Mbona hizi dini zinachanganya?

Mbona hizi dini zinachanganya?

Mungu hayupo mkuu.

Angekuwapo watu wasingeijua internet ya bando ikoje.

Kila mtu angekuwa anagonga unlimited ya kampuni ya simu na unlimited ya WiFi kama mimi tu.

Kama yupo, kwa nini anipendelee mimi nisiyemuamini halafu wanaomuamini wengine wawe wananuka umasikini hata bando wapate kwa manati na wengine wana viswaswadu vinepasukapasuka vioo ni hatari kwa afya zao lakini wanadunda navyo tu?
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tuendelee kutamba na hizi pumzi tulizochukua mkopo tena mkopo wenyewe kausha damu ile ya mtu hulali kama hujarejesha rejesho.

Ukiwa mzima huumwi hata ukucha mkononi umeshikilia device yako charge 70% bundle la kutosha mfukoni una cent mbili tatu za kubadili mboga huku kichwani ukihisi una akili za kutosha aah mbona wewe mwanaume!,ikiwa sijui second tano mbele nini kitanitokea nina nidhamu mno na kinywa na vidole vyangu hasa wakati huu teknolojia illvyoenea.
Mwisho wa yote ni kifo mkuu.
Ujizuie, usijizuie, mwisho wa yote ni kifo.
 
Mungu aliumba ulimwengu mzuri tu ila walimwengu ndio wanauharibu
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakuumba ulimwengu ambao walimwengu hawangeweza kuuharibu?

Aliweza kuuumba hivyo, lakini hakutaka tu? Kama aliweza, je, kweli ana upendo wote?

Au, hakuweza kuumba ulimwengu hivyo, ila alitaka? Kama ni hivyo, je, ana uwezo wote?

Na kama aliweza na alitaka, kwa nini tunaona ulimwengu ambao walimwengu wanaweza kuuharibu?
 
Mungu hayupo mkuu.

Angekuwapo watu wasingeijua internet ya bando ikoje.

Kila mtu angekuwa anagonga unlimited ya kampuni ya simu na unlimited ya WiFi kama mimi tu.

Kama yupo, kwa nini anipendelee mimi nisiyemuamini halafu wanaomuamini wengine wawe wananuka umasikini hata bando wapate kwa manati na wengine wana viswaswadu vimepasukapasuka vioo ni hatari kwa afya zao lakini wanadunda navyo tu?
Inasikitisha Mungu anakuwa na upendeleo 🤣🤣 Mungu anakuwa na sifa na tabia za kibinadamu kabisa 🤣
 
Inasikitisha Mungu anakuwa na upendeleo 🤣🤣 Mungu anakuwa na sifa na tabia za kibinadamu kabisa 🤣
Eti Mungu ana taifa teule analisaidia lile taifa teule lake liwachape mataifa mengine kwenye vita.

Mpaka hapo hujajua tu kuwa huyo Mungu katungwa na hao watu wa hilo taifa teule tu? 😂😂😂
 
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakuumba ulimwengu ambao walimwengu hawangeweza kuuharibu?

Aliweza kuuumba hivyo, lakini hakutaka tu? Kama aliweza, je, kweli ana upendo wote?

Au, hakuweza kuumba ulimwengu hivyo, ila alitaka? Kama ni hivyo, je, ana uwezo wote?

Na kama aliweza na alitaka, kwa nini tunaona ulimwengu ambao walimwengu wanaweza kuuharibu?
Asilimia chache sana ameacha katika kufanya ulimwengu uwe perfect , nazani tumsifie Kwa kile kidogo alichofanya , Mungu fundi sana , tuna enjoy Kwa kidogo icho icho alichotuumbia ,
 
Eti Mungu ana taifa teule analisaidia lile taifa teule lake liwachape mataifa mengine kwenye vita.

Mpaka hapo hujajua tu kuwa huyo Mungu katungwa na hao watu wa hilo taifa teule tu? 😂😂😂
Kiranga leo j5 ya majivu umeenda kanisani lakini
 
Mungu ameumba binadam mwenye uwezo wa kum judge , ndio uone ni jinsi Gani yeye alivyo mwamba
 
PAPA Francis anapigania maisha huko ICU yaani hataki kwenda mbinguni [emoji1787]

Izi DINI sometime zinachanganya sana sasa papa hataki kwenda mbinguni nani anataka? kama papa hataki?...

Kwaresma NJEMA.
Mwandiko wako wako tu unaonyesha wewe ni wa mudi. Kwaresma huijuwi. Acha kejeli kwenye uhai wa mtu. Kufa wewe kwanza kama ni sifa.
 
Asilimia chache sana ameacha katika kufanya ulimwengu uwe perfect , nazani tumsifie Kwa kile kidogo alichofanya , Mungu fundi sana , tuna enjoy Kwa kidogo icho icho alichotuumbia ,
Hujajibu swali langu, umejitungia lako mwenyewe ukajibu unalotaka.
 
Wale wote wanaosema Kiranga anapenda sana hizi mada oneni sasa, Kiranga anaitwa sana kuchangia hizi mada.

Kwa sababu watu wengi wanapenda kusikia mawazo ya Kiranga kuhusu hizi mada.

Kuhusu dini kuchanganya watu.

Dini lazima zikuchanganye.

Kwa sababu zimejengwa katika misingi ya uongo.

Hao mapapa wamesoma falsafa na theolojia wengi wao kiukweli ni ma atheist ila wanajifanya wanaamini Mungu kwa sababu wanaona hiyo ndiyo njia ya ku control watu tu.

Ni vigumu sana kusoma falsafa na theology ukafika level ya kuwa Cardinal au Papa bila ya kujua mambo kama the problem of evil na kuwa na uelewa kuwa hizi dini ni kabobo tu.

Papa Francis aloulizwa swali la the problemnof evil na kasichana kadogo hapo Manila, kaliuliza kwa nini watoto wadogo wanaishia kujiuza kwa natatizo wakati kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote?

Papa alishindwa kujibu na akaishia kulipiga danadana za kisiasa tu swali hilo.

Nampongeza Papa kwa kukosa jibu, hapa angesema freewill ingekua mtifuano
 
PAPA Francis anapigania maisha huko ICU yaani hataki kwenda mbinguni [emoji1787]

Izi DINI sometime zinachanganya sana sasa papa hataki kwenda mbinguni nani anataka? kama papa hataki?...

Kwaresma NJEMA.

Aliyekwambia ukifa saivi unaenda mbinguni ni nani?
 
Back
Top Bottom