Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Mbona Moro uko katikati ya Dodoma na Dar lakini uko vizuri
what something special do Lindi Offer in between? kama mkoa hauna inachoprovide automatically huo mkoa hauwezi kuwa popular maana mafanikio huja kwa kuzingatia kiwango cha nguvu ya sumaku ya vivutio vilivyopo mwisho wa kunukuu.
 
Watanzania sisi ni washamba sana na malimbukeni na tusiojielewa; hivi tz hii ukiacha Dar kuna wapi kwingine kulikoendelea kiasi cha mtu kukesha akiponda sehemu nyingine?!!!!!!

Hivi makelele haya ninayoyaona ni ya watu kutoka sehemu hizi hizi za tz nilizotembelea na mimi au zingine?!!!!

Mikoa nane (8) ya nchi hii niliyowahi kufika na kuishi inanifanya nicheke sana baadhi ya commentsi humu.......
 
Ni viongozi kukosa maono (vision),ubinafsi,kuendekeza siasa , kulalamika ,kufuatilia maisha ya watu badala ya kufikiria na kuwa wabunifu:
1.Mji wa Lindi unapaswa kuwa na Bandari
2.Lindi ina beach nzuri zafaa kuwa na hotel za kitalii.
3.Michezo ya mbio za boti baharini zaweza kutangazwa na kufanyika Lindi na watalii wakaja na kuwepo mzunguko wa pesa.
4.Sijui hata kama maeneo ya uwekezaji yameanishwa na kama Mkoa wanatangaza fursa zilizopo Lindi.
 
Mikoa nane uliyotembea ni michache sana kwako kuijadili lindi
Nimetembea Tanzania yote kila mkoa , ni wilaya baadhi tu sijafika na nyingi ni hizi mpya ,
Lindi pamedorora , na maisha yake kama mtwara tu ni ghali ! Nimelala Guest house ya 25000 lindi , kitanda ni 4x6 na hakina neti maji ni ya kuchota na ndoo, tv ya chogo., hii sio miaka ya 90, ni juzi tu hapa zimepita siku 9 tu
 
Kweli mambo ya msingi yanayoweza kuipa miji hadhi hayafanyiki:
Mfano Miji mingi tuliyonayo mipango miji(master plan) sio kipaumbele hata kupanda miti tu tunashindwa kupanda, kuongeza barabara za lami zinazounganisha Wilaya katika Mikoa husika ni mipango ambayo haizungumzwi(Kama nchi imefunguliwa kibiashara,inatakiwa iende sambamba na kufungulia barabara kwa kuwekewa lami).
 
Ruangwa eneo ambako mke wangu ameajiriwa huko
 
Sumbawanga wao wamejukita sana katika kilimo mkuu ndio shughuli yao kubwa ya kiuchumi mkuu......

Pia ukilinganisha na iringa kama unavosema kumbuka iringa katika wilaya ya mufindi mji wa mafinga wao ndio wanaongoza kwa production ya mbao Tanzanian nzima unaambiwa 75% ya mbao if I'm not mistaken yatoka kwao....huwezi compare na Lindi ambayo pia ndio ina bahari as you claim kuwa inaweza kuwa chanzo cha mapato kama beach au Wenda hata kama bandari...lakini kumbuka kama anavyodai huyo mkuu aliyetangulia kuwa Lindi yazungukwa na Dar ea salaam na Mtwara Miji ambayo ina beaches nzuri na bandari nzuri kubwa luliko hata huko Lindi.....

Even if wakijenga bandari huko ngumu sana kuwa kubwa kama ya mtwara au Lindi

Issue ya morogoro kuwa mbona opo katikati ya Dar es salaam na Dodoma lakini inakuwa hali ya kuwa haipigiwi promotion Mimi nakataa....
Kuna miradi mingapi mikubwa ipo morogoro hali yakuwa Lindi haipo???

SGR imepita hadi Lindi pia????
 
Mkoa wa Lindi mlishakwama, usijifariji.
 
Mkuu "Sijaona" najua kwenu Lindi. Lakini huo ndio ukweli. Acha usemwe.
 
Morogoro inakua yes, lakin taratibu mnoo. Sijui lini Morl itakua JIJI.
 
Lodge moja niliwahi kufikia huko miaka ya 2010's mwanzoni hapo,lodge maji hakuna wakatuonyesha maji yaliyotumika kufulia nguo wakasema yako hapo kwny hio ndoo mnaweza kuyaogea, nikasema tu Hiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Lindi iko mwambao wa pwani (Factor kubwa kwa ukuaji wa miji/mji)
Lindi ina beach nzuri (biashara, utalii, uvuvii)
Lindi ina makumbusho ya majengo ya kale nayo pia utalii wa kihistoria
Bado ina ardhi na vinginevyo

View attachment 2307018
Huku ndiko kwa kwenda kukamatia fursa ,ni mkoa mzuri Wilaya zake zote zina fursa ya kila aina..

Lindi yenyewe na Mafia kuna beaches za kuzidi hadi Zanzibar wakasome.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…