Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

Babe la mji

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2019
Posts
983
Reaction score
2,058
Kwa muda mrefu tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawa ndugu zetu kutoka Zanzibar wamekuwa hawaridhishwi na huu muungano, inasemakena hadi Rais wa kwanza wa Zanzibar alishawahi sema muungano ni kama koti likikubana unalivua.

Pia nakumbuka awamu ya 4, Rais akiwa Kikwete kuliibuka wimbi kubwa sana la wanaharakati kutoka Zanzibar wakiongozwa na jumuia ya UAMUSHO wakidai Zanzibar inatakiwa kuwa huru eti kisa viongozi wao wanachaguliwa kutoka Tanganyika.

Lakini jambo la ajabu awamu hii ya sita ni kama hakuna tena hizi harakati za kuvunja muungano wetu mtukufu sasa najiuliza je, shida ilikuwa nini kwa hizi harakati na imekuaje awamu hii zisisikike tena? Au ulikuwa ni unafiki tu wa wanasiasa na sasa hivi wameona huu muungano unawanufaisha na wao!

Kwa mtazamo wangu muungano huu Zanzibar ndiyo wana manufaa kuliko Watanganyika hivyo wanapaswa kuupigania ili uendelee na wao wazidi kunufaika.

Mzanzibar ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika wakati Mtanganyika hana hiyo haki Zanzibar. Je, nani hapo ananufaika? Nawaomba tena Wanzanzibar waache unafiki huu muungano wao ndiyo wanufaika.

MUUNGANO UDUMU MILELE.
 
Sasahivi wanakula hawawezi kuongea, ngoja mlo uishe kama yaliyomtokea polepole huoni now ana bwatabwata.

Ila huu muungano wa hovyo sana eti muungano wa nchi mbili ila kuna serikali mbili, moja kupe nyingine shamba la bibi CCM mnatukosea sana, iko wapi Tanganyika?

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa mtazamo wangu muungano huu Zanzibar ndiyo wanamanufaa kuliko Watanganyika hivo wanapaswa kuupigania ili uendelee na wao wazidi kunufaika.
Huu ni mtazamo wako. Unayo haki ya kutoa mawazo kwa mujibu wa katiba ya JMT na umeitumia ipasavyo. Hali halisi ilivyo haiko hivyo unavyoitazama.

Wazanzibari bado hawaridhiki na uendeshaji wa mambo JMT. Hivi Sasa kuna watu wanapigania haki za Zanzibar na bado hawajasimama. Unajaribu kudanganya ili Wazanzibari wabweteke ila wanaendelea.
 
UAMSHO walikuwa ni raia wa kawaida tuu, sio wanasiasa kama unavyotaka kuamini. Moja ya sharti la kutoka kwao jela ni kutoendelea na harakati zilizowapeleka ndani.

Naona kama unataka kuwalisha maneno wazanzibari. Hio ardhi na vitunguu maji ndio umeona hoja ya wazanzibari waridhike na kupoteza utambulisho wao ? Ni kweli wanapenda urojo na viazi (potatoes) vinahitajika na vinatoka Tanganyika, lakini sidhani kama ukivunjika muungano ndio wakulima wa Tanganyika watasusa kufanya biashara!

Kama muungano una faida na unahitajika hakuna cha kuogopa ni kupeleka kura ya maoni tuu ili wananchi wauridhie. Nchi nyingi zenye kujiamini zilishafanya hivyo mfano Ugiriki iliuza wananchi wake na wakakubali kuendelea na muungano wa ulaya.

Kama faida ni nyingi basi hakuna shida hio kaka, lakini naona kama unajitekenya na kujifurahisha. Iko wazi Tanganyika ndio anapeta na Nyerere ndio amelazimisha. Watu tunaishi kama tuko kwenye open-air prison (check-points kila 5km) halafu unakuja na hoja za vitunguu ? Hata Palestine chini ya Israel hawana checkpoints nyingi kama Zanzibar.
 
Mbona hujasemea awamu ya tano? CCM wamefanikiwa kuzima hilo vuguvugu kupitia dalali wao Zotto Kabwela, ila ni kwa muda tu wakiwa wanajipanga waibukie tundu gani.
 
