Status
Not open for further replies.

nergomafioso

Senior Member
Joined
Apr 3, 2024
Posts
109
Reaction score
284
Mimi kama kijana ninaye jitafuta bado ninaishi na mama yangu mzazi pamoja na mdogo wangu ambaye kwa sasa yupo kidato cha nne, dada yangu wa kwanza ameolewa yupo na familia yake yeye kaniacha miaka 6 ndio nikafuatia na mimi nimemuacha mdogo wangu wa mwisho kwa miaka 10.

Katika swala la maadili nashukuru mungu uyu bi mkubwa alijitahidi kutuweka kwenye mstari na alikuwa mkali mno unapoenda kinyume na matakwa yake, mkono ulihusika ili kuhakikisha tunakaa kwenye mstari sababu sisi wote tumelelewa bila ya baba, angalau mimi mshua kidogo alikuwa na nafasi nzuri kielimu na kiuchumi ila sikuwahi kupata walau malezi upande wa baba tulikuwa tukionana nilipokuwa mdogo kama na umri wa miaka kama 8-9 kushuka chini ila sikuwahi kujua kwanini hatuishi na baba.

Ukiwa mdogo sometimes na malezi niliyolelewa sikuwa mtu wa kujudge mambo kwa upana wake niliishia kuliacha hewani tu lipite as long as napata mahitaji yangu ya msingi ayo mengine watajua wenyewe.

Chekechea nilisoma shule za kulipia ila sikuwa na moment nzuri kabisa upande ule kwasababu ya lifestyle niliyokuwa nayo na shule uzungu ulikuwa mwingi mnoo nakutana na vitoto vya kishua, tambo zao na majivuno yakanifanya niingize miss kidogo na kucompare na maisha ya nyumbani ambapo kipindi hicho mama ni personal secretary wa wa wakili flani maarufu kidogo mkoani hapo na mdingi sikuwa najua kazi yake nikimuuliza mama ananijibu kwa utani mara kada wa ccm, mara aniambie tapeli basi shida tupu.

Mzee mwenyewe akija na kigari chake akiniletea na vizawadi nasahau maswali yangu yote naishia kufurahi tu na namuacha aende bila kunipa majibu ya kueleweka ya maswali yangu.

Kimbembe nikienda uko shule tulikuwa na kipengele cha kujitambulisha mwenyewe pamoja na wazazi wako na wadhifa wao apo ndo nakuwa na kiwewe na kukosa jibu zuri la kuwapa sababu nilikuwa naogopa sana kusema uongo kwahiyo ikifika sehemu ya kuwatoa wasifu wa wazazi upande wa mama ntatiririka vizuri tu ila ukifika upande wa mzee ntaishia kutaja majina yake na kabila tu maswali yanayofuata ningekaa kimya tu sasa ile kitu ilikuwa inawachekesha wanafunzi wenzangu na kuonekana sijui ilikuwa inanikata sana na kidogo kidogo nikaanza kuichukia shule. Jambo ambalo sitokuja kusahau mpaka uzee wangu kipindi hicho nasoma utaratibu ulikuwa kama shule nyingine tu za kawaida kwamba ukihitaji kwenda chooni unapaswa kuomba ruhusa kwa mwalimu husika anayefundisha tena kwa lugha ya kingereza "please teacher may i go out?" Mwalimu akikubali unaenda kiroho safi akigoma inabidi utulize mshono mpaka muda wa mapumziko.

Kuna kitoto kilikuwa kinaitwa Recho kina asili ya kiarabu na kaumbo kadogo ila kalikuwa kajanja sana chenyewe kanaweza kwenda chooni hata x2 kabla ya kengele ya break kugonga kalikuwa kanaomba ruhusa kama mara 3-5 mwalimu akigoma utashanga kimtu kimechomoka nduki hicho bila ruhusa kikirudi pale mwalimu akianza kugomba kanajua kujieleza na kiasi chake upande wa ngeli kaliijua si haba basi mwalimu mwenyewe atasanda.

