Pre GE2025 Mbinu za wizi wa kura zinazotumiwa na CCM zabainika; ni hizi hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
baseless. mwaka 2020 sisi pia tulisimamia uchaguz.sio kwel hakuna aliyelazimishwa. sema nyie vijana hampigag kura. sisi tumekaa pale kituon ni wazee wanaletwa wengine hawez hata kutembea vizur ila anajikongoja anapiga vijana wako zao vijiwen wanachek ball.
 
Hii nondo imetulia.

Siwezi kupoteza muda kushiriki chafuzi. CCM acha iibe, iharibu, kisha wananchi watakapochoka wataamua cha kufanya huko mbeleni wao wenyewe. Lakini CCM kamwe haitoki madarakani kwa chafuzi
Wewe unafikiri wananchi "watachoka" lini , mkuu 'Missile'. Hivi hadi tulipo fikia sasa hivi kweli tunaweza kusema wananchi hawajachoka?

Sasa hivi kinacho kosekana ni njia za kuwapanga na kuwaongoza wananchi hao tu basi ili waifanye hiyo kazi ya kuwaondoa CCM.

Ngoja nieleze kidogo. Haya wanayo fanya CCM sasa hivi tukielekea kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa, wananchi wanajua kila kitu kinacho pangwa na CCM. Wananchi wanajuwa kwamba uchaguzi/uchafuzi huu ni maandalizi ya uchafuzi wa mwakani (uchaguzi mkuu). Hawa wanao pachikwa kwenye nafasi hizi za uongozi huko mitaani ndio wakala wakuu wa kuchafua uchaguzi mkuu kuiwezesha CCM kuendelea. Wananchi wanayajuwa haya, na baadhi yao, ndio hao, kama wewe mnao amua kususia uchafuzi huu wa mwanzo.
Kwa bahati mbaya sana, CCM haijali, tena ndiyo furaha yao kuu kwa wananchi kutojitokeza; kwa sababu hiyo tayari ni njia ya wao kuendelea.

Ina faida gani kujiandikisha na kwenda kupiga kura ikijulikana tayari kuwa CCM ni washindi kwa njia haramu?

Kama kuna faida, moja ni kuwaonyesha CCM kuwa watu hawawataki; pamoja na kura zao kuharibiwa, lakini ukweli huo utakuwa upo wazi mioyoni mwao, na hata machoni mwa watu (hata wakiuficha ukweli huo). Hivi 'guilty consciousness' haiwezi kupunguza, au hata kutia uoga wasifanye baadhi ya maovu yao?

Lakini, tukiachana na hiyo sababu moja hapo juu; baada ya wananchi wengi kujiandikisha na kupiga kura na kura zao kuharibiwa, na wanbanchi hao wakaona ukweli huo. Hivi hatua hii haiwezi kuwa njia nzuri ya kuwapanga na kuwaongoza wananchi kutoka kwa wingi zaidi na kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu; na kuhakikisha kwamba safari hii kura zao watakataa zisichezewe?
Ni njia ipi iliyo rahisi kumshawishi mwananchi kukataa uharibifu wa kura yake; badala ya kutojishughulisha kabisa na kwenda kupiga kura (kususa)!

Mkuu 'Missile of the Nation', ninakuomba ujaribu kuweka fikra zako hapa, ili sote tujaribu kupata njia inayo weza kusaidia kuwa ondoa hawa CCM. Kususia uchaguzi siyo njia sahihi hata kidogo.
 
Hii nchi imeoza sana kwenye masuala ya uchaguzi. Wizi uliofanyika mwaka 2020 umewakatisha tamaa wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura.
Uzuri ni kwamba hawa hawa wanaotumika kuiba baada ya uchaguzi tunaishi nao mitaani na hali ya maisha inapokuwa mbaya kwa sababu ya viongozi waliopata uongozi bila kuwa na sifa na wao wanaathirika. Yaani mtu unapewa kisu unaambiwa jikate mwenyewe na wewe unajikata. Ndiyo maana tunafananishwa na manyani.
 
