Instagram ni jini lile, linanyonya Mb kama Damu vile, usipokuwa na self control Instagram inaweza kukufanya ukajiunga bando kila siku.
Anyway me pia nilikuwa muhanga wa hilo, ili kuendana na huu ukata na vifurushi kuwa bei juu niliamua kubadirika.
Niliamua kuwa na self control tu maana japokuwa kweli tuna enjoy huko mjini Instagram ila hakuna cha maana tunachoingiza, unless otherwise uwe unafanya biashara za mitandaoni.
Nilijiwekea ratiba ya kuingia mjini Instagram, Kwa siku naingia mara 3 tu, kuanzia asubui ya 3-4 kisha natoka, narudi tena jioni ya 10-11 kisha namalizia na usiku wa sa 3-4
Target ikiwa ni kuvizia matukio muhimu, mfano kama Mimi napenda sana mpira so info za mpira kama zitatokea night nishalala, basi nitazikuta asubui sa 4, na kama zitatokea nishatoka huko nitazikuta jioni, na zikitokea jioni nazimalizia usiku, kwahiyo ni kama vile life cycle hivi.
Kwahiyo saizi natumia zangu Mbs 3300 kwa week, najiunga kila jpil, na kama ikitokea jpil imefika bado zipo basi naenda kuzimalizia YouTube kabla sijaunga zingine.