Hiyo meli ina uraia wa Tanzania. Ila mmiliki anaweza akawa sio mtanzania. Tanzania tuna usajili wa aina 2, huku bara tuna closed ship registration hii inaruhusu wazawa kusajili meli au mzawa awe na share kuanzia 59%.
Zanzibar wana open ship registration, mtu yoyote anaruhusiwa kusajili meli kule na itapeperusha bendera ya Tanzania. Meli nyingi zilizosajiliwa na wageni walipita kule. Baadhi ndio hizo, mnazoona mataifa mbalimbali. Usajili huu haumbani mtu kwa nchi kama Panama au Liberia unasajili meli online. Tatizo la usajili kama huu hauna usimamizi wa karibu kujua meli ulizosajili zipo kwenye status ipi