Jana nimeuza USDT 1 kwa pesa ya madafu Tzs2809. Hii ni kwenye crypto platforms.
Hapo unapata picha wapi Tzs inaelekea. USDT ni stable coin maana yake thamani yake ni sawa na US dollar.
Ok, sababu ya pesa ya Tanzania kwenda chini ni nchi kuendelea kushindwa vibaya kwenye kuzalisha na kuuza bidhaa au huduma nje ya nchi na sisi kupata pesa za kigeni.
Kamwe usidanganywe na wanasiasa.
Siku zote tazama namba.
1. Mwaka 2022/2023 tuliuza nje si zaidi ya $8bn. Unafahamu kiasi gani tulitumia pesa yetu kununua bidhaa au huduma nje? $16bn.
2. Lakini pia ukiangalia vizuri unagundua vile uchumi wetu ulivyo mdogo na umesinyaa. Mdogo sana. Kwa mwaka pamoja na kelele zote kwenye mahindi yatuuzi zaidi hata zaidi ya $100m.
3. Kiufupi Tz inawanufaisha watu wachache sana
a)umepata bahati yakuzaliwa kwenye familia yenye msingi mkubwa wa kifedha.
b) umefanikiwa kwenye biashara kwa hustle zako za jasho na damu.
c) Umeajiriwa kwenye kitengo na kazi yako ni kuiba pesa za umma, rushwa na ulaghai.
4. Tofuati na hapo, utaishi maisha yako kwa kiasi kikubwa kwa tabu na ikitokea hujapata nafasi yakuona watu wengine wanavyoishi vizuri, utaendelea kupigwa fix na wachache wanaonufaika kwa kukukandamiza na kukuipia kwa ujinga wako.