama kitu Cha ziada ambaye hahitaji maandalizi yoyote ya kuongea naye, ni kukukurupuka tu na kuanza kuongea chochote kinachokuja kinywani mwako.
Wewe tafakari hata sasa ni mara ngapi umejaribu kuomba hata dakika tano tu ukajikuta umeganda na kuishiwa na Cha kuomba, maneno yote yameisha? Unajua ni kwa sababu hukupangilia hoja zako, uanze na ipi, ifuate ipi, Kisha ifuate ipi, na mwisho nimalize na ipi.
Fikiria Mungu amekaa anakusikiliza maana umekuja kuongea naye, unafika kwake huna Cha kuongea umeishiwa. Ni kama ulikuwa hujui kabisa unakuja kuongea Nini mbele zake, hukuandaa hoja zako.
Wakati mwingine kuomba Kunahitaji akili timamu, Kaa chini andaa hata mfululizo wa maombi yako ya wiki nzima, weka hoja zako kadhaa ambazo utakuwa unaombea kila siku na uzipangilie vizuri Moja baada ya nyingine. Nakwambia utashangaa kujikuta umeomba masaa mawili bila hata kujua.
Unapoenda kuongea na Mungu, Fanya maandalizi binafsi ya hoja zako ili iwe rahisi kwako kuomba na ujue naanzaje na kumalizaje.
Itakusaidia sana kukaa muda mrefu kwenye maombi.
Mfano; Anza kwa kumshukuru Mungu dakika kadhaa, ingia kwenye kuomba Rehema na Toba na kujitakasa dakika kadhaa, mwalike Roho Mtakatifu, ingia kwenye Ombi la kwanza dakika kadhaa, Kisha ombi la pili dakika kadhaa n.k
Kuandaa maombi yako na mpangilio wa hoja zako pia ni akili ya rohoni na Wala sio kuwa mwili, kwani Mungu mwenyewe ameturuhusu kuleta hoja mbele zake na hakuna hoja inayopelekwa mahali kwa kukurupuka, lazima mtu akae chini azipange hoja vizuri Moja baada ya nyingine kabla ya kuzipeleka.
Au waweza kuwa na list ya maombi unayoombea kila siku, mfano: familia, ndoa, hali yako ya ukuaji wa kiroho, kuombea uchumi, watoto, kuombea huduma yako, n.k Katika kila hoja unaiombea kwa upana wake kabla ya kwenda hoja nyingine.
Mfano, katika kuombea ukuaji wako wa kiroho, utamuomba Mungu akupe neema ya kuomba zaidi, utaombea hali yako ya kusoma neno na kulielewa, utaombea hali ya utoaji wako, utaomba Mungu akubadilishe tabia zako n.k.
2: Jitengenezee madhabahu yako maalumu ya maombi.
Watu wengi hawana mahali maalumu pa kuombea, anaombea popote tu anapoona au anapobahatisha, ninajua hili si dhambi unaweza kuombea tu popote lakini haitakukuza kiroho maana huwezi kuwa serious kwenye maombi kwa kuombea popote bali utakuwa makini zaidi ukienda kuomba eneo ulilotenga kuwa unaongea na Mungu.
Mathayo 6:6 "Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako Cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za baba ..."
Kwenye hii kauli ya Bwana Yesu, mbali na maana nyingine yoyote lakini anaonyesha unapoomba lazima uwe na mahali maalumu unapojifungia rasmi kwa ajili ya kuomba, mahali panapokupa utulivu, mahali panapokupa faragha.
Yeye mwenyewe alipenda kwenda kuombea kwenye mlima wa mizeituni, je ni kweli hakuwa na mahali pengine pa kuomba? Ni kwamba alipachagua pale kuwa madhabahu yake ya maombi.
Mtu yeyote asiyekuwa na mahali maalumu anapojificha kuomba kila siku hawezi kukua kimaombi na hawezi kuomba kwa muda mrefu.
Lazima ujitengenezee madhabahu ya maombi, kama ni nyumbani kwako Tenga chumba maalumu utakapokuwa unafanyia maombi, kama ni chumbani kwako basi ijulikane, kama mazingira ya nyumbani kwako si mazuri basi tafuta sehemu nyingine labda kanisani, labda eneo Fulani la wazi (binafsi Kuna miaka ya nyuma ambapo sikuwa na mazingira mazuri ya maombi na Kuna uwanja Fulani wa wazi niliuchagua kuwa naombea, na ningeamka kila siku saa nane na kuzunguka ninaomba hapo Hadi saa kumi na mbili asubuhi kwa miaka ya kutosha nilifanya hivyo).
Lazima na wewe uchague eneo lako la maombi:
Moja ya faida za kuwa na eneo lako maalumu la maombi ni:
Moja: Mwili wako utazoea Hilo eneo, kila unapoingia hapo akili yako na mwili wako vinahama kimaombi, mwili wa mwanadamu una tabia hizo, ndio maana ukipanda tu kitandani akili haiwazi kingine zaidi ya kulala maana ndivyo ulivyoizoesha, ukiingia tu jikoni akili inawaza tu chakula maana ndivyo ulivyoizoesha.
Vivyo hivyo ukiingia tu kwenye eneo lako la maombi akili inahama kuanza kuomba maana tayari uneshaizoesha hivyo.
Mbili: Sehemu unapoombea kila siku huwa panatengeneza wingu fulani au uwepo fulani wa kimaombi kwenye ulimwengu wa roho, kumbuka kila siku unaomba hapo hivyo anga linakuwa tayari limefunguka kimaombi na kunakuwa na wepesi sana wa kuomba unapoingia tu eneo hilo.
Kumbuka kila ukiomba kila siku nguvu ya Mungu na uwepo wa Mungu unakaa kwenye hilo eneo tofauti na unapohangaika Leo umeombea hapa kesho pale, lazima upate ugumu sana wa kuomba.
Ndio maana watu wote waliotembea na Mungu nyakati za biblia kuanzia agano la kale hadi agano jipya walikuwa na mahali maalumu wanapoenda kuomba, wengine kwenye milima, wengine kwenye bustani Fulani, wengine hekaluni, wengine kwenye nyumba Fulani kama wanafunzi wa Yesu walivyopenda kuombea kwenye nyumba ya Mariam n.k
Kuwa na madhabahu yako binafsi mahali unapokutana na Mungu, hili ni jambo muhimu na la kiroho na itakusaidia kutengeneza mazingira rafiki ya uwepo wa Mungu na ya kiuzoefu katika kukuwezesha kuomba kwa muda mrefu na kuomba vizuri zaidi.
Nifuatilie kwenye sehemu ya pili nitaeleza mbinu ya tatu ya kukusaidia kuomba vizuri na kwa muda mrefu.
Mungu akubariki.