Shida ilianzia hapo sielewi ni uoga tu au kuna kitu kilikuwa kinanisumbua ila mpalianda nilikuwa nikiomba ruhusa ninyimwe naogopa kutoka darasani ata kama mkojo umenibana to the maximum mi nilikuwa naendelea kuomba ruhusa mpaka nikubaliwe na mwalimu akikataa basi nitaishia kuomba mpaka mkojo unatoka nimekaa hapo hapo kwenye kiti mwalimu mdadisi ndiye angejua kama ichi kitoto kinakaribia kushusha mzigo maana sauti inabadilika kadri uvumilivu ulivyo nishinda, ningekibinya Kibamia kwenye kaptura mwishoe kojo lingenitoka hapo hapo kwenye kiti na ruhusa ndo zingekomea hapo na kujiandaa kwa aibu mpya🥺

Tulikuwa tunatumia viti vidogo vya plastic size kama ile wanayo tumia kutengeneza ma pot ya kujisaidia watoto wadogo miaka ya sasa, nikishajikojolea hapo ningeuchuna kimya mpaka wambea wa darasa waniripoti kwa mwalimu.

Nae mwalimu angeishia kunisema na kumtolea mifano Recho mtoto mdogo ananizidi akili hii kitu iliniumiza sana na tukio lilijirudia mara 2 ndani ya muda tofauti na ni tukio limeacha alama kwenye maisha yangu sababu shule ilipo na nyumbani umbali haukuzidi 2 km kwahiyo sikuwa napanda school bus asubuhi nilikuwa naenda na mmaza anapoenda kazini ila mchana hakukuwa na haja ya kufatwa na dada wa kazi sababu tulikuwa wanafunzi wengi tunatembea kwa miguu mpaka nyumbani wanaotoka mbali ndio walilipiwa usafiri na wazazi wao.

Kwahiyo ninapojikojolea ilinipasa kutembea hivyo hivyo mpaka nyumbani na hiyo siku wenzangu wangenitenga na kutembea la mmoko kama Rambo yupo vitani njiani nilikuwa nakutana na bullying kutoka kwa watu mbalimbali na maoni hasi juu yangu iliniumiza sana na ikanifanya niichukie shule kabisa ikifika asubuhi nakuwa mtata sana kwenye suala la kwenda shule bila sababu ya msingi.

Namshukuru mungu upande wa taaluma nilikuwa vizuri na niliwanyoosha haswa hao watoto wa vibopa sababu ya uelewa niliokuwa nao na nilikuwa miongoni mwa watoto ambao wangepewa nafasi ya kufanya presentation tunapoenda kwenye ziara za shule kama redioni au kwenye maonyesho mbalimbali ila sikuwahi kuwa proud na hiyo kitu mpaka nimemaluza ile shule na kuingia darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 7 ndo nakutana na viyande wenzangu watoto wa walala hoi katika shule ya kayumba...

Itaendelea chapter 2
 
Chapter 2
Maisha katika shule ya kayumba niliyafurahia mno uku nilikutana na watoto wenzangu kutoka familia mbalimbali ila nilienjoy ule muunganiko na kusahau mambo ya washua kule nursery nikakutana na waswahili wenzangu,
Nilipo kuwa darasa la kwanza hakuna mwanafunzi aliyefua dafu kitaaluma zaidi yangu sio kwa sababu nilikuwa bora kuliko wao ila ni vile nilikuwa nimefocus na masomo ukichanganya lugha ya kiswahili ndio lugha mama st. Kayumba ndani ya mwaka mzima nilipata alama nzuri katika mitihani na nilikuwa napata alama 100% katika masomo yote siachi ata nukta.

Kama ulivyo utaratibu wa shule nyingi nchini siku ambayo shule inafungwa basi wangetajwa wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kwa madarasa yote kuanzia darasa la 1-7 na zawadi zingegawiwa kwa wale top 3.
Mihula yote minne nilikuwa kinara mbele ya wanafunzi wenzangu na kupelekea kufahamika na walimu na wanafunzi wengine wa madarasa ya juu kama best student kwakuwa matokeo pamoja na ugawaji wa zawadi ulifanyika assembly na karibu wanafunzi wote walishuhudia zoezi hilo.

Mwaka uliofuata niliingia darasa la 2 tayari nikiwa nafahamika kiasi fulani kwa baadhi ya walimu na wanafunzi wa madarasa ya juu, kuna brother mmoja sikumbuki jina lake tumuite  davis yeye tulikuwa tunasoma nae shuleni hapo ila sikuwa najua anasoma darasa la ngapi, kuna namna alikuwa anatengeneza mazoea na mimi bila ya kuelewa nia yake ni nini kwa wakati huo ila sikuwahi kumtilia maanani, nilimuona kama watu wengine wanaohitaji kunifahamu zaidi kiundani shida yeye ilikuwa too much.

