Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilitumia sim banking kuweka hela kwny akaunti yangu ya tigopesa ilikuwa usiku kama saa 4 hela nilikuwa nataka nilipie vifaa asbh.Chief hebu tushirikishe tafadhali ilikuwaje hiyo?
Mkuu Naomba Uzi wako uwe una uupdate Mara kwa Mara ili tuzidi kuzijua hizo mbinu wanazotumia hawa matapeliNikiwa kama wakala wa E-money (Miamala ya pesa) nimeshuhudia mambo mengi sana ambayo nafikiri kwa kuyasimulia naweza nikawasaidia watu wengi sana especially mawakala wa hizi Mpesa,Tigopesa, AirtelMoney nk kuepuka utapeli ambao hufanywa na watu wenye nia mbaya. Natambua kwa wakala anayefanya kazi kwa kutegemea kamisheni let say ya laki 3 kwa mwezi unapotapeliwa let say laki 7 inauma sana na inaweza kukurudisha nyuma kimaendeleo. Zifuataza ni mbinu ambazo hutumiwa na matapeli kwenye hizi miamala.
Mbinu 1: Wakala unapokea ujumbe wa kupokea pesa mfano, "...imethibitishwa umepokea kiasi cha Tsh xxx kutoka kwa xxxx salio lako ni xxx" Wakati unashangaa nani katuma hiyo pesa (Kutoa) mara unapokea simu mara nyingi hujitambulisha kwamba wanatokea Mpesa, Tigopesa etc watakuuliza kama kuna pesa umeipokea imetumwa kimakosa na mtu hivyo wanaomba uirudishe, mara nyingi huwa wanajitahidi kukuwekea pressure sana wa vitisho vya kuifungia laini yako ili usipate wazo la kuangalia salio, Ukifanya kosa ukawasikiliza ukaituma hiyo pesa IMEKULA KWAKO.
Mara nyingi njia hii hufanyika kwa ushirikiano na wafanyakazi wa mitandao husikaambao husaidia kujua kiasi cha salio ulilonalo kwenye simu yako. Na katika hili tigopesa wanafanya sana.
Solution: Hakikisha unamhudumia mtu unayemuona mbele yako, Kama mtu akikosea kutuma pesa mtandao husika baada ya kukupigia simu wataikata iyo pesa na kuirudisha kwa mhusika na sio kukwambia wewe wakala uirudishe. Na hakikisha messeji yoyote ya muamala unayopokea kwenye simu yake imetoka M-Pesa, TigoPesa nk na sio kwenye namba flani ya simu.
Mbinu 2: Mtu anakuja anakuja anakupa simu yake anakuomba umtolee pesa, unamuuliza shilingi ngapi anakwambia hana ukakika, anakuomba umuangalizie salio, ukiuliza salio inakuomba password, unamuomba akupe password anakuomba simu ili aweke password alafu anakaa nayo akisubiri meseji ya salio iingie then anakupa iyo msg ya salio. Labda unaona msg "Imethibitishwa salio lako ni 590,000..." atakwambia umtolee labda lakin5 na Mara nyingi unapokuwa unafanya hayo huyo mtu anakuwa ana hali flani ya haraka sana na anakuwa anakuharakisha au ukute hiyo simu yake inaita mara kwa mara hivyo kukukatisha mara kwa mara kutoa pesa. Mara anatokea mtu either ana bodaboda au gari nje, Basi huyu mteja wako anakuulizaa, Kaka /dada ushatoa? unamjibu "bado, kuna watu wanakupigia hapa wananikatisha katisha sana" atakwambia, "Samahani dada/kaka naomba wakati unaendelea kutoa nipe hiyo hela nimpe huyu jamaa hapa nje ananisubiri kuna mgonjwa hapo tunampeleka hospitali" Kwakuwa unaona una simu yake ambayo umeona msg ina salio la kutosha na kweli umeona kuna mtu anamsubiri nje UKIMPA TU HIYO HELA UMELIWA, Anaondoka na simu atakuachia, ukiweka password aliyokupa itagoma, unakuta ka simu kwenyewe ni ka itel kapya ka 20,000.
Solution: Mbinu hii imewatapeli watu wengi sana pesa, hakikisha USIMPE MTEJA PESA KABLA HUJAPATA MSG YA KUCONFIRM KWENYE SIMU YAKO YA UWAKALA, NA PIA USIMPE MTU PESA KWA KUANGALIA MSG ALIYOIPATA YEYE KWENYE SIMU YAKE. Mteja anapokuja kwako kutoa hela akikuomba umtolee, akishakupa simu USIIMRUDISHIE MPAKA UMALIZE KUFANYA MUAMALA (Usimpe aweke password alafu akurudishie mwambie akutajie password na kama hataki mwambie atoe mwenyewe). Ukimpa simu aweke password ndo hutumia huo mwanya kuweka msg ya kuonyesha wana salio kwenye simu yao, Mpe mteja pesa pale tu unapopata confirmation kwenye simu yako.
