MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 595
Mie sioni kama zimekufa wala kufifia, kama mzanzibari msimamo wangu juu muungano uko pale pale. Sijawahi kuunga mkono wala kupenda muungano, wala sioni faida yake yoyote.Umenena vema, lakini hoja ni kwa nini vuguvugu la kudai Zanzibar huru limefifia?
Kwa maandiko yako mazuri, naamini unalo la kusema juu ya hoja hiyo...
Naamini katika mashirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar, sawa na nchi nyengine yoyote ile kama Kenya, Uganda, Oman, Comorro n.k. Mashirikiano baina ya Zanzibar na taifa jengine lolote yasiathiri utambulisho wa mzanzibari wala utamaduni wake kama taifa huru.
Hakuna ulazima wa muungano baina ya nchi mbili hizo, zinaweza kushirikiana na kila moja ikafanya shughuli zake bila ya msuguano au muingiliano uliopo sasa ambao umekuwa kikwazo kama sio kisiki!