Mbinu zinazotumiwa na Matapeli kwenye M-Pesa,Tigo Pesa Airtel M n.k

Chief hebu tushirikishe tafadhali ilikuwaje hiyo?
Nilitumia sim banking kuweka hela kwny akaunti yangu ya tigopesa ilikuwa usiku kama saa 4 hela nilikuwa nataka nilipie vifaa asbh.


Hela ikaingia msg haikuja lkn nilivyocheki salio kwny tigopesa ilionyesha ipo...asubuhi nmeamka niende kwa wakala nitoe hamna hata senti kupiga simu tigo naambiwa sijui nmetuma hela kwa Mtu anaitwa bakari maulid na namba haipatikani.

Kwenda polisi nikaandikiwa maelezo halaf file liende kwa mtu anayedili na mambo ya mtandao sijui nn.

Nikaona isiwe tabu nimwachie Mungu tu.
 
Mkuu Naomba Uzi wako uwe una uupdate Mara kwa Mara ili tuzidi kuzijua hizo mbinu wanazotumia hawa matapeli
 
Huu sasa ni ujambazi
 
Sawa lakini ukijua walau mbinu 10 wanazozitumia hautakuwa sawa na yule asiyejua kabisa hata mbinu moja
Mkuu kuna wakati anaweza akaja mtu akakuambia Nina ndugu yangu anataka kunitumia hela sasa mi niko mtandao mwingne naomba atume kwenye Namba ya wakala moja kwa moja na akisha toa ukimpa hela anampiga mhusika apige simu Huduma kwa Wateja aseme amekosea namba nawe kwa unaweza ukapigiwa na mtandao husika kuhusiana na huo mwamala
 
Sawa lakini ukijua walau mbinu 10 wanazozitumia hautakuwa sawa na yule asiyejua kabisa hata mbinu moja
Unacho paswa kujua ni kuwa

Simu yako ya uwakala haishikwi na mtu zaidi yako na msaidizi wako

Usiruhusu mteja kishika simu yako ya uwakala

Mteja akija na haraka achana nae akapate Huduma mbele ya safari

Mteja akija anajifanya hajui chukua nafasi ya kumfundisha bila kushika simu yake we mpe maelekezo kulingana na Huduma anayo taka kuifanya

Hakikisa masaidizi wako anajua mashart ya ofisi kuhusu kazi ya uwakala
 
Nimekusoma vizuri mkuu Ahsante
 
Kaka asante sana kwa somo aisee, nice points
 
Wakala ni mzembe kwani anatakiwa ukishatoa pesa na ujumbe kumfikia aombe simu yako ili aone ujumbe uliotumiwa wewe pia mimi binafsi nilikwenda kutoa pesa kwa wakala akafanya hivyo, hizi bishara mtu anatakiwa kuwa makini kila hatua.
Mawakala wwngi hupuuzia hiyo
 

Mitandao yote inaingiliana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…