Mbinu ziko nyingi ila hizi ndo hutumika zaidi na zingine wataongeza wadau.
Sawa mkuu nitafanya ivoMkuu Naomba Uzi wako uwe una uupdate Mara kwa Mara ili tuzidi kuzijua hizo mbinu wanazotumia hawa matapeli
Huu sasa ni ujambaziKuna ndugu yangu mmoja hivi ye aliibiwa kwa namna hii. Walikuja wateja wawili jioni karibia na kufunga biashara kuweka pesa kila mmoja kaja wa wakati wake waliweka kama laki tisa hivi alafu kaja mtu mwingine watatu akamuuliza kama anapesa ya kuweka jamaa akasema kaishiwa.
Mpaka kufikia mda huu jamaa jua anapesa cash kama milion na nusu ile laki tisa ya wajamaa wawili na ela zake zingine za kutwa mzima,huyu watatu yeye kaja kuhakikisha kama jamaa now hana pesa ya kutuma tena bali ana cash tupu. Alipofunga hesabu wakati anaenda kwake yupo njia za uchochoro akakutana na gari limepaki alipolifikia wakatoka watu wamejifunga usoni kininja wakamteka na kusepa nae mpaka walipoona panafaa wakampora pesa wakasepa jua wakati huo pesa walizo rushiwa washazitoa tayari.
Mkuu mbinu zinabadilika kulingana na mahali walipo matapeliMkuu Naomba Uzi wako uwe una uupdate Mara kwa Mara ili tuzidi kuzijua hizo mbinu wanazotumia hawa matapeli
Sawa lakini ukijua walau mbinu 10 wanazozitumia hautakuwa sawa na yule asiyejua kabisa hata mbinu mojaMkuu mbinu zinabadilika kulingana na mahali walipo matapeli
Mkuu kuna wakati anaweza akaja mtu akakuambia Nina ndugu yangu anataka kunitumia hela sasa mi niko mtandao mwingne naomba atume kwenye Namba ya wakala moja kwa moja na akisha toa ukimpa hela anampiga mhusika apige simu Huduma kwa Wateja aseme amekosea namba nawe kwa unaweza ukapigiwa na mtandao husika kuhusiana na huo mwamalaSawa lakini ukijua walau mbinu 10 wanazozitumia hautakuwa sawa na yule asiyejua kabisa hata mbinu moja
Unacho paswa kujua ni kuwaSawa lakini ukijua walau mbinu 10 wanazozitumia hautakuwa sawa na yule asiyejua kabisa hata mbinu moja
Nimekusoma vizuri mkuu AhsanteUnacho paswa kujua ni kuwa
Simu yako ya uwakala haishikwi na mtu zaidi yako na msaidizi wako
Usiruhusu mteja kishika simu yako ya uwakala
Mteja akija na haraka achana nae akapate Huduma mbele ya safari
Mteja akija anajifanya hajui chukua nafasi ya kumfundisha bila kushika simu yake we mpe maelekezo kulingana na Huduma anayo taka kuifanya
Hakikisa masaidizi wako anajua mashart ya ofisi kuhusu kazi ya uwakala
Sawa mkuu utekelezaji mwemaNimekusoma vizuri mkuu Ahsante
Kaka asante sana kwa somo aisee, nice pointsUnacho paswa kujua ni kuwa
Simu yako ya uwakala haishikwi na mtu zaidi yako na msaidizi wako
Usiruhusu mteja kishika simu yako ya uwakala
Mteja akija na haraka achana nae akapate Huduma mbele ya safari
Mteja akija anajifanya hajui chukua nafasi ya kumfundisha bila kushika simu yake we mpe maelekezo kulingana na Huduma anayo taka kuifanya
Hakikisa masaidizi wako anajua mashart ya ofisi kuhusu kazi ya uwakala
Asante mkuu tuko pamoja maana hii biashara inachangamoto nyingi sanaKaka asante sana kwa somo aisee, nice points
Mawakala wwngi hupuuzia hiyoWakala ni mzembe kwani anatakiwa ukishatoa pesa na ujumbe kumfikia aombe simu yako ili aone ujumbe uliotumiwa wewe pia mimi binafsi nilikwenda kutoa pesa kwa wakala akafanya hivyo, hizi bishara mtu anatakiwa kuwa makini kila hatua.
Mkuu kuna wakati anaweza akaja mtu akakuambia Nina ndugu yangu anataka kunitumia hela sasa mi niko mtandao mwingne naomba atume kwenye Namba ya wakala moja kwa moja na akisha toa ukimpa hela anampiga mhusika apige simu Huduma kwa Wateja aseme amekosea namba nawe kwa unaweza ukapigiwa na mtandao husika kuhusiana na huo mwamala
Mkuu hili la kuingiliana elimu haija pita vya kutoshaMitandao yote inaingiliana.
Hao ndo kuwapiga wapate akili.Mkuu hili la kuingiliana elimu haija pita vya kutosha
Hili hata wakala ukimwambia naweka mtandao A natuma matandao B unakuta nae anakushangaa kuwa imeanza lini?