Mbona Mbowe amesahaulika mapema hivi?

Mbona Mbowe amesahaulika mapema hivi?

Napenda kuwasalimu kwa jina la alietuumba. Ndugu zangu, ingawa inafahamika kuwa CCM na Serikali yake wana uzoefu, ujuzi na uwezo wa kucheza na saikolojia ya wapinzan wao kwa kuanzisha jambo baada ya jambo, lkn safari hii aisee wameweza kufanya jambo ambalo wengi hatukulitarajia hata kidogo katika kipindi hiki ambacho mh Mbowe analala mchongoma na masela mbali mbali kule keko. Ni kweli tumezoea kuyaona baadhi ya mambo ambayo CCM na serikali yake huyafanya kwa lengo la kuwapoteza maboya wapinzani wao, mfano halisi ni mwaka 2015 ambapo CCM ya mzee Kikwete walikuja na style ya "mchawi mpe mtoto akulelee". Na kweli style hii ilizaa matunda baada ya wapinzani kuingia mkenge kwa kumpokea mtoto huyo ili wamlee na matokeo yake ilikuwa ni ushindi mtamu kwa CCM, huku wapinzani wakishikana uchawi wenyewe kwa wenyewe. Sasa baada ya CCM kufanya yale iliyofanya mwaka 2015, safari hii tulijua hali ingekuwa tofauti. Lakini kwa weledi mkubwa CCM imekuja na Mbinu nyingine ya kutuliza hali kuhusu kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani mh Mbowe. Kwanza walikuja na swala la gazeti fulan kuleta taharuki, na pili wakamalizia na picha la Sabaya akimuhusisha hayati Magufuli katika kesi yake. Na kwahili naweza kusema wamefanikiwa maana wanaharakati wote waliokuwa wanampigania Mbowe aachiwe huku mitandaoni washaonekana kumtelekeza mwenyekiti wao na kuvalia njuga swala la Sabaya. Hii ndo CCM iliyomshinda hata Nyerere mwenyewe bwana!!
Kila anayekwenda kumuuliza kwa siri kama ni gaidi majibu anayokutana nayo aikifika mtaani anajisemea"mchuma janga hula na wakwao"....anapiga kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada kamalizia hivi:
"Lakini kwa weledi mkubwa CCM imekuja na Mbinu nyingine ya kutuliza hali kuhusu kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani mh Mbowe. Kwanza walikuja na swala la gazeti fulan kuleta taharuki, na pili wakamalizia na picha la Sabaya akimuhusisha hayati Magufuli katika kesi yake. Na kwahili naweza kusema wamefanikiwa maana wanaharakati wote waliokuwa wanampigania Mbowe aachiwe huku mitandaoni washaonekana kumtelekeza mwenyekiti wao na kuvalia njuga swala la Sabaya. Hii ndo CCM iliyomshinda hata Nyerere mwenyewe bwana!!"
Nenda kapate chanjo tafadhali.
 
Napenda kuwasalimu kwa jina la alietuumba. Ndugu zangu, ingawa inafahamika kuwa CCM na Serikali yake wana uzoefu, ujuzi na uwezo wa kucheza na saikolojia ya wapinzan wao kwa kuanzisha jambo baada ya jambo, lkn safari hii aisee wameweza kufanya jambo ambalo wengi hatukulitarajia hata kidogo katika kipindi hiki ambacho mh Mbowe analala mchongoma na masela mbali mbali kule keko. Ni kweli tumezoea kuyaona baadhi ya mambo ambayo CCM na serikali yake huyafanya kwa lengo la kuwapoteza maboya wapinzani wao, mfano halisi ni mwaka 2015 ambapo CCM ya mzee Kikwete walikuja na style ya "mchawi mpe mtoto akulelee". Na kweli style hii ilizaa matunda baada ya wapinzani kuingia mkenge kwa kumpokea mtoto huyo ili wamlee na matokeo yake ilikuwa ni ushindi mtamu kwa CCM, huku wapinzani wakishikana uchawi wenyewe kwa wenyewe. Sasa baada ya CCM kufanya yale iliyofanya mwaka 2015, safari hii tulijua hali ingekuwa tofauti. Lakini kwa weledi mkubwa CCM imekuja na Mbinu nyingine ya kutuliza hali kuhusu kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani mh Mbowe. Kwanza walikuja na swala la gazeti fulan kuleta taharuki, na pili wakamalizia na picha la Sabaya akimuhusisha hayati Magufuli katika kesi yake. Na kwahili naweza kusema wamefanikiwa maana wanaharakati wote waliokuwa wanampigania Mbowe aachiwe huku mitandaoni washaonekana kumtelekeza mwenyekiti wao na kuvalia njuga swala la Sabaya. Hii ndo CCM iliyomshinda hata Nyerere mwenyewe bwana!!
Wale diplomat jana walikuwa ikulu au wapi?
 
Wewe unapenda mipango yetu yote iwe wazi kwenu watesi wetu ,? Hamtafanikiwa, ni ajabu sema Mwenyekiti wa Chama ,na Chama chenye wafuasi ml 15 useme amesaulika, sijui unatumia vigezo gani?

Ni juzi wawakilishi wa nchi zinazowapa misaada, wametinga kisutu, mkaja na ngojela eti magari ya magereza mabovu , leo mnakuja na lingine

Nyie wabambe njaa mmealibu sura ya nchi, na sarikali ya awam ya 6 , alafu huyo mama anawachekea ,itoshe KUSEMA mmetimiza malengo YENU kumkwamisha huyo mama, mpaka mda huu mmefanya kuona kuongoza taifa Kama ni mzigo kumbe sivyo
Wafuasi milioni kumi na tano? Sijui umetumia kigezo gani kuja na hizo takwimu.
 
Kitendo cha kuandika mada kuhusu yeye ni dalili tosha kwamba hajasaulika! Umeacha kuandika kuhusu mama yako, ambaye ndo amesaulika unamwandika mwamba ambaye anatrend! Shame on you girl
 
Hapana Kila jambo hutokea kwasababu zake na kipindi chake
 
Unayohakika Dudumizi,ilikuwa ndio lengo kumbambikia ili asahaulike sio, ona hata mnaogopa kumtoa mwamba hadharani. 😆
Kama alibambikiwa au hakubambikiwa, mahakama ndo itaamua. RIP Chacha Wangwe na Ben SAA8.
 
Hahahaaa,muulize IGP kwanini aliitisha Press!Muulize huyo mama yenu kwanini alienda BBC kueleza aliyoeleza!
Kama si urais wa kuokota,Samia haingii kwa Mbowe hata theluthi moja!
Raisi alienda BBC au BBC ndo ilienda kwa raisi kule Ikulu?
 
Hakuna dili la ruzuku tena! Utampigania mtu ambaye hana pesa za kukulipa ktk mikutano na safari?
Nafikiri hii ndio sababu ya yeye kusahaulika kwa haraka sana. Waswahili wanasema "mkono mtupu haulambwi.
 
Back
Top Bottom