Nina binti mwenye miaka 4 na miezi 7 sasa ! kutokana na uwezo wake wa kuchnaganua mambo nilijua ataanza shule akiwa na miaka 5 tu ! Lakini cha kushangaza amekuwa mzito ,hadi sasa hajajua kusoma hata maneno ya kawaida kama baba mama bibi nk !Cha kushangaza ni uwezo wake wa kushika mambo nje ya darasa ! mFANO ANAWEZA KUELEZEA HABARI ALIYOONA KWENYE TV ! na akaichambua kidogo mfano ...atauliza hivi kwa nini wanaoua albino hawakamwatwi !
Au waziri mkuu Pinda ameseama asali ni chakula bora! Au mimi nampenda Rais Obama tu ! Na anajua kuwa sasa hivi kuna mgogogro wa katiba kati ya CCM na UKAWA! Mfano mwingine ni unapo muomba kusali wakati wa kulala ataongea hadi unaogopa! juzi alituacha hoi alipoanza kunukuu maneno ya Bibilia ...Kama yesu alivyosema leteeni mizigo niitawatua ,waacheni watoto wadogo waje kwangu hapo alikuwa amechomekea kuwaombea albino wanaouawa na kujiombea yeye na mdogo wake wataalamu nisaidieni uelewa huu uhamie pia darasni kwenye hesabu na kusoma kwani wakati mwingine nikimfundisha hunigomea kwa mfano nikimwambia hii j yeye hinibishia na kusema hii ni m ,akiona unamzidi atakuuliza kwa nini ni j!