Fabian the Jr
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 756
- 751
Nikiwa kama wakala wa E-money (Miamala ya pesa) nimeshuhudia mambo mengi sana ambayo nafikiri kwa kuyasimulia naweza nikawasaidia watu wengi sana especially mawakala wa hizi Mpesa,Tigopesa, AirtelMoney nk kuepuka utapeli ambao hufanywa na watu wenye nia mbaya. Natambua kwa wakala anayefanya kazi kwa kutegemea kamisheni let say ya laki 3 kwa mwezi unapotapeliwa let say laki 7 inauma sana na inaweza kukurudisha nyuma kimaendeleo. Zifuataza ni mbinu ambazo hutumiwa na matapeli kwenye hizi miamala.
Mbinu 1: Wakala unapokea ujumbe wa kupokea pesa mfano, "...imethibitishwa umepokea kiasi cha Tsh xxx kutoka kwa xxxx salio lako ni xxx" Wakati unashangaa nani katuma hiyo pesa (Kutoa) mara unapokea simu mara nyingi hujitambulisha kwamba wanatokea Mpesa, Tigopesa etc watakuuliza kama kuna pesa umeipokea imetumwa kimakosa na mtu hivyo wanaomba uirudishe, mara nyingi huwa wanajitahidi kukuwekea pressure sana wa vitisho vya kuifungia laini yako ili usipate wazo la kuangalia salio, Ukifanya kosa ukawasikiliza ukaituma hiyo pesa IMEKULA KWAKO.
Mara nyingi njia hii hufanyika kwa ushirikiano na wafanyakazi wa mitandao husikaambao husaidia kujua kiasi cha salio ulilonalo kwenye simu yako. Na katika hili tigopesa wanafanya sana.
Solution: Hakikisha unamhudumia mtu unayemuona mbele yako, Kama mtu akikosea kutuma pesa mtandao husika baada ya kukupigia simu wataikata iyo pesa na kuirudisha kwa mhusika na sio kukwambia wewe wakala uirudishe. Na hakikisha messeji yoyote ya muamala unayopokea kwenye simu yake imetoka M-Pesa, TigoPesa nk na sio kwenye namba flani ya simu.
Mbinu 2: Mtu anakuja anakuja anakupa simu yake anakuomba umtolee pesa, unamuuliza shilingi ngapi anakwambia hana ukakika, anakuomba umuangalizie salio, ukiuliza salio inakuomba password, unamuomba akupe password anakuomba simu ili aweke password alafu anakaa nayo akisubiri meseji ya salio iingie then anakupa iyo msg ya salio.
Labda unaona msg "Imethibitishwa salio lako ni 590,000..." atakwambia umtolee labda lakin5 na Mara nyingi unapokuwa unafanya hayo huyo mtu anakuwa ana hali flani ya haraka sana na anakuwa anakuharakisha au ukute hiyo simu yake inaita mara kwa mara hivyo kukukatisha mara kwa mara kutoa pesa.
Mara anatokea mtu either ana bodaboda au gari nje, Basi huyu mteja wako anakuulizaa, Kaka /dada ushatoa? unamjibu "bado, kuna watu wanakupigia hapa wananikatisha katisha sana" atakwambia, "Samahani dada/kaka naomba wakati unaendelea kutoa nipe hiyo hela nimpe huyu jamaa hapa nje ananisubiri kuna mgonjwa hapo tunampeleka hospitali"
Kwakuwa unaona una simu yake ambayo umeona msg ina salio la kutosha na kweli umeona kuna mtu anamsubiri nje UKIMPA TU HIYO HELA UMELIWA, Anaondoka na simu atakuachia, ukiweka password aliyokupa itagoma, unakuta ka simu kwenyewe ni ka itel kapya ka 20,000.
Solution: Mbinu hii imewatapeli watu wengi sana pesa, hakikisha USIMPE MTEJA PESA KABLA HUJAPATA MSG YA KUCONFIRM KWENYE SIMU YAKO YA UWAKALA, NA PIA USIMPE MTU PESA KWA KUANGALIA MSG ALIYOIPATA YEYE KWENYE SIMU YAKE. Mteja anapokuja kwako kutoa hela akikuomba umtolee, akishakupa simu USIIMRUDISHIE MPAKA UMALIZE KUFANYA MUAMALA (Usimpe aweke password alafu akurudishie mwambie akutajie password na kama hataki mwambie atoe mwenyewe). Ukimpa simu aweke password ndo hutumia huo mwanya kuweka msg ya kuonyesha wana salio kwenye simu yao, Mpe mteja pesa pale tu unapopata confirmation kwenye simu yako.
Mbinu 3: Nipo arusha Nina ninamtumia jamaa yangu no za wakala aliyepo hapa ila jamaa yupo kigoma. Jamaa anatoa hela..msg inakuja kwa wakala....huyu wakala anadhani ni Mimi...na ninamtajia jina lililotuma....akishanipa noti tu......jamaa Wa kigoma analalamika kwamba amekosea no ya wakala....na wao wakiangalia wanaona ela IPO kigoma imetumwa kwa wakala Wa arusha.....wanairudisha.
Mbinu 4: Au anakuja MTU anabandika till no yake hapo kwako bila kujua Wateja kama 10 HV wote unawaambia hujaona msg....ohoooooo kitu imeenda pengine
Mbinu 5: Kuna ndugu yangu mmoja hivi ye aliibiwa kwa namna hii. Walikuja wateja wawili jioni karibia na kufunga biashara kuweka pesa kila mmoja kaja wa wakati wake waliweka kama laki tisa hivi alafu kaja mtu mwingine watatu akamuuliza kama anapesa ya kuweka jamaa akasema kaishiwa.
Mpaka kufikia mda huu jamaa jua anapesa cash kama milion na nusu ile laki tisa ya wajamaa wawili na ela zake zingine za kutwa mzima,huyu watatu yeye kaja kuhakikisha kama jamaa now hana pesa ya kutuma tena bali ana cash tupu. Alipofunga hesabu wakati anaenda kwake yupo njia za uchochoro akakutana na gari limepaki alipolifikia wakatoka watu wamejifunga usoni kininja wakamteka na kusepa nae mpaka walipoona panafaa wakampora pesa wakasepa jua wakati huo pesa walizo rushiwa washazitoa tayari.
Mdau Wa 1: Nyongeza usimruhusu mteja akupe hela uzihesabu then umrudishie kisha akazuga zuga akakurudishia tena umwekeee hapa hakikisha unahesabu tena pesa alizokupa.usimwamini mteja hata kidogo.mimi pia nina ofisi ya uwakala na nmb bahati mbaya hilo tukio limenitokea mwenyewe.nimeibiwa laki kwa mtindo huo.nikwamba utapomtumia salio palepale anahamisha na line anatupa.tuwe makini hizi biashara zenyewe hazina faida kivileee
Mdau Wa 2: Halafu njia nyingine jamaa anakupigia. Halafu anakuwa very smart, hana haraka. Anakupigia anakwambia yeye ni wakala wako mkuu. Kuna pesa wamekutumia hebu angalia salio. Kwanza anakwambia umtajie namba yako nyingine akupigie huko ili simu yenye line ya wakala iwe free. Ukishamtajia namba Zako anakupigia huko then anakwambia kuna salio limetumwa kwako na kukutaka ucheck salio. Ukichek unakuta salio ni lile lile lako. Then anakwambia bado halijaingia. Ndo anaanza kukupa process za kufuata ili salio jipya liingie. Hapo anakutajia namba kibao hata huwez gundua kwa haraka kuwa ni namba zake. Ukibugi tu unajikuta umehamisha salio lako lote kwake na inakuwa ishakula upande wako. Walishanipigia Mara mbili ila zote nilipangua. Mara ya kwanza nilishtukia mchezo hatua za mwisho nkakata simu. Second time wakapiga tena nkawatukana tu wakakata simu yao
Mbinu ziko nyingi ila hizi ndo hutumika zaidi na zingine wataongeza wadau.
Mdau wa 3: Kuna utapeli mpya umeingia mjini na huu niliushuhudia mimi mwenyewe kwa macho yangu hapo kinondoni. Nilienda kwa dada mmoja kutoa pesa, wakati niko pale nikisubiri nitumiwe hiyo pesa ili niitoe kuna gari aina ya harrier ilikuja ikapaki pembeni, akashuka jamaa mmoja mwenye muonekano nadhifu na heshima tu.
Yule bwana akasema alihitaji kuweka pesa laki 5, yule dada akasema sawa hakuna shida. Yule dada akampa yule jamaa simu ili aandike namba ya simu inayowekewa pesa. Yule jamaa akamwambia yule dada "Dada nakutajia naomba uiandike tu" Basi jamaa akataja zile namba akatoa na pesa laki tano akampa yule dada. Dada yule akatuma ile pesa, wakati yule dada anatuma jamaa akawa kama anaongea na simu kama kwa dakika mbili hivi, alipokata akamuuliza yule dada, "Dada umeshaweka?" Dada akamjibu kwamba tayari ameiweka,
Jamaa akaangalia simu yake akamwambia yule dada "Mbona mimi sijaiona kwenye simu yangu? Limekuja jina gani?" Dada yule akamwambia jina lililokuja. Jamaa akamwambia, "Aaaah dada umekosea kuandika hiyo namba, hilo sio jina langu na simu yangu hii hapa sijaipata iyo hela" Dada akaanza kuwapigia voda wairudishe wakamwambia iyo pesa tayari imeshatolewa.
Jamaa alikuwa very calm wala hakuonyesha hofu au kupanic, akamwambia yule dada, "Dada kama unanirushia nirushie niondoke, la sivyo nipe hela yangu niondoke" Yule dada akawa anakataa kurudisha pesa, jamaa akasema anaenda polisi maana yeye hana kosa, kwamba katoa pesa, kataja namba ya simu yake lakini haijaingia kwenye simu yake. Yule dada kusikia polisi akamrudiashia jamaa hela yake. Jamaa akawasha gari akaenda.
Kumbe issue inakuwa kwamba wanakuwa wamepanga kabisa, mmoja anakuwa mahali anasubiri hela iingia aitoe fasta, na ndo maana jamaa alikuwa anaongea nae kwenyw simu akishahakikisha hela imetolewa ndo anaanza kudai hela yake.
Ushauri,
Mteja mpe simu aandike mwenyewe namba ya simu inayowekewa hela au mpe karatasi aandike. Tofauti na hapo usikubali kutajiwa namba ya simu.
Mdau wa 4:
Mke wangu kaibiwa juzi kati. Walikwenda jamaa wawili wakasema wanahtaji kuweka laki tisa mpesa. Wife akawaambia sawa, wakampa hela laki 9 ahesabu. Alipomaliza kuhesabu yule jamaa aliyempa hela akamuuliza makato ya kutoa laki tisa kwa huyo atakayemtumia ni kiasi gani? Wife akamwambia ni Elfu 8, jamaa akaguna na kuanza kulalamika kwamba hiyo ada ni kubwa sana. Akamwambia wife amrudishie hela yake atafute njia nyingine ya kumtumia huyo mtu. Wife akamrudishia, jamaa akaiweka mfukoni lile bunda la hela. Wakati wanataka kuondoka yule mwenzake waliyekuja nae akaanza kama kumsema mwenzake kwamba atume tu kwasababu hakuna njia nyingine rahisi. Wakabishana kama dakika mbili hivi jamaa akaonekana kuelewa, basi akamwambia wife, basi hebu itume tu, akaingia mfukoni akatoa bunda la pesa akampa wife. Wife kwa sababu ashazihesabu akaweka kwenye droo akatuma laki 9 jamaa wakaondoka.
Muda kidogo wife kuangalia vizuri lile bunda la pesa, alikuta bunda zima kasoro noti mbili za juu ni karatasi zilizotolewa photocopy ya picha ya pesa. Bunda zima lilikuwa feki za karatasi, kasoro elfu ishirini zilizokuwa juu.
Kumbe wale mabwana walikuwa na bunda mbili mbili, moja OG moja feki hivyo baada ya kuhesabu ile OG waliirudisha wakampa FEKI.
Ushauri.
Hakikisha pesa yoyote unayomuwekea mteja umeihesabu vizuri na kuhakikisha kuwa ni pesa halisi. Maana ile bunda angeifungua tu angejua maana zilikuwa karatasi kabisa.

Last edited: