Mbona uzalishaji umeme wa Julius Nyerere hatuoni umuhimu wake?

Kwani huo mradi ushakamilika na kuanza kufanya kazi?
 
Mlioko mbali na Siasa hamjui tu ni kiasi gani Siasa ina athari kiasi gani kwenye maamuzi mengi ya Nchi

Pamoja na uzalisha kuongezeka wa Umeme, lakini bado Umeme umeendelea kuwa wamgawo Nchi hii

Hizo bei za umeme kutoshuka

Mwanzoni walisema gharama za kuunganisha Umeme vijijini Ingekuwa 27,000 lakini leo hii gharama zimepanda hadi 330,000 🙌
 
Umeongea pumba sana bora ingekaa kimya
 
Unaweza kutuambia umeme umepanda lini na umetoka kiasi gani kwenda kiasi gani? Maana bei ya sasa ya 350-360 ninavyokumbuka iliainishwa mwaka 2017.


Pia Nchi hii kwa watu wa kipato cha chini wasiotumia zaidi ya unit 75 kwa mwezi wanalipa umeme bei rahisi mno, kama upo Kundi hili nenda Tanesco wakupunguzie bei, unit ni kama sh 100

Kwa Sisi tunaotumia zaidi ya unit 75 kwa mwezi bei ni roughly 350-360.

Ukicompare huko Duniani kwa Kaya za uwezo wa Chini I doubt kuna Nchi nyingi rahisi kushinda Sisi

Pia umeme wa Nyerere hautumiki sababu hakuna miundombinu, kujenga Tu Bwawa hakufanyi automatic umeme upatikane Nchi nzima, kujenga nguzo na miundombinu mengine mpaka ifike Nchi nzima kunahitaji matrilioni ya hela ambayo si wewe wala Serikali mwenye uwezo huo. Ni process itachukua miaka na miaka.
 
Nyie watu wekeni akiba ya maneno. Mmesahau mgao wa umeme? Umeme kukatika asubuhi mpaka jioni au jioni mpaka asubuhi maa tano kwa wiki? Mara ya mwisho lini umesikia mgao wa umeme? Na ujue tofauti ya mgao na umeme kukatika.
Umeme kuna uzalishaji na usambazaji. Bwawa limeongeza uzalishaji usambazaji ni shughuli nyingine ambayo itachukua miaka kukaa sawa. Ila kwa kweli Tanesco sasa hivi wanajitahidi.
 
Umeanza vizuri lakini umeharibu mwishoni kwa kusema kujenga bwawa hakufanyi kuwa na umeme.
 
Nilisema humu kipindi cha jpm kua yawezekana akawa na idea nzuri kuhusu bwawa la uzalishaji umeme! But kwa system ya utawala wa Tanzania ni ngumu mnoooo kupata umeme wa uhakika moja kwa moja cz humo ndimo kuna madili mengi san. Na pia hawa watu hawatak kufanya kila kitu kwa wananchi then kesho wakose cha kujinadi!!!
 
Nilitarajia kwa yale ma kilowati tulioambiwa itazalishwa hakuna mtanzania ambaye angakuwa anatumia gesi wala kuni. Umeme ulitakiwa uwe rahisi kuliko ulaya
 
Umeanza vizuri lakini umeharibu mwishoni kwa kusema kujenga bwawa hakufanyi kuwa na umeme.
Kama unahisi umeme unapanda daladala Sawa, Ile minguzo na distribution line ya Grid ya Taifa ukisoma kwa wataalam kwa kila km inacost mamia ya milioni mpaka Bilioni kadhaa tegemea na Eneo, halafu unahitaji kucover Maelfu ya kilomita, usione Serikali inanunua umeme nje kwa mikoa ya mpakani, ni Gharama kubwa Sana kusupply umeme.

Angalia hapa kama unataka kujielimisha namna umeme unavyokuwa supplied


View: https://youtube.com/watch?v=M50RamBzLX0&si=iLYlUnqiBixUgl1O
Kuna mradi unaitwa Taza, Unatoka Iringa kwenda Zambia kupitia Tunduma, umecost Dola za kimarekani si chini ya milioni 500 (zaidi ya Trilioni za madafu). So si shughuli ya kitoto kujenga hii miundombinu.
 
No, aliweza kushusha ghArama ya kuungamisha umeme kuwa 27,000 na ilifanya kazi, usitulishe matango pori

Na huyo huyo ndio alie pandisha malipo ya loarn board kutoka 9 - 15, na ndie alie Chota hela za Wastaafu huko NSSF mpaka mfuko ukateteleka na kuamua kuja na kikokotoo cha 45%.

Kizuri hakikosi kasoro.
 
Huo mradi unahitaji watu wenye akili nzuri ndio utaona faida yake, kwasasa tusubiri hadi CCM watakapoondoka madarakani.
 
Na huyo huyo ndio alie pandisha malipo ya loarn board kutoka 9 - 15, na ndie alie Chota hela za Wastaafu huko NSSF mpaka mfuko ukateteleka na kuamua kuja na kikokotoo cha 45%.

Kizuri hakikosi kasoro.
Alijitahidi kuwapa wale walio chini wapate mfano halisi ni kuunganishiwa umeme wa Tanesco kwa 27,000. Hii ililenga wenye kipato cha chini wapate umeme, Waliokuwa wanatoa milio kipindi cha Magu ni wale waliokwishapata,
Sasa kwa Samuya wanufaika ni walionacho [waliokwishapata],
unabisha nipe mfano 1 tu kumtetea. Sikubaliani na yote ya Magufuri, lakini ni bora X200 kuliko Samia
 
Tatizo Ni Pale Wahuni Walipojipenyeza Ndani Serikali Hii
Kwanza Wakapandisha Kuunganishiwa Umeme
Wakaweka Kodi Ya Jengo Tanesco Ndiyo Waikusanye
 
😭😭😭😭
 
Kuna wilaya moja hv inaitwa tunduru aisee ile wilaya umeme unasumbua kinoma, haipiti siku umeme haujakatika hata zaid ya mara 5 kwasiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…