Mbona kila msanii anamlalamikia tu Diamond, Kuna siri gani?

Mbona kila msanii anamlalamikia tu Diamond, Kuna siri gani?

Wints

Member
Joined
Dec 31, 2022
Posts
30
Reaction score
45
Toka Diamond atoke kimuziki hakuna mwaka haujapita bila msanii mwenzie yeyote kumlalamikia either anawaroga na kuwaibia nyota au anawafanyia figusu wasiendelee kimziki.

Wasanii kama Qchilla, mavoko, ommy dimpoz, tunda man, alikiba, nandy, aslay, Professor jay, darassa, harmonize etc wote wamemlalamikia kwa mambo hayo

Je, unahisi ni kwamba wote wanamsingizia au wote wana chuki nae binafsi au kweli ndo mambo yake kuiba nyota za wenzie?
 
Hamna kosa kubwa kama kutokujua kuwa ww mwenyewe ni sehemu ya tatizo. Kwani kila siku utakuwa unawalaumu na kuwa lalamikia wenzio walio fanikiwa.

Wasanii wa kibongo walivyo kama wachezaji wa kibongo, hawajui kujiongeza,hawajui kesho yao kwenye kazi zao (vision),waoga wa kuwekeza na hawajitumi hapo ndipo Mondi anapo wapiga gap.

Ndio maana wengi wamekwama wameishia hapa hapa ndani ila nje bado wamestack, mfano tu Mario kwa kifupi ktk miaka miwili kwa Tz yy ndiye msanii bora kwa bongo kishamailiza na kuishika game na hata kwa upande wangu album yake kwa mwaka jana kwangu ndio album bora,tatizo naye anaingia ktk kundi lile lile la wasiojua kuiljiongeza na kuwekeza kwenye kazi zao,hata hizi show tu EA kuzipata ana struggle na muda siku zote haumsubiri mtu ,muda wako ukipita ndio basi tena.
 
Wasanii wengi ni vilaza hawana elimu

Diamond sababu kawazidi mafanikio mbali.. wanamuona ndio amechukua nyota zao wote.. huku uhalisia wao hawana ubunifu kama diamond.
Hili ndio jibu lake.
Diamond anajituma sana, haridhiki haraka na habweteki kwa mafanikio aliyokuwa nayo.
Shida ya wasanii wengine wanaridhika haraka na wakishapata umaarufu kidogo wanavimba kichwa haraka na kujisahau ndio maana hawafiki mbali.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Hata wewe kazini unaweza kuwa unalalamika boss anakubania wakati unalipwa mshahara vizuri tu....watu hatupendi kufanya juhudi, tunapenda kitonga cha kushuka..
Kila msanii hapo unakuta anataka kolabo na Diamond ili auze zaidi...mbona wasafi inacheza nyimbo zao, wanataka nini tena?
 
Toka Diamond atoke kimuziki hakuna mwaka haujapita bila msanii mwenzie yeyote kumlalamikia either anawaroga na kuwaibia nyota au anawafanyia figusu wasiendelee kimziki.

Wasanii kama Qchilla, mavoko, ommy dimpoz, tunda man, alikiba, nandy, aslay, Professor jay, darassa, harmonize etc wote wamemlalamikia kwa mambo hayo

Je, unahisi ni kwamba wote wanamsingizia au wote wana chuki nae binafsi au kweli ndo mambo yake kuiba nyota za wenzie?
Baadhi ya watu waliodhulumu sana haki za wasanii walipata kuwepo, wapo kwenye uongozi wa domo.na nyoka haachi sumu.
 
Shida ya mtu siwezi chukulia ni furaha kwangu ila maisha yanapambaniwa eti walahi
 
Chiddy Benz anawaomba pesa ma Djs wakimnyima anatishia kuwapiga. Huyu ni Chiddy sio kama hawa wengine wana status zao angalau.

Diamond hatoi mikopo wala msaada kwa hao uliowataja au kuleta ushikaji katika kazi . Yupo seriously na Music.

Sasa huo uswahili wa kujuanajuana ukiukataa unakuwa adui wa watu wengi wapenda vimeo(kukopa na kuombaomba)
 
Back
Top Bottom