Mbinu zinazotumiwa na Matapeli kwenye M-Pesa,Tigo Pesa Airtel M n.k

Mkuu hili la kuingiliana elimu haija pita vya kutosha

Hili hata wakala ukimwambia naweka mtandao A natuma matandao B unakuta nae anakushangaa kuwa imeanza lini?
Hao ndo kuwapiga wapate akili.
Ukipiga hata laki nne halafu kamishen inakuja 80.... Ndo akili itafungua....(utani Mkuu)
 
nyongeza usimruhusu mteja akupe hela uzihesabu then umrudishie kisha akazuga zuga akakurudishia tena umwekeee hapa hakikisha unahesabu tena pesa alizokupa.usimwamini mteja hata kidogo.mimi pia nina ofisi ya uwakala na nmb bahati mbaya hilo tukio limenitokea mwenyewe.nimeibiwa laki kwa mtindo huo.nikwamba utapomtumia salio palepale anahamisha na line anatupa.tuwe makini hizi biashara zenyewe hazina faida kivileee
 
Hao ndo kuwapiga wapate akili.
Ukipiga hata laki nne halafu kamishen inakuja 80.... Ndo akili itafungua....(utani Mkuu)
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] ujue walio pewa jukumu la kuwaelimisha mawakala wanakaa ofisini

Ila wapige hela wanajifanya kuitisha semina kwa mawakala lengo sio kufundisha ila nikupiga hela za kampuni


Elimu ya mara kwa mara kwa mawakala ni mhimu kuliko hata wahusika wanavyo lichukulia
 
Hii pia imemtokea Dada yangu last week. Sema ni hela mbuzi. Siku ya kwanza wamechukua thirty, na ndo ulikuwa hiyo hiyo kwa tigopesa yake. Kesho yake wakampiga tena 15 baada ya kuweka hiyo hiyo 15. Halafu text ya tigopesa ikaingia umetuma pesa kwenda namba XXX. Kuwapigia tigo wakajibu eti hii kitu haiwezekani labda we mwenyewe umetuma. Siku ya tatu ikaja tena text kuwa muamala haujafanikiwa. Kumbe jamaa alikuwa kwenye system anataka kujitumia tena pesa. Kweli Tigo ndo wanaongoza kwa wizi Huu. Wanafanyakazi wao wengi hawapo loyal!
 
Hawa tigo wana baadhi ya mambo wanashindwa kuyafanyia marekebisho kwa Wateja hasa inapo tokea umekosea hela bahati mbaya
 
Halafu njia nyingine jamaa anakupigia. Halafu anakuwa very smart, hana haraka. Anakupigia anakwambia yeye ni wakala wako mkuu. Kuna pesa wamekutumia hebu angalia salio. Kwanza anakwambia umtajie namba yako nyingine akupigie huko ili simu yenye line ya wakala iwe free. Ukishamtajia namba Zako anakupigia huko then anakwambia kuna salio limetumwa kwako na kukutaka ucheck salio. Ukichek unakuta salio ni lile lile lako. Then anakwambia bado halijaingia. Ndo anaanza kukupa process za kufuata ili salio jipya liingie. Hapo anakutajia namba kibao hata huwez gundua kwa haraka kuwa ni namba zake. Ukibugi tu unajikuta umehamisha salio lako lote kwake na inakuwa ishakula upande wako. Walishanipigia Mara mbili ila zote nilipangua. Mara ya kwanza nilishtukia mchezo hatua za mwisho nkakata simu. Second time wakapiga tena nkawatukana tu wakakata simu yao
 
Duuuh mzee hongera unaonekana uko makini kwelikweli aisee
 
baba angu naye kaibiwa hvyo kama ww laki 2 kwenye voda....alitumiwa hela kwenda kutoa akaambiwa hela ulimtumia mtu flan flan siku flan na mdaa..kupiga simu voda ndo akaelekezwa hvyo akasema ye hajafanya transaction yoyote tokea apate hyo pesa
Wakamwambia aripoti police

aliona ata akienda police haisaidi chochote utapewa tu rb ukae nayo tu bure..mwisho wa siku alikumbuka alimpa wale wanaosajili line simu yake. Tukajua ndo hao hao wamemwibia

So na ww pesa yako haiwezi potea hiv hiv kama hujafanya muamala huenda simu yako alishika mtu hawa matapel wakipata tu mwanya wa kushika simu yako umeliwa
 
Hawa watu wapo smart sana usipokua makini unaliwa huyo wako wanafanana na hawa hawa wanaopiga umeshinda kiasi flan naona wameiboresha kihivyo baada ya kusanukiwa
 
Mimi tokea siku hiyo situmii tena simbanking na hela nikiweka kwny simu namtumia mtu hapohapo haikai hata dakika 2
 
Njia nyingine ni hii inayotumiwa sana na mawakala ambao sio waaminifu hasa kwa wateja wakiume:-

Unaenda kwa wakala kuweka pesa kwenye acount ya simu yako na wakala anaikariri namba yako ya simu kisha anampatia tapeli wa kike ambae anakutumia pesa kiasi flani na baada ya kutuma tu anakupigia simu kuwa katuma pesa kimakosa hivyo anaomba kwa unyenyekevu sana umrudishie! Kwa udhaifu wa wanaume wengi utarudisha pesa huku ukiwa tayari umeshaanza matamanio na same tyme anapiga simu mtandao husika ili kuiblock ile pesa ambayo alikutumia na hewani humpati tena!
 
Hivi kwa mfano ninarundika pesa zangu Kwene M-Pawa yani M-PESA inakuwa zero balance muda wote wanaweza niiibia hao watumishi wa voda wasio waaminifu????
 
Mmoja aliniambia et anaomba simu yangu anisajiri na kifurushi cha chuo, nikampa simu lakn baada ya hapo lain yangu ikafungiwa, nikaja kugundua alitaka kufanya muhamara kwa kutumia miaka iliyoko kwenye kitambulisho changu kama password.
 
Mmoja aliniambia et anaomba simu yangu anisajiri na kifurushi cha chuo, nikampa simu lakn baada ya hapo lain yangu ikafungiwa, nikaja kugundua alitaka kufanya muhamara kwa kutumia miaka iliyoko kwenye kitambulisho changu kama password.
Hahahaa aisee ndo hvyo usikubali kuwapa sim wana mbinu zao uyo anaonekana hakua mzoefu
Mana ata huyo mzee wangu aliambiwa hvyo hvyo wamuungie vifurushi vya chuo
 
Utapeli nilioupata jana,Walinipigia simu wakisema wametoka kitengo cha Bonus cha voda,nimeshinda Laki mbili na simu ya Techno,wakataka kujua mara ya mwisho niliweka shs ngap mpesa? Nikawaambia hivi naongea na nyie nna balance la mia tano,rusheni hiyo laki mbili basi nije voda shop kuchukua techno,mbona walikata simu.
 

[emoji23][emoji23]uliwaweza kweli matapeli wakubwaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…