Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mbona upo kimya sana kuhusu hili sakata la Naibu waziri wa katiba na sheria Pauline Gekul?
Dorothy Gwajima hujawahi kukaa kimya kiasi hiki linapotokea jambo la kuzalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia kiasi cha kijana mdogo kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa na Naibu waziri!
Dorothy Gwajima kama uliweza kujitokeza kwa mbwembwe za hali ya juu na kuwananga na kuwasema walimu eti kisa tu wameruhusu kuucheza wimbo wa Zuchu wa Honey. Mbona hili jambo la Gekul umekaa kimya kama vile hulioni?
Wewe huwa unajinasibu kuwa unapinga sana unyanyasaji wa kijinsia na hupendi kuona raia akifanyiwa kitendo cha kinyanyasaji. Sasa mbona hili la Gekul umekausha kimyaaaaa?
Zile mbwembwe zako za kwenye media hasa linapotokea jambo lolote la unyanyasaji wa kijinsi mbona kwa Gekul hatukuoni!
Mbona hutoi matamko yako ya mbwembwe nyingiiiiiiiiiiiiiiii kama tulivyokuzoea!
Kuna siri gani kati yako na Pauline Gekul mpaka "umeufyanta"?