Mbinu za Kuwa Tajiri(Milionea) - Sehemu ya II(Part Two)

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Mtu asikudanganye kwamba ukienda kwa wachawi au waganga utapata dawa ya kuwa tajiri. Watu wameenda huko na kutapeliwa kwamba wakiwatoa kafara watoto au wazazi wao ndio watapewa dawa ya utajiri. Ukiwa tajiri kwa njia hiyo basi ujue jehanam inakusubiri kwa hamu ikutafune.

Wewe unayefanya biashara au unayepanga kuanzisha biashara, leo nakupa kanuni/mbinu za kukuwezesha kuwa milionea, ukizitendea kazi sawasawa. Kanuni/mbinu hizi zinatokana na Maandiko ya kwenye Biblia lakini ni kanuni au mbinu zinazotambulika na kukubaliwa na wasomi waliobobea kwenye masuala ya biashara.

Zifuatazo ni kanuni/mbinu 7 zinazoweza kukusaidia kuwa milionea:

1. Fanya Kazi kwa Bidii
Mithali 10:4 – “Mkono wa mtu mvivu huleta umaskini, bali mkono wa mwenye bidii hutajirisha.”
👉 Mtu mwenye bidii anajituma. Hangoji kusukumwa bali anachukua hatua mwenyewe kwa hiari. Katika ulimwengu wa kibiashara bidii pia inamaanisha: kufanya kazi kwa masaa mengi ili kujenga msingi wa biashara yako. Kwa mfano, Elon Musk – anafanya kazi kwa zaidi ya saa 80 kwa wiki, ili kuhakikisha biashara zake zinakuwa na ubunifu wa hali ya juu.

2. Uwe Mwaminifu na Mwadilifu
Mithali 11:1 – “Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Bwana; bali vipimo vya haki humpendeza.”
👉 Uaminifu kwa wateja na washirika wa biashara utakujengea sifa nzuri, na kukupatia wateja wengi zaidi. Epuka udanganyifu unapopima bidhaa kwa mizani. Epuka kuvutia wateja kwa maneno ya uongo au ahadi za uongo.

3. Uwe Mkarimu na Mtoaji
Mithali 11:25 – “Mtu mkarimu atastawi; naye anyweshaye wengine, atanyweshwa mwenyewe.”
👉 Utoaji kwa wengine huleta baraka na fursa zaidi za kupata utajiri. Mataifa mengi yaliyobarikiwa yana watu wanaojua siri ya ukarimu - wanajitoa sana kuwasaidia maskini na yatima.

4. Epuka Uvivu na Kupoteza Muda
Mithali 6:10-11 – “Kulala kidogo, kusinzia kidogo, kukunja mikono upate usingizi; basi umaskini wako utakuja kama mnyang’anyi, na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.”
👉 Usipende sana usingizi. Watu wenye mafanikio hulala masaa yale tu yanayoshauriwa kiafya. Usipoteze muda kwenye mijadala isiyo na tija kiuchumi, kiafya, kijamii na kiroho. Tumia muda wako vizuri kwakuwa muda ni mali(Time is Money).

5. Usihofu Kuanza Kidogo
Ayubu 8:7 – “Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, mwisho wako utakua sana.”
👉 Biashara nyingi kubwa zilianza kwa mtaji mdogo lakini kwa uvumilivu na juhudi, zikakua.

6. Mtangulize Mungu katika Biashara Yako
Mathayo 6:33 – “Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
👉 Ni muhimu sana tukimruhusu Mungu awe Mshauri wetu mkuu na Mlinzi wetu Mkuu. Kila siku kabla ya kuanza biashara yako jizoeze kuiombea. Jizoeze kuomba Mungu akulinde na kukuepusha na majanga yanayoweza kuipata biashara yako - kama vile kuibiwa, duka au jengo lako la biashara kuungua moto au kuporomoka au kupata ajali unapokuwa safarini.

7. Tangaza Biashara Yako
Mathayo 5:15-16 – “Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali huiweka juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu...”
👉 Kama unafanya biashara nzuri lakini watu hawaijui, itakuwa vigumu kupata wateja. Matangazo ni njia ya kuifanya biashara yako ing'ae kama taa, ijulikane na kufanikiwa.

Hizo ni baadhi tu ya kanuni au mbinu za kukuwezesha kuwa tajiri au milionea. Naamini umeona sasa kwanini shetani anawazuia watu kusoma Biblia. Biblia ina hazina kubwa zilizofichika. Mungu akubariki na aibariki biashara yako. Amen

Kama ulipitwa na Sehemu ya I ya Mbinu za Kuwa Tajiri, link hii hapa
 
pesa haitafutwi, pesa inawekewa mtego. Unautega unatulia zako, utajiri unakuja.
Amekueleza ni aina gani hiyo ya mtego? Kuna mitego mibaya. Ukitumia pesa yako kukodi pikipiki ili umvizie tajiri anayekwenda kuweka pesa benki, umnyang'anye pesa zake, huo mtego ni wa kishetani.

Mimi katika points hizo nimeeleza mtego mzuri: matangazo ni mtego mzuri. Unalipia matangazo, unapata wateja wengi na pesa nyingi zaidi.
 
**** uzi geodavie kasema biblia sio neno la Mungu, nenda katoe maoni yako huko. adheists na kobazis wanafurahia na kushangilia wakisema nabii huyo yuko sahihi
 
**** uzi geodavie kasema biblia sio neno la Mungu, nenda katoe maoni yako huko. adheists na kobazis wanafurahia na kushangilia wakisema nabii huyo yuko sahihi
Hao Atheists niliwapa maswali wakashindwa kujibu. Wanawaonea tu watu wasiojua Maandiko.

Kama Maandiko yanenavyo, akili zao zimepofushwa. Try to imagine: Biblia hawaiamini. Inakuwaje sasa wanaamini maneno ya mtu anayejiita Nabii - jina ambalo limetokana na hiyohiyo Biblia.
 
Sawa Mkuu,umemsahau ya kujisimamia mwenyewe kama Chungu,Hana kiongozi Wala mfalme!
 
Fungua PM yako nina ujumbe wako tafadhali.👐
 
Utajiri wa masharti ni kama ushamba Fulani Kuna watu wanapesa nyingi lakini hawajawahi kwenda kwa waganga wew na likidonda lako hakiponi unasema wewe unahela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…