UAMSHO walikuwa ni raia wa kawaida tuu, sio wanasiasa kama unavyotaka kuamini. Moja ya sharti la kutoka kwao jela ni kutoendelea na harakati zilizowapeleka ndani...
Umenena vema, lakini hoja ni kwa nini vuguvugu la kudai Zanzibar huru limefifia?

Kwa maandiko yako mazuri, naamini unalo la kusema juu ya hoja hiyo.

Mimi, Mtanganyika, nafikiri Wanzibari wamebadilisha 'strategy'.

Wanadai Uhuru wao kimya kimya.

Kwanza kabisa, Mtanganyika asipewe wala asinunue ardhi Unguja, maana Tanganyika ni Nchi tofauti na Unguja.

Kodi ndani ya Unguja, ni tofauti na Tanganyika.

Na sasa mikopo inasainiwa na Wizara ya Fedha ya Tanganyika, tunagawana lakini wakati wa kulipa, miaka 20 ijayo, hatujui mlipaji atakuwa nani.

Ukiangalia humu Jamii Forums, manung'uniko ya Muungano yamehama kutoka Unguja, yamehamia Tanganyika. Hili ni jambo jema, ili pande zote za Muungano tuwe na uelewa wa pamoja.

Na jibu lake lake liko wazi.

Tunahitaji kuwa na Makubaliano yanayokubalika pande zote, bila kulazimishana.

Tunahitaji Katiba Mpya.

Katiba Mpya ndiyo Uhai wa Muungano huu.
 
Sasahivi wanakula hawawezi kuongea, ngoja mlo uishe kama yaliyomtokea polepole huoni now ana bwatabwata...
Niliwahi kusimuliwa na Mzee mmoja ambaye alikuwemo kwenye Bunge la wakati wa Muungano, kisa kimoja cha utani kuhusu Mzee Abeid Amani Karume, mara tu baada ya Muungano, mwaka 1964.

Kisa hicho kinasema kuwa, mara baada ya Muungano, Mzee Karume aliulizwa na Wazee wenzake Zanzibar, kwenye Bao, kuwa imekuwaje amekubali kumezwa na Mwalimu Julius Nyerere?

Mzee Karume akawajibu Wazee wenzake, kuwa, "Yakhe, Julius nishamzidi akili. Yeye akija kwangu, (Unguja), anaishia Sebuleni, wakati miye nikienda kwake, (Tanganyika), naingia mpaka Chumbani anakolala".

Na kweli.

Mzanzibari anatutawala Watanganyika, kwa kila kitu, kama Rais wa JMT, wakati Mtanganyika hawezi kuwa Rais wa Unguja, asilani.
 
Kwa muda mrefu tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawa ndugu zetu kutoka Zanzibar wamekua hawalizishwi na huu muungano, inasemakena hadi Rais wa kwanza wa Zanzibar alishawai sema muungano ni kama koti likikubana unalivua...
Kelele zinajitokeza pale tu mwanadamu asipopata kile walichokubaliana. Hivi kama TANESCO ingetupa umeme 24hrs 7days kwa siku30 bila mgao, hivi kelele zingetokea wapi? Kwa vile mkataba wetu kati ya mtanzania aliyeweka umeme na TANESCO, NI KUWA TANESCO atagawa umemenao watapata malipo kwa kila kiwango cha umeme wanachopata.

Tatizo kubwa kati ya Tanganyika na Zanzibar ni kitendo cha Tapeli Nyerere kubadili kila kilichopo katika mkataba mpaka kuiweka Zanzibar katika hadhi ya mkoa kama Mbeya, Mwanza, Kigoma au Mara. Hili ni kosa kubwa sana. Angalia hata mijadala inayoendeshwa katika TV, media na magazetini- Utasikia mbona Mwanza ina wakazi wengi kuliko Zanzibar, eti inakuwaje Zanzibar wapate mgao mwingi kuliko Mwanza - Du Nyerere katuweza na Nyerererism. Kama ni hivyo Kwanini hatusherekei siku ya Muungano kati ya Mwanza na Tanganyika? Bado Elimu kubwa inahitajika! Watanzania tuna majibu RAHISI KWA MASWALI MAGUMU SANA.
 
Back
Top Bottom