Hii nondo imetulia.
Siwezi kupoteza muda kushiriki chafuzi. CCM acha iibe, iharibu, kisha wananchi watakapochoka wataamua cha kufanya huko mbeleni wao wenyewe. Lakini CCM kamwe haitoki madarakani kwa chafuzi
Wewe unafikiri wananchi "watachoka" lini , mkuu 'Missile'. Hivi hadi tulipo fikia sasa hivi kweli tunaweza kusema wananchi hawajachoka?
Sasa hivi kinacho kosekana ni njia za kuwapanga na kuwaongoza wananchi hao tu basi ili waifanye hiyo kazi ya kuwaondoa CCM.
Ngoja nieleze kidogo. Haya wanayo fanya CCM sasa hivi tukielekea kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa, wananchi wanajua kila kitu kinacho pangwa na CCM. Wananchi wanajuwa kwamba uchaguzi/uchafuzi huu ni maandalizi ya uchafuzi wa mwakani (uchaguzi mkuu). Hawa wanao pachikwa kwenye nafasi hizi za uongozi huko mitaani ndio wakala wakuu wa kuchafua uchaguzi mkuu kuiwezesha CCM kuendelea. Wananchi wanayajuwa haya, na baadhi yao, ndio hao, kama wewe mnao amua kususia uchafuzi huu wa mwanzo.
Kwa bahati mbaya sana, CCM haijali, tena ndiyo furaha yao kuu kwa wananchi kutojitokeza; kwa sababu hiyo tayari ni njia ya wao kuendelea.
Ina faida gani kujiandikisha na kwenda kupiga kura ikijulikana tayari kuwa CCM ni washindi kwa njia haramu?
Kama kuna faida, moja ni kuwaonyesha CCM kuwa watu hawawataki; pamoja na kura zao kuharibiwa, lakini ukweli huo utakuwa upo wazi mioyoni mwao, na hata machoni mwa watu (hata wakiuficha ukweli huo). Hivi 'guilty consciousness' haiwezi kupunguza, au hata kutia uoga wasifanye baadhi ya maovu yao?
Lakini, tukiachana na hiyo sababu moja hapo juu; baada ya wananchi wengi kujiandikisha na kupiga kura na kura zao kuharibiwa, na wanbanchi hao wakaona ukweli huo. Hivi hatua hii haiwezi kuwa njia nzuri ya kuwapanga na kuwaongoza wananchi kutoka kwa wingi zaidi na kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu; na kuhakikisha kwamba safari hii kura zao watakataa zisichezewe?
Ni njia ipi iliyo rahisi kumshawishi mwananchi kukataa uharibifu wa kura yake; badala ya kutojishughulisha kabisa na kwenda kupiga kura (kususa)!
Mkuu 'Missile of the Nation', ninakuomba ujaribu kuweka fikra zako hapa, ili sote tujaribu kupata njia inayo weza kusaidia kuwa ondoa hawa CCM. Kususia uchaguzi siyo njia sahihi hata kidogo.