Jamaa sikuwa na story nae nyingi ila kila ninapokutana nae aliishia kuniuliza majina yangu kamili yote matatu nikishamjibu ndio angeridhika na kuniacha ila nilikuwa namtajia jina langu na jina la kati tu apo angeendelea kunipiga viswali mjinga mpaka nimpe na jina la ukoo ndo angeridhika na nafsi yake hii kitu sikuwa nafurahishwa nayo kabisa na style anayotumia kuniuliza ilikuwa inanikera haiwezekani mtu kila mnapokutana akusahau jina yeye hanaga story zaidi ya kumtajia majina yangu. Nilimuona mzinguaji ananidadisi au kunikejeli maana jina langu la ukoo limekaa kiutata kidogo wengi wanapolisikia huishia kucheka na kushindwa kulirudia mara ya pili, hivyo nayeye nilimuona kama ananichora tu na kunikejeri kutokana na majina yangu.
Ilifika muda akaanza kuja mtaani kwetu baada ya kufahamu niko na mazoea na dada mmoja jirani yetu yeye ni tomboy ila alikuwa muumini mzuri tu katika dhehebu la Roman Catholic na walifahamiana kwenye kwaya zao uko kanisani. Uyu dada mwanzo alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo akiwa na genge lake la matunda na ufundi baiskeli apo mtaani.

Uyu dada jina lake  Frola tulikuwa tumezoeana sana kwakuwa shule nilikuwa naingia mchana asubuhi nilipenda kuspend muda mwingi gengeni kwake kwakuwa nilipenda sana baiskeli ila sikuwahi kumiliki kwa wakati huo, alinifundisha ufundi baiskeli na akiwa na dharula aliweza kuniachia hiyo biashara yake na yeye akaenda kwenye mambo yake pasipo kufunga biashara kama alivyokuwa anafanya hapo awali.

Kuna mambo mengi hapo kati mengine ningependa niruke ili kuifupisha hii story ila kwa upande wa mtaani Frola aliimarisha bond yangu na Davis tukawa tumezoeana na akaacha tabia yake ya kunihoji maswali yake ya ajabu.

Siku moja jioni baada ya kutoka shule Davis alinifata atiwa na mwenzake mmoja wakiwa na baiskeli ya mountain bike na akaanza kunihoji maswali yake kama kipindi cha nyuma na nahisi alijua kabisa sipendezwi na yale maswali ila aliniambia nimjibu hatonisumbua tena, nilivyo mjibu niliona mwenzake amekuwa excited na majibu yangu na muda huo huo ndo akamtambulisha uyo mwenzake kwa majina yote matatu na kuniambia anasoma nae darasa la 6,
Nilibaki nimetoa macho pale nisielewe mambo yanavyoenda kwanini majina ya ubini yafanane, ikabidi nianze kumchunguza upya nikaona kuna baadhi ya vitu tunafanana kama sura ila kwa mbali, skin tone na masikio.
Akatumia muda huo kunitambulisha kwamba yule ni kaka yangu upande wa baba yangu , nilifurahi mnoo....

Itaendelea chapter 3
 
Chapter 3
Baada ya huo utambulisho ndio rasmi undugu baina yetu ulianzia hapo broo alionekana kunijali mnoo, mimi nilifikisha nyumbani taarifa nzima juu ya ndugu yangu huyu na mama aliishia kufurahi na kusifia watoto wa siku izi tumekuwa wadadisi mnoo ikaisha hivyo sikuwahi kujua nyuma ya pazia kiliendelea nini ila nilikuwa na utaratibu kupewa tsh. 10 au tsh. 20 kwa ajili ya matumizi ya shule ila nikienda shule broo yeye alikuwa anasimamia shoo nzima kwenye swala la chakula na alikuwa proud kunitambulisha kwa wenzake mimi ni mdogo wake, baiskeli yake akufika shule alikuwa anaifunga hakuna mtu anaigusa ila mimi pekee nilikuwa nawahi shule nikaichezee na hakuwa na noma juu ya hilo akaanza kuja nyumbani wakafahamiana na mama na muda mwingine alikuwa anakuja na mzee na anaweza muacha home alafu baadae akamfuata . Kumbe na yeye anajua kuendesha gari maana muda mwingine alikuwa anakuja nyumbani na gari ya mshua akiwa na rafiki zake na kuniletea vizawadi nilikuwa nafarijika sana, aliniambia tuna kaka yetu mkubwa kwa bahati mbaya sikuwahi kufanya nae mazungumzo yoyote ila nilimfahamu kwa kumuona kwa mbali sikuwa na ujasiri wa kumfata na kuongea nae lolote alikuwa mkubwa ila hakuwa amezidi miaka 25 kwa makadirio ya macho.

