Mbona Total wameishindwa Tanzania, ingekuwa kampuni ya Kenya mngechekelea ila sasa wanahama wote

Hujui kinachoendelea wewe! Endelea kuhangaika na Covid-19 yenu huko ya TZ hayawahusu!
 
Jana wamefungua kituo cha mafuta tatizo uko Tanzania halafu unapiga kelele ngoja wp yako iishe kama itaongezwa
 
Mna siku 30 zingine za kua kama wanawali wanao subiri kuolewa
 
Tatizo kila mmoja wenu ana maelezo yake, kunao mnasema hiyo ilikua mojawapo wa vigezo kwamba kama watajenga bomba lazima wafunge biashara zote zingine, yaani mbona msitulie mpate spin moja ya kutumia.
Wewe read the advert on the newspapers utaelewa.........
 
Kwa ufupi sana wewe jamaa huwa unawashwa washwa sana Tanzania,na ipo siku utakunwa vizuri mno.
Wewe kila siku kushupalia mambo ya Tanzania wakati ya kwenu huko yanakushinda,watu wenye vijicho utawajua tu.
 
Wewe read the advert on the newspapers utaelewa.........

Anyway wewe huwa naona uko balanced kiaina kwenye mabango yako, sio kama waimba mapambio wa Lumumba, hivyo I will settle with your explanation, it's true some firms normally dispose of assets lacking strategic importance.
 
Opera News Tanzania

Get Opera News on Facebook.

JOIN NOW

[https://res]

Kampuni ya Mafuta ya Total, imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa inaondoka nchini kwakuwa imeanza kuuza baadhi ya mali zake.

Mkurugenzi wa Total nchini Tanzania, Marsha Msuya-Kilewo amesema kuwa tetesi hizo zimetokana na hatua ya kampuni hiyo kuuza baadhi ya mali zake, suala ambalo amesema ni utaratibu wa kawaida wa kampuni na halina uhusiano wowote na mpango wa kuondoka nchini.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa uuzwaji wa baadhi ya mali zake una uhusiano wa tukio la Total kununua mali za Kampuni ya Gulf Africa Petroleum Corp (Gapco) mwaka 2017.

Ameiambia The Citizen kuwa baada ya kununua mali zote za Gapco nchini, Total imekuwa na vituo vingi vya kiutendaji ambavyo wakati mwingine vimekuwa vikishindana vyenyewe vinapokuwa vituo vingi katika eneo moja.

“Tulifikia hatua ambayo vituo vyetu vya huduma katika baadhi ya maeneo vilikuwa vinashindana vyenyewe kwa vyenyewe. Uamuzi bora zaidi wa kibiashara katika wakati huo ulikuwa kuuza baadhi ya mali. Lakini kwa ufupi, Total iko Tanzania kwa muda wa kudumu, tupo sana,” amesema.

Madai ya kuwa Total inaondoka nchini yalianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuweka kwenye vyombo vya habari Septemba 1, 2020 kuwa inauza baadhi ya bidhaa zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…