Mbona Azam UTV hawaoneshi mpira leo?

Mbona Azam UTV hawaoneshi mpira leo?

Naelewa sasa kwa nini Vodacom Tz mliletewa MD Mkenya tena mwenye shahada ya Lishe sijui mapishi.

Cowards everywhere,hivi mantiki ya kufungia channels zingine zinazoonesha mpira huwa ni nini hasa?

Hamtaki ushindani au?
Ni upumbavu kabisa
 
Matangazo yao yalikuwa yanaeleza kwamba wataonyesha mechi zote. Leo hawaonyeshi Mali na Ivory Coast, tatizo nini?
Cha kushangaza wamezifunga KBC/UBC ambazo zinaonyesha.
Wako msibani wamepoteza waajira saba kwa mpigo kwenye ajali
 
Wako msibani wamepoteza waajira saba kwa mpigo kwenye ajali
Kwani ni msiba wa tz nzima? Si msiba wao? Sisi misibabyetu huwa wanalia? Si hawatutambui kabisa? Sikatai, ajali inasikitisha lkn huo sio msiba wa tz nzima,namaanisha sio kila mtu ni mfuwa hapa.
 
Ndipo hapa hata YESU alisema acha wafu wazike wafu wao
Sio kila mtz amefiwa hapa,huo ni msiba wao,kutuzimia tv haimaanishi wanajali sana, wangekuwa wanajali angewapandisha ndege mbwiga huyu
 
Jamaa wamekata matangazo ya soka kwani soka ni sherehe kumbukeni tumelipia hii huduma sio msaada au kama vipi kateni matangaza sio mtuletee mziki ya kihuni


Au mruhusu matangazo ya KBC na UBC tuomboleze wote huu ni kutukomoa na miziki
Hivi star time Chanel ipi inarusha mpira jamani nisaidieni game ifwatayo Ghana na Tunisia niione utv maombolezo
 
Stupid AZAM, yaani mavipindi yote mmeyaacha yaendelee kasoro mpira tu..mmezingua big time
 
Azam,poleni sana kwa msiba. Ajali iliyotokea Igunga. Lakini mtaniwia radhi,pamoja na kusikitika sana na msiba huu,mlitakiwa Utv Mount she mpira, channel zingine ndio mngelia msiba. Huo siosiba wabtaifa, tumelipia king'amuzi tulikuwa na haja ya kuona mpira Utv.

Kutoonyesha mpirabhaimaanishi mmelia sanaaa msiba, sisi wenzenu tumefiwa sana lakini misiba huwa sio ya taifa. Wengine hapa tunapoandika ni yatima.

Jueni sio wote wanaolia,wengine walitaka kuona Afcon kwasababu tumelipia 28,,000 kwenye hulo luking'amuzi lwenu lwa kijinga. Sifuri kabisa.
Teh.....Basi wangezima tv nzima
 
Kupitia uzi huu nimegundua wanaopondaga Azam Tv wakizuga wanamiliki Dstv kumbe wengi wetu tunadowea Afcon ya bure kutoka Utv yaani Kitonga.

Wabongo mnabidi mfahamu hili, Televisheni za Taifa kama Rwanda Tv, Uganda Tv na KBC huwa wanarusha michuano hii bure lakini kwa masharti matangazo hayo yasiwe nje ya nchi zao. Ndio maana Azam Tv anazipiga pin wakati wa mechi zisionekane huku Tanzania. Kama ambavyo Utv hii ya Azam Tv ambayo tunaangalia Afcon hapa Tanzania haipatikani kwa nje ya Tanzania mpaka hapo michuano itakapoisha.

Poleni Azam Tv kwa msiba ila next time inabidi muwe na plan B kwani kwa kitendo cha leo kimewapunguzia credibility kubwa sana.
 
Matangazo yao yalikuwa yanaeleza kwamba wataonyesha mechi zote. Leo hawaonyeshi Mali na Ivory Coast, tatizo nini?
Cha kushangaza wamezifunga KBC/UBC ambazo zinaonyesha.
Nadhani ni maombolezo labda !
 
Nilidhani ni msiba ndio sababu (japo havina mahusiano)

Lakini nikashangaa matamthilia yote yanaoneshwa

Nadhani hawa jamaa nao hawajielewi
 
Wamezuia mpira tu lkn sinema zetu wameachia..sasa ndio kuomboleza gani?! Halafu watu wamelupia huduma unawakatia vipi kiholela tu?! Bahati mbaya akafa mmiliki wa azamu si ndio watazima na mitambo kbs.
 
Wabongo bure kabisa

Dunia haiwezi kusimama kisa kampuni imepoteza wafanyakazi

Fine wao kupitia UTV wanaomboleza basi wangeziachia zile channels zingine kwenye king'amuzi chao zinazoonesha mpira badala ya kuendelee kuzifungia.
Hata alipofariki mmiliki wa ITV mzee Mengi, haikuwa hivyo! Je siku akifariki Bakhresa, si ndiyo itazimwa kabisa!
 
Ulishawahi kuona lini superspot wanakata matangazo eti sababu ya kuomboleza. kuomboleza hatukatai ila hamuwezi kuacha kuonyesha AFCON, kuna channel nyingi chagueni nyingine. La sivyo mtapata double impact huku msiba kule mnapoteza wateja
 
Back
Top Bottom