Mwaka huo huo mama alianguka ghafla kazini kwake na kuwahishwa hospital inasemekana presha ilikuwa inamsumbua na mwaka huo huo aliacha kazi alipokuwa anafanya na ikabidi atupeleke nyumbani kwa mjomba (kaka yake aliyemwachia ziwa) na hapo tukafanyiwa utaratibu mimi na dada yangu kupatiwa uhamisho na kuhamia shule za jirani karibu na kwa uncle na yeye alipata kazi mkoani singida katika chama cha ushirika ikabidi atuache hapo na yeye akaelekea singida.

Hii kitu iliniathiri sana kitaaluma ila baba na kaka walikuwa wanakuja siku moja moja kuniona nikawa nafarijika nakujiona hatupo wapweke mimi na sister ila habari mbaya zaidi kunasiku baba alikuja kunipa taarifa ya kwamba amehamishwa kikazi na ataelekea dar-es-salaam na familia yake yote itahamia uko . Habari hii ilinishtua sana kwakuwa mimi nilikuwa nimeshamzoea sana huyu ndugu yangu na hapo ndipo tulipotengana na mpaka leo hii sijawahi kuonana na ndugu yangu yoyote upande wa baba zaidi ya baba mwenyewe naye kwa nadra sana, na hivyo ndio nilivyo tenganishwa na ndugu zangu na hakuna yeyote aliyewahi kunitafuta maisha yakaendelea...

Kama mnavyojua uangalizi unaoupata kwa mzazi ni tofauti utakaopata kutoka kwa ndugu uncle alijitahidi kuhakikisha tunasoma na kwakuwa yeye pia alikuwa na watoto wawili wa kwanza alikuwa anasoma sawa ba dada yangu ila shule tofauti wa pili alikuwa wa kiume kama mimi yeye ndo alikuwa anaanza chekechea jumla alikuwa anasomesha watoto wa4 halikuwa jambo jepesi kutufuatilia watoto wote mkewe alikuwa mwalimu kapangiwa vijijini uko kuja hadi likizo au weekends mara chache.

Uncle alikuwa mkali mnoo na anaogopwa sana mtaani pale yeye ndio alikuwa msimamamizi wa shamba la familia lenye ukuwa wa ekari 11 na ndani kulikuwa na miembe na minazi ya kutosha, watu wa mtaani walikuwa wanaiba sana na yeye alikuwa akiwakamata anawachapa fimbo za kufa mtu wengine hadi kuzimia kabisa, ninavyo waambia alikuwa mkali namaanisha.

Pamoja na ukali wake haikunifanya niwe na hofu juu yake nikaanza tabia za utoro darasani na kutengeneza kundi ambalo tulikuwa hatuingii darasani tunazurula mitaani mpaka muda wa kurudi nyumbani na sisi ndio tunarudi kama tumetoka shule.
Nilipokuwa kwa uncle nilisoma darasa la 3 na la 4 hatimae tabia zangu za shule zikajulikana nilipigwa fimbo na kuomba msamaha siwezi rudia tena, na nilipomaliza mtihani wa taifa std 4 mama alinichukua tena nikaanza kuishi nae akiwa ndo amerejea kutoka singida na mdogo wangu wa mwisho na tukahamua wilaya fulani ndani ya mkoa huo huo ila ila tulimwacha dada kwa ucle kwakuwa alikuwa anaingia darasa la saba na uhamisho ulishindikana.

Kule kwa uncle ingawa ni mjini ila shule niliyokuwa nasoma ilikuwa na madawati mawili ambayo walikaa moniter na msaidizi wake mixer vilanja na vichwa vya darasa tuliobaki sakafu mixer vitofali vilihusika tulikuwa zaidi ya watoto 60 tunakaa chini, ila shule mpya niliyohamia ingawa ilikuwa wilayani ila walijitahidi kutoa elimu bora picha linaanza mkuu wa shule shangazi yangu,
Mama alimueleza vioja vyangu vyote nilimuahidi ntabadirika na kweli term ya kwanza mabadiliko yalionekana atleast top 3 nilikuwa sikosi ingawa bado kuna uhuni nilikuwa nao ila nilihakikisha uyu shangazi zisimfikie taarifa mbaya zozote walimu walitokea kunikubali kutokana na uwezo wangu kitaaluma nikachaguliwa kuwa kiongozi wa chakula kutoka WFP hapo shuleni baada ya kuleta vyakula vya msaada kwenye shule za msingi wilayani hapo.

Zilikuwa zinaingia tani za kutosha za mahindi, maharage na unga wa uji ule wa njano kutoka shirika la chakula na mimi pamoja na mwalimu flani kijana ndio tulikuwa wasimamizi kuhakikisha kila siku watoto wanakula na siku za kufunga shule tulikuwa tunaondoka na unga, mahindi na maharage kwa ajili ya familia maana stock iliruhusu . Wanafunzi walikuwa wanakula kande ila mahindi tulikatazwa yasikobolewe na maharagwe yalikuwa kama kokoto upande wa walimu walikuwa wanakoboa kidogo kwa ajili yao na mimi share yangu ilikuwa uko nikishasimamia wenzangu wote wamekula mkukuru vizuri na mimi ndio nile wenzangu walinionea wivu mnoo mpaka namaliza la 7 nshainjoy sana tu.

Mindset yangu ilikuwa inaniambia O-level siwezi soma wilayani hapo nikasema sasa ndio wakati wangu kuvuka border nikasome mabording mbona mzee pesa anayo hashindwi kunisomesha na nna wajomba waliahidi kunisomesha na nilipomaliza la 7 nikaenda kwa uncle mkubwa zaidi upande wa mama yeye ni daktari wa binadamu nikasoma ma pre form one na mainterview nikaenda kufanya kwenye shule kadhaa za private ila sikupelekwa walisema mazingira ya shule hizo hayakuwa mazuri mwisho wa siku matokeo yametoka nimefaulia shule ya kata jirani kidogo na nilipisomea primary nikashonewa uniform uko uko tanga wakasema nikaanzage kusoma uku nitahamishwa badae, sikuwa na hiyana ukichanganya darasa letu wote hakuna aliyefaulu kwenda shule za vipaji maalum wanangu wote walifaulia apo.

Uncle alikuwa mtu wa dini sana suruali zake zilikuwa kubwa mnoo kama lile kung'utio la mashineni na mimi nilishonewa suruali kubwa sana miguu miwili inapita yote kwenye mguu mmoja na akapiga mkwara nikienda kwa mama nisiifanye kichupa yaani modo nilinunuliwa vifaa vya shule nimerudi mkoani hata mama mwenyewe hakuafiki na ukubwa wa ile suruali nikamconvice tuipunguze akakubali ila ndo fundi kusimamiwa ili asiipunguze sana .
Mie tena baada ya kurudi nyumbani nikasema uyu mmaza asinitanie mimi ni brand siwezi vaa suruali lote ili nilikesha usiku niliipunguza na sindano ya mkono alafu nikaikata kabisa kabisa nyama ya ndani ili asilete gejageja asubuhi alinipeleka shule uku ananisema sana akaniambiwa nikiambiwa nimpeleke mzazi nitafute mzazi wa kumpeleka siwezi kumuaibisha kwa ujinga wangu. Baada ya kufanya malipo na kunikabidhi kwa muhasibu mama hakuwahi kurudi shuleni tena mpaka nimemaliza, ada na michango mingine alikuwa ananipa hela napeleka mwenyewe,
Nikaanzisha na vijitabia vipya ambavyo hakuwahi kuvijui kama niko navyo mpaka namaliza kidato cha nne....

Itaendelea chapter 4
 
Samahani mkuu...
Kuna mtu amedukua akaunti yako right..🤔
yani hata sielewi anataka kusema nn sisi mambo ya kukalia viti vya plastic yanatuhusu nn? kwa nn atufanye wehu kiasi hiki? anatuonaje sisi ni watu wazima na heshima zetu!!
 
Avumiliwe tu, ili tuone mwisho wake maana blah blah kibao.
 
Asa kwa Ujinga huu Vunja Bei anachaje kufilisika ...na Diamond anashindwaje kuwa tajir no1 nyoko zake duniani..🤬🤬
Kama hawa ndo wateja!!?
 
Kwenye uandishi Kuna kitu kinaitwa flash-forwarding, hapa mwandishi anatakiwa kuruka matukio yasiokuwa na umuhimu ndani ya story yake... Mambo ya kusema tulikula makande cjui na mambo km hayo unakuta hayana umuhimu sana kuyasisitiza...
Story haileweki inaenda wapi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…