Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,430
- 11,813
mkuu kuna madhara gani kula mayai ya kienyeji mbona sijawahi sikia boss?!
Mayai yote yakiliwa kupita kiasi yana madhara bila kujali kama ni ya kienyeji au yakisasa [emoji108][emoji108]
Siyo kwa kuwa ni ya kienyeji basi ndiyo mtu atifue anavyotaka la hasha!
Tena mayai ya kienyeji ndiyo yana nguvu zaidi kwa hiyo na hatari yaweza kuwa kubwa iwapo yataliwa bila kiasi.
Yai la kienyeji moja tu laweza tosha kwa wiki kutoa virutubisho vinavyotakiwa toka kwenye yai.
Sasa mtu anapokula mengi mara kwa mara huoni ni hatari kubwa ?
Mwili unamejengwa kwa uwiano kwa namna ajuavyo Mwenyezi Mungu mwenyewe.
Kila hitaji kwa kiasi , inapotokea vingine vikizidi mahitaji baada muda husababisha mwili udhaifu.