Nikiwa kama wakala wa E-money (Miamala ya pesa) nimeshuhudia mambo mengi sana ambayo nafikiri kwa kuyasimulia naweza nikawasaidia watu wengi sana especially mawakala wa hizi Mpesa,Tigopesa, AirtelMoney nk kuepuka utapeli ambao hufanywa na watu wenye nia mbaya. Natambua kwa wakala anayefanya kazi kwa kutegemea kamisheni let say ya laki 3 kwa mwezi unapotapeliwa let say laki 7 inauma sana na inaweza kukurudisha nyuma kimaendeleo. Zifuataza ni mbinu ambazo hutumiwa na matapeli kwenye hizi miamala.
Mbinu 1: Wakala unapokea ujumbe wa kupokea pesa mfano, "...imethibitishwa umepokea kiasi cha Tsh xxx kutoka kwa xxxx salio lako ni xxx" Wakati unashangaa nani katuma hiyo pesa (Kutoa) mara unapokea simu mara nyingi hujitambulisha kwamba wanatokea Mpesa, Tigopesa etc watakuuliza kama kuna pesa umeipokea imetumwa kimakosa na mtu hivyo wanaomba uirudishe, mara nyingi huwa wanajitahidi kukuwekea pressure sana wa vitisho vya kuifungia laini yako ili usipate wazo la kuangalia salio, Ukifanya kosa ukawasikiliza ukaituma hiyo pesa IMEKULA KWAKO.
Mara nyingi njia hii hufanyika kwa ushirikiano na wafanyakazi wa mitandao husikaambao husaidia kujua kiasi cha salio ulilonalo kwenye simu yako. Na katika hili tigopesa wanafanya sana.
Solution: Hakikisha unamhudumia mtu unayemuona mbele yako, Kama mtu akikosea kutuma pesa mtandao husika baada ya kukupigia simu wataikata iyo pesa na kuirudisha kwa mhusika na sio kukwambia wewe wakala uirudishe. Na hakikisha messeji yoyote ya muamala unayopokea kwenye simu yake imetoka M-Pesa, TigoPesa nk na sio kwenye namba flani ya simu.
Mbinu 2: Mtu anakuja anakuja anakupa simu yake anakuomba umtolee pesa, unamuuliza shilingi ngapi anakwambia hana ukakika, anakuomba umuangalizie salio, ukiuliza salio inakuomba password, unamuomba akupe password anakuomba simu ili aweke password alafu anakaa nayo akisubiri meseji ya salio iingie then anakupa iyo msg ya salio. Labda unaona msg "Imethibitishwa salio lako ni 590,000..." atakwambia umtolee labda lakin5 na Mara nyingi unapokuwa unafanya hayo huyo mtu anakuwa ana hali flani ya haraka sana na anakuwa anakuharakisha au ukute hiyo simu yake inaita mara kwa mara hivyo kukukatisha mara kwa mara kutoa pesa. Mara anatokea mtu either ana bodaboda au gari nje, Basi huyu mteja wako anakuulizaa, Kaka /dada ushatoa? unamjibu "bado, kuna watu wanakupigia hapa wananikatisha katisha sana" atakwambia, "Samahani dada/kaka naomba wakati unaendelea kutoa nipe hiyo hela nimpe huyu jamaa hapa nje ananisubiri kuna mgonjwa hapo tunampeleka hospitali" Kwakuwa unaona una simu yake ambayo umeona msg ina salio la kutosha na kweli umeona kuna mtu anamsubiri nje UKIMPA TU HIYO HELA UMELIWA, Anaondoka na simu atakuachia, ukiweka password aliyokupa itagoma, unakuta ka simu kwenyewe ni ka itel kapya ka 20,000.
Solution: Mbinu hii imewatapeli watu wengi sana pesa, hakikisha USIMPE MTEJA PESA KABLA HUJAPATA MSG YA KUCONFIRM KWENYE SIMU YAKO YA UWAKALA, NA PIA USIMPE MTU PESA KWA KUANGALIA MSG ALIYOIPATA YEYE KWENYE SIMU YAKE. Mteja anapokuja kwako kutoa hela akikuomba umtolee, akishakupa simu USIIMRUDISHIE MPAKA UMALIZE KUFANYA MUAMALA (Usimpe aweke password alafu akurudishie mwambie akutajie password na kama hataki mwambie atoe mwenyewe). Ukimpa simu aweke password ndo hutumia huo mwanya kuweka msg ya kuonyesha wana salio kwenye simu yao, Mpe mteja pesa pale tu unapopata confirmation kwenye simu yako.
Mbinu ziko nyingi ila hizi ndo hutumika zaidi na zingine wataongeza wadau.