Mbinu za wizi wa chaguzi zote unafanana mkuu.
Hili ninalielewa vizuri sana mkuu'tpaul', na nikushukuru sana kwa kufanya uchambuzi makini kama ulivyo uweka hapo juu.
Lakini naomba unisome vizuri maana yangu katika bandiko hilo nililo mjibu mkuu 'Erythro'. Sikuwa na maana kuwa kuna njia tofauti kati ya maovu wayafanyayo CCM. Pengine itakusaidia kidogo kunielewa ninacho lenga ukinisoma kwenye majibu niliyo yaweka kwenye bandiko linalo mjibu mkuu 'Missille' ambaye yeye , kama walivyo wengi, mipango yake ni kususia kujiandikisha na kupiga kura; kwa mategemeo tu kwamba siku moja CCM itawaonea huruma waTanzania. Hili kamwe halitatokea.
 
Nami ninakubaliana na wewe mia kwa mia,kwamba wananchi ndio wenye uwezo wa kuzuia CCM wasifanye uharibifu, na wakati mzuri wa kufanya hivyo ni huu wa uchaguzi wa viongozi.

Toka mwanzo kabisa, 2020, tuli washauri CHADEMA waanze maandalizi ya kuwapa elimu wananchi huko vitongojini/mitaani kwa lengo hili hili, lakini kwa bahati mbaya sana naona ushauri haukukubaliwa, na sasa tupo hapa; hali ikiwa mbaya zaidi hata kuliko ile ya 2020!
 
Mkuu,
Bandiko zuri, umejadili vizuri mbinu za hao wezi.

Swali, je kama nchi tunatokaje hapo tulipofikishwa na hicho kikundi cha wezi kinachoongoza nchi bila ridhaa ya wananchi?!!
Kwa maoni yangu, hii sasa hivi ndiyo ingekuwa ni "MADA KUU" nchi nzima. Na huko ndani ya vyama vya upinzani kwenyewe sasa hivi ingekuwa ni kupanga mikakati ya kuwawezesha wananchi kukataa ujinga unaofanywa na CCM.
 
Hiyo mbinu ya kuletewa matokeo ndio hutumika zaidi. Mnakuta tu mtendaji kabandika matokeo ambayo hata hamjui yametoka wapi
 
Kwa hiyo wewe ulishudia nini 2020 nkuu?
 
Hii nondo imetulia.

Siwezi kupoteza muda kushiriki chafuzi. CCM acha iibe, iharibu, kisha wananchi watakapochoka wataamua cha kufanya huko mbeleni wao wenyewe. Lakini CCM kamwe haitoki madarakani kwa chafuzi
Nyie msiopiga kura hamna uhalali wa kulalamikia uchafuzi ilihali hata hamshiriki
 
Well narrated. Tatizo sijui kwa nini CDM wanashindwa kusoma mchezo huo na kuwathibiti wahuni hao.
 
Kila chenye mwanzo hakikosi mwisho Muda utasema Tusubiri. Na Kila afanyaye siku zake duniani zinahesabika hakuna atakaye dumu
 
Safari hii patachimbika
Tumesubiri sana tuone palipochimbika lakini wapi. Maneno mengi vitendo zero, wakati wahuni wanafanya kweli na mnabaki kupiga kelele tu. Viongozi wa CDM wanatekwa badala na nyie kufanya kweli kuwathibiti wahuni mnabaki kupiga kelele kwenye majukwaa.

Siku CDM mkiamua utashangaa wananchi wengi watakaoungana na nyie. 2015 wananchi waliamua na wakawa tunawasubiri CDM mseme kitu ili shughuli ianze mkajifanya waungwana na white hair wenu.
 
Tatizo sijui kwa nini CDM wanashindwa kusoma mchezo huo na kuwathibiti wahuni hao.
Jibu lipo kwenye namba 5 mkuu.
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoa mada, polisi hutumika kifanikisha wizi kwa shuruti.
👇
 
Jibu lipo kwenye namba 5 mkuu.
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoa mada, polisi hutumika kifanikisha wizi.
👇
Wizi wa kura ni mchakato (process) kama alivyosema mtoa hoja.

CDM walitakiwa wapinge kwa nguvu zote utaratibu mbovu na wa kihuni na kanuni zake wakati wa kujiandikisha kwenye daftari. Wapiga kura wengi wana vitambulisho kwa nini mtu haombwi uthibitisho wowote (Kitambulisho cha kura, taifa, leseni, kadi ya benki etc) wa kuthibitisha kuwa anayeandikisha ndo mwenye jina halisi.

Pili kwa nini CDM hawakukomaa ili daftari la wapiga kura linalotumika uchaguzi mkuu, hilo ndo liboreshwe na litumike kwenye kupiga kura badala ya utaratibu wa hovyo na wa kihuni uliofanywa safari hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…