Mbinu zipi wamezitumia Wakinga kuwa wafalme Kariakoo?

Vigoli vya wakinga vinawapumbaza sana watu. Kukaa kote kkoo. Mkisema wakinga wamejaa mnatushangaza sana. Sema wanavigori. Wamepangana kumi kwenye mstari mmoja wa fremu. Na ni watu wenye sifa,, Wakinga na wanyakyusa wanasifa ila hawana ujaaji wala utajiri mnaouongelea.
Watu huongelea as if kuna mkinga au mnyakyusa kawahi nunua ghorofa la mchaga kkoo.. waknga wapo kwenye vigori. Tofautisha vigori na maduka ya jumla. Unawakuta wakinga mchikichi, congo, unasema wamejaa kkoo kweli? Tena kwenye vigori. Anakwambia nalipa milioni tano, nina store tano.. sasa zile fremu za wachaga ndani mule mnadhani ni bei gani? Wabena, Wakinga, wanyakyusa. Wapo kwenye vigori. Wanachukua mzigo kwa maboss wenye maduka, tshirt, jeans, sijui magauni . Na hata wanaoagiza hawawezi agiza kama wenye maduka yao. Unaona mtu anaagiza balo kila week anashusha balo 9 wakati wenzako wanaleta container tisa za nguo na mavitenge.😂😂😂.
Wakinga wanyakyusa, wabena. Wanavigori bado vya kiremba milioni 30.
 

Aisee sio kwa huu mkeka. Umetisha Boss
 

Tuwape na link kabisa The 20 richest people on the Dar es Salaam Stock Exchange
 
Werevu wameshaacha na biashara za kariakoo na walichofanya wameacha Majengo mengi ambayo ni fremu za biashara, "hyper stages" hizo hapo kariakoo hao magiant hawaoni kama wanapata kitu, japo siye kajambanani tu nawaona waliokodi ni matajiri kweli.
 
 
Jamaa uko deep sana kuna majina mengi nawafahamu vizuri ni mulemule haujatia chumvi

Bila kuwasahau akina Deo Marandu wa Emirate Aluminium Profile
 
Mkuu habari,vipi nikiwa na mtaji wa milion 80 naweza kuingia hapo kariakoo nikafungua duka?
 
Unafungua mkuu,inategemea utajikita sekta gani ila huo ni mtaji mzuri sana kwenye biashara kama utakachokifanya utakuwa umekifanyia upembuzi yakinifu.
Nipo mkoani mkuu nafanya biashara ya mazao kwa muda mrefu ila nimeona nihamie kariakoo ila kwa biashara tofauti sio hii tena
 
Nipo mkoani mkuu nafanya biashara ya mazao kwa muda mrefu ila nimeona nihamie kariakoo ila kwa biashara tofauti sio hii tena
Nitakupa angalizo mkuu.

Kama huko ulikokuzoea unaona kuna mwanya wa kutoboa komaa huko huko Kariakoo ina kawaida ya kuwapoteza watu kwenye game (lengo siyo kukutisha),labda utumie formula ya kugawa mtaji mmoja ubaki kwenye fani zoefu mmoja kwenye fani ngeni.
 
Binafsi nahitaj Connection na wauzaj wa Electronics Na Vifaa Vya Baiskel Apo Mjini K/Koo msaada Tafadhari.[emoji1488]
 
Wala hutowaona hapa wakijitetea.....
Mtawasifia, mtawaponda wala hutowaona wakijifungulia nyuzi humu.
Ukabila hauna msingi wala uhusiano na mafanikio ya mtu.
Kuna wakinga ni wala Unga tu, kuna wachaga ni walevi tu warabu vile vile.
Anafanikiwa mtu yeyote analost mtu yeyote.
Ukimaliza Kusema sisi wakinga/wachaga tuna hivi. Ondoa wingi weka umoja iwe mimi nna hivi.......
 
Kugawa mtaji kwakweli naona pesa haitatosha kwasababu hata huo mtaji niliokuulizia sio wote wangu si unajua huku mikoani kuna namna fulani ukijiweka watu wanakuletea akiba zao uwatunzie wakishauza korosho zao
 
Hapa kadri watu wanavyozidi kuamka nakuambia itakuwa kazi mno kununua ama kuchangia mchaga Mana wao huwa hawanunui kwa wengine Bali kwa kabila lao tu na sifa zao. Ni suala la muda tu watu watakwepa biashara zao. Kama iyo kampuni ya mapembelo na gnm so mtu atatumia mapembelo atasema wachaga tayari wanayo pesa Hakuna haja ya kuwaongezea ngoja tuwape walio masikini.
Ni kweli wapo juu Ila sio kuleta dharau na kujiona kuwa wao Ni Bora kuliko wengine,utadhani Kama waliamka wakajikuta wanayo hayo maghorofa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…