Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

Ni mazoea mabaya sana kupenda kula mayai kwa wingi na mara kwa mara!

Ni kwa bahati mbaya sana kwenye jamii ama hawana ufahamu juu ya maswala ya lishe salama au wengine wanafahamu athari ya kula mayai mengi mara kwa mara lakini wanapuuza miiko!
Mkuu kuna madhara gani kula mayai ya kienyeji mbona sijawahi sikia boss?!
 
Uko vizuri mkuu Mimi napenda kula ila kupika ndo kasheshe ile gesi mtungi mdogo huwa unakaa hata miaka miwili nisipopata mtumiaji huwa siitumii
 
Hapo chini ni list ya baadhi ya mbogamboga, we inaonyesha unapendelea nyanya na kitunguu zaidi.😜

Nyanya,
Kitunguu,
Hoho
Pilipili
Tango
Ndimu
Tembele
Kabichi
Mchicha
Mnafu
Bamia
Ngogwe
Biringanya
Chegere
Harage bichi
Chinese cabage
Sukuma wiki
Etc
 
Napenda sana kujipikia ndizi mshare na nyama. Kingine ni wali na maharage ya nazi 🀭
zamani hizo niko chini ya himaya ya wazazi hamna chakula nilikua sipendi kula kama ndizi,mpk naondoka nyumbani kila mtu anajua sipendi ndizi,lakini sasa hivi sijui ni maisha sijui nini ila nilijaribu jifunza pikaa ndizi tangu hapo hadi leo ndizi ni one of my favourite food.

hasa zikiwa za nazi na zaidi nizipike mwenyewe,nilimpkia mama angu 1st day ananitembelea kwangu tangu nitoke home alifurahi na hakuamini alihisi ni ndoto. Ndizi tamu sana na ndio mana ni moja ya vyakula gharama ktk kuvipika ili vitoke vitamu.
 
Hivi Kuna kitu gani najua kupika zaidi ya chai!! Tena sometime huwa chai inakuwa na mabuja sijui yanatokeaga wapi!.. wataalum hebu nijulisheni hili nakosea wapi
Utakua hauko serios mkuu,chai au uji?!
 
Uko vizuri mkuu Mimi napenda kula ila kupika ndo kasheshe ile gesi mtungi mdogo huwa unakaa hata miaka miwili nisipopata mtumiaji huwa siitumii
zamani hizo nilinunua jiko la gesi ila niilikua nalitumia kuchemshia maji ya kuoga tu lkn baadae niliona ni ujinga nikaanza jifunza kupika na msosi wangu wakwanza pika ni CHIPS japo nilipika kau kau chipsi ila mwanzo mgumu.
 
zamani hizo nilinunua jiko la gesi ila niilikua nalitumia kuchemshia maji ya kuoga tu lkn baadae niliona ni ujinga nikaanza jifunza kupika na msosi wangu wakwanza pika ni CHIPS japo nilipika kau kau chipsi ila mwanzo mgumu.
Kupika najua ila muda na kampani ndo shida
 
sili wala sigusi wala kukaribia

hoho
nyanya chungu(ngogwe)
bamia (mlenda kwa ujumla)
biringanya

hizo vitu sigusi kabisa lakini naweza kupika kitu ambacho siwezi pika wala sitokaa nitake kupika ni mlenda,lakini hizo ngogwe,bamia,biringanya kichanganya pamoja ukapika ni mboga ambayo mama angu mzazi anaipenda sana kula na ugali.

ninapopata mgeni nyumbani nikipka dagaa huwa naweka ngogwe au biringanya lakini kwenye kula nampakulia vyote mgeni mimi nakula dagaa tupu.

napenda mboga zote za majani kasoro majani ya maboga (sijawahi yaelewa kila nikijahdi kuyaelewa